Nimetapeliwa jamani

Nimetapeliwa jamani

pole sana. yaani wewe unaacha maduka yooooooote unaenda kubadilishia hela kwenye ngazi?

na liwe fundisho kwa wote wa namna hii
 
hakuna mazingaombwe wala nini. walikuchezea fix paleplae lakini hukuona tu. Huku ni kuibiwa kizembe kabisa. Anyway sio kama nafurahia ila lazima ukweli usemwe.

Hapana kaka. Hela nilihesabu kwa umakini na akili timamu mpaka zikatimia 222,000. Baada ya hapo sijui kulitokea nini huko mfukoni. Niamini
 
Babuyao, pole sana!! Lakini wakati mwingine ni mipango ya kukuandaa kupata pesa nyingi zaidi!! kwa hiyo usisikitike sana. We chukulia tu kuwa hiyo pesa umeichange kwa exchange rate ya chini sana.

Pole sna, if cheap is expensive, why not expensive is cheap.
 
Awa jamaa wanakupa rate ya Dola ambayo uwezi kuikataa,Usifikirie kuwa wanatumia uchawi!wanakupa an Offer that you can not refuse!Lazima uingie King.
 
Kama ulisalimiana naye kwa kupeana mkono basi kuibiwa ulianzia pale pale kabla hujapanda ghorofani.
 
Pole sana, lakini kama cheap is expensive, why not expensive 2 be cheap.
 
Pole sana ndugu, ila ndo siku nyingine usipende vitu vya shortcut
 
Kama ulisalimiana naye kwa kupeana mkono basi kuibiwa ulianzia pale pale kabla hujapanda ghorofani.
Mkuu, yule gwiji mkuu tulipeana mkono. Tena baada ya kuhesabu pesa nilimuuliza kama pesa hizo ni legal na valid akasema nisiwe na wasiwasi. Nikamuuliza kwa nini duka liko kifichoni akasema lengo ni kukwepa kodi kidogo. Nikawapa ushauri wafanye biashara y wazi kwani kificho kwa wateja kinatisha. Jamaaa akecheka na kunikaribisha tena akinisindikiza mpaka langoni
 
Ulitaka aibiwe mwezi gani mkuu..believe it ndio kashaibiwa kimazingaombwe...ni tamaa ulimponza mkuu, tumpe pole kwa maumizi ya kupoteza ngawira zake ambazo alizosotea kwa namna anayojua yeye.
Unbelievable! hii lazima umetunga tu, no way, absolutely impossible.
Yaani leo, Machi 2013, uibiwe kiZOMBIE namna hiyo? no way.
Kama ni kweli basi AMKA!.
 
si kosa lako, ni midawa yao ya kukuchanganya akili, ila pole sn. ukisikia mtu kaenda ofisini ndio hapo na huo ndo mshahara wao, kazi hakuna na elimu ninayo ndo ujasiriamali huo. ila pole pole sana najua machungu ya pesa na hivi ilivyokuwa ngumu zaidi ya reli ya kati.
 
Awa jamaa wanakupa rate ya Dola ambayo uwezi kuikataa,Usifikirie kuwa wanatumia uchawi!wanakupa an Offer that you can not refuse!Lazima uingie King.
Rate yao ni nzuri sana lakini wanatumia mazingaombwe pia au tuite mysteriou ujanja "kunywa" pesa ya mteja. Hili sina shaka. Ndo walinifanya nikiwa na AKILI TIMAMU NA UMAKINI MKUBWA. Sina maelezo mengine. Kwangu ni nguvu za giza pia zipo. The devil at work.
 
Hapana mkuuu, nilipewa mkononi laki 2 na elfu 22. Nikanywewa zote na kubakiwa na elfu 50 tu.

pole sana mkuu hao wamecheza na akili yako lolz...
ila wewe uliwaamini sana aise.. tangu lini pesa zika badilishwa ktk ngazi.. shukuru Mungu kama hizo 50 sio bandia.
 
Pole.We tamaa yako ya kuonyeshwa rate ya juu kuriko unazoziona kwenye mbao za maduka.
We kesho rudi mitaa hiyo utawaona.Polesi wanajua tatizo ujasema ulikuwa wabadilisha dora ngapi.?
Wazungu na baadhi wa wageni wanje wamekuwa wanalizwa.SIYO MAZINGAOMBWE NI WEWE UNAKUWA HAUKO MAKINI KUHESABU.Pole kesho utakuwa mjanja tena
 
Pole sana ndg yangu, kila siku ni muhimu sana kumuomba Mungu kabla hujatoka nyumbani kwako na kumkabidhi njia zako zote za siku hiyo. Kuna wengine wanakupigia simu eti wewe wanaomba uwe supplier wao wanakutumia namba eti ya mwenye pruduct, kisha maelezo meengi kwamba wataje bei ya juu ya pruduct kwa meneja wao kisha hela itayozidi wanagawana na wewe na mhasibu wao, be careful with them!
 
Back
Top Bottom