Wanabodi, habari zenu.
Leo asubuhi nimeenda zangu city centre kwa shughuli. Nilikuwa na kiasi fulani cha hela ya kigeni mfukoni. Nikaamua kwenda kwenye moja ya maduka ya kubadiili pesa mtaa wa samora. Katika kusimama na kuangalia vibao vya exchange rates kwenye maduka hayo jamaa mmoja akanikaribia na kunambia kuna duka jirani ambalo wanabadili kw bei nzuri zaidi. Akapendekeza nimfuate anioneshe. Ilikuwa ni jirani sana, jengo refu la gorofa.
Kufika pale tukakutana na" mwenye duka" kwenye ngazi. Jamaa angu akamweleza shida yangu. Mwenye duka akaniuliza kiasi cha hela ninachotaka kubadilisha. Nikamweleza. Akasema tumsubiri. Akapanda juu akarudi na hela ya kitanzania kaifunga vema. Akanipa. Nikahesabu, nikaridhika. Tukaagana. Nikiwa njiani nikapata kishawishi cha kuangalia hizo pesa. Nilishangaa kukuta nimebakiwa na elfu 50 tena zikiwa zimekunjwa na kufungwa kwenye mpira kama nilivokuwa nimekabidhiwa.
Sikuamini macho yangu. Kwa kuwa nilikuwa nimefika mbali nilishindwa kuwarudia wale watu. Nipo hapa nauguza maumivu ya kutapeliwa kimazingaombwe. Sielewi nifanye nini! Jihadharini sana na matapeli jamani.