bongo dsm.....Balozi na MR. II......dedication to you.... ila pole sana, na tunashukuru kwa taarifa.......
ALERT:
kama una hela kuanzia 100,000/= au zaidi, kama una vito vya thamani, simu za thamani, nguo za thamani,....chochote chenye kuweza kuleta ulaji kwa mtu mwingine...afu upo Dsm, maeneo ya Ubungo, Buguruni, Karume, Kariakoo, Posta......basi unatakiwa kuzungumza na wale ulioapanga kuzungumza nao kwa siku hiyo....usiongee, wala kuongozana...wala kumsikiliza..wala kupeana mikono na mtu mwingine yeyote ambaye humjui...........
Mkuu, yule gwiji mkuu tulipeana mkono. Tena baada ya kuhesabu pesa nilimuuliza kama pesa hizo ni legal na valid akasema nisiwe na wasiwasi. Nikamuuliza kwa nini duka liko kifichoni akasema lengo ni kukwepa kodi kidogo. Nikawapa ushauri wafanye biashara y wazi kwani kificho kwa wateja kinatisha. Jamaaa akecheka na kunikaribisha tena akinisindikiza mpaka langoni
hakuna mazingaombwe wala nini. walikuchezea fix paleplae lakini hukuona tu. Huku ni kuibiwa kizembe kabisa. Anyway sio kama nafurahia ila lazima ukweli usemwe.
Asante kwa ushuda wako. Ndicho kilichonipata mimi leo. Nilihesabu tena kwa sauti noti za elfu 10 ishirini na zilizobaki zilikuw za elfu 2 na mia 5. Nilipokuja kuangalia nikiwa peke yangu nilikuta pesa ya elfu 10 imebaki 1 tu na zingine zote ni za mia 5 na elfu 2 tu. Ni maajabu ya kishetani kabisa.Huu wizi wa kimazing'aombwe uliwahi kunitokea na wala sio uzembe. Mie mwaka jana kuna siku nilikuwa na shida ya Tshs na nimezoea kubadili katika duka moja lililopo karibu na makutano ya barabara ya Samora na Morogoro. Siku hiyo ilikuwa Jumapili na maduka mengi yalikuwa yamefungwa. Katika eneo hilo nilimkuta bwana mmoja alieniambia wanabadilisha dola kwa kiwango kizuri kama katika duka hilo. Aliniambia wako nyuma (along brbr ya Morogoro kuelekea bandarini) hivyo nimpe dola aniletee Tshs. Niligoma maana nilihisi ni tapeli. Nikamwambia alete hizo pesa kwanza. Kweli alienda na baada ya muda akarudi na noti mpya za 10,000 kama zimetoka benki. Hapa pia nilitia wasiwasi kuwa zaweza kuwa feki. Baada ya kuzichunguza sana nikaridhika, bado nilitaka tuende nae hadi kwenye jengo la PPF tower lilipo karibu nikadhibitishe kama ni pesa halali. Niliingia pale na kumkuta bwana mmoja katika biashara zake nikamwomba nae achunguze hizo pesa kama sio feki. Jamaa aliziangalia kwa muda akasema kwa ujuzi wake zile pesa zilikuwa halali. Nikazikunjia mfukoni nikaanza safari ya kurudi nyumbani. Nikiwa karibu na nyumbani nikahisi mfuko ulikuwa unatuna. Kufika nyumbani nikaamua kuzitoa. Nilipata mshtuko mkubwa kwa nilichoshuhudia. Noti zote za 10,000 nilizochukuwa zikiwa mpya zilikuwa zimebadilika kuwa noti za 500 za kawaida (sio brand new). Ndio maana mfuko ulikuwa unatuna. Hivyo huu utapeli wa kichawi/mazing'aombwe upo hapo Samora na inawezekana wengi wamelizwa ila wameamua kukaa kimya kama mie nilivyokaa muda wote huo.
Kabisa. Mimi haiwezi kunitokea katika mazingira kama hayo. Yaani maduka ya kubadilisha yalivyojaa halafu mtu anibadilishie fedha kwenye ngazi?
Haaaaah, kumbe wewe ni "she" mi huwa nadhani ni "he". Back to the topic, ni kweli kabisa ungeibiwa siku hiyo lakini pengine mtego kama huo ulishaupitia sehemu nyingine.Ha nimestuka kusoma hii habari mana kuna siku na mimi nilisamama nafikiri ni hapohapo akaja mtu harakaharakaakaniambia dada yule muhindi pale anabadili kwa bie ndogo,kweli ckumtilia maanani maana nilipiga fixed amount ya pes nilliyotaka mbona ningeumbuka mtoto wa kike
Haaaaah, kumbe wewe ni "she" mi huwa nadhani ni "he". Back to the topic, ni kweli kabisa ungeibiwa siku hiyo lakini pengine mtego kama huo ulishaupitia sehemu nyingine.
He mbona umemelizia kama vile unanifahamu.kweli nilishatapelewa tana pesa nyingi na tangu hapo hata salamu ya mtu siitikii.ee mimi ni she tena mrembo wa haja mashalaah.hahhaaa
Wanabodi, habari zenu.
Leo asubuhi nimeenda zangu city centre kwa shughuli. Nilikuwa na kiasi fulani cha hela ya kigeni mfukoni. Nikaamua kwenda kwenye moja ya maduka ya kubadiili pesa mtaa wa samora. Katika kusimama na kuangalia vibao vya exchange rates kwenye maduka hayo jamaa mmoja akanikaribia na kunambia kuna duka jirani ambalo wanabadili kw bei nzuri zaidi. Akapendekeza nimfuate anioneshe. Ilikuwa ni jirani sana, jengo refu la gorofa.
Kufika pale tukakutana na" mwenye duka" kwenye ngazi. Jamaa angu akamweleza shida yangu. Mwenye duka akaniuliza kiasi cha hela ninachotaka kubadilisha. Nikamweleza. Akasema tumsubiri. Akapanda juu akarudi na hela ya kitanzania kaifunga vema. Akanipa. Nikahesabu, nikaridhika. Tukaagana. Nikiwa njiani nikapata kishawishi cha kuangalia hizo pesa. Nilishangaa kukuta nimebakiwa na elfu 50 tena zikiwa zimekunjwa na kufungwa kwenye mpira kama nilivokuwa nimekabidhiwa.
Sikuamini macho yangu. Kwa kuwa nilikuwa nimefika mbali nilishindwa kuwarudia wale watu. Nipo hapa nauguza maumivu ya kutapeliwa kimazingaombwe. Sielewi nifanye nini! Jihadharini sana na matapeli jamani.
ni pm leo au kesho.
dahh pole aisee, ila huwezi kumckiliza mtu wa kukutana nae tu halaf mkaenda kufanya biashara kwenye ngazi manake bureu huwa wana office na wanaangalia vitambulisho na wanatoa risiti ambazo zina id reg. ya ktambulisho chako labda kama na ww hizi forex ulipiga sehemu.