Nimetapeliwa jamani

Nimetapeliwa jamani

Babuyao hebu check tena huo mfuko wa pembeni, inawezekana umejichanganya.
 
Babuyao, pole sana!! Lakini wakati mwingine ni mipango ya kukuandaa kupata pesa nyingi zaidi!! kwa hiyo usisikitike sana. We chukulia tu kuwa hiyo pesa umeichange kwa exchange rate ya chini sana.

Hahahahaha! umenichekesha aisee na ushauri wako kiboko eti chukulia umiechange kwa exchange rate ya chini sana!
 
Mambo ya mazingaombwe yapo kama hayajakutokea wewe shukuru Mungu. Afadhali huyo ametapeliwa pesa ndogo. Mimi nilitapeliwa Dollar 2,100 nikajikuta nina 270,000 tu.
 
Wanabodi, habari zenu.
Leo asubuhi nimeenda zangu city centre kwa shughuli. Nilikuwa na kiasi fulani cha hela ya kigeni mfukoni. Nikaamua kwenda kwenye moja ya maduka ya kubadiili pesa mtaa wa samora. Katika kusimama na kuangalia vibao vya exchange rates kwenye maduka hayo jamaa mmoja akanikaribia na kunambia kuna duka jirani ambalo wanabadili kw bei nzuri zaidi. Akapendekeza nimfuate anioneshe. Ilikuwa ni jirani sana, jengo refu la gorofa.

Kufika pale tukakutana na" mwenye duka" kwenye ngazi. Jamaa angu akamweleza shida yangu. Mwenye duka akaniuliza kiasi cha hela ninachotaka kubadilisha. Nikamweleza. Akasema tumsubiri. Akapanda juu akarudi na hela ya kitanzania kaifunga vema. Akanipa. Nikahesabu, nikaridhika. Tukaagana. Nikiwa njiani nikapata kishawishi cha kuangalia hizo pesa. Nilishangaa kukuta nimebakiwa na elfu 50 tena zikiwa zimekunjwa na kufungwa kwenye mpira kama nilivokuwa nimekabidhiwa.

Sikuamini macho yangu. Kwa kuwa nilikuwa nimefika mbali nilishindwa kuwarudia wale watu. Nipo hapa nauguza maumivu ya kutapeliwa kimazingaombwe. Sielewi nifanye nini! Jihadharini sana na matapeli jamani.


pole sana ndugu.. ni bora umesema hapa nawengine tuchukue tahadhari


jamani tusipende njia zisizo kubalika . tujenge tabia ya kupata huduma kutoka sehemu zilizo rasmi. hakuna sababu ya kuchukuliwa na mtu eti utapata bei nzuri. kama unataka kwenda dukani kupata huduma pata huduma dukani. siyo nje ya duka mtu anakuuliza unataka nini unasema nataka kununua saa , halafu unaambiwa mimi nina saa nauza..... hiini hatari si kwa pesa yako tu bali pia kwa usalama wako
 
Pole sana ndugu yangu, mimi pia ni mhanga wa utapeli hapa bongo kwa hiyo naweza kuwa miongoni mwa wale walio kuelewa barabara.
 
Asamte kwa ushauri. Ukweli pes hiyo wala sijaitumia kwani inanipa kichefuchefu.

Kama kipato chako ni kikubwa ni bora ukaipereka kwenye vituo vya yatima, umeshajiuliza kwa nn pesa zilipotea kimiujiza??
 
Jenga tabia ya kutokukubali kuingia kwenye mazungumzo na mtu au watu usiowafahamu. Hii ni kanuni yangu niliyojiwekea.
 
Yani watu wanatafuta pesa kwa juhudi kumbe bado kuna mijinga inakwenda kutupa pesa kwa watu wa Filmeee!!?? hiyo ndio inaitwa Wash kaka.
 
karibu mjini and always kupenda urahisi vina gharama zake na hiyo ndo gharama yenyewe
 
Babuyao, pole sana!! Lakini wakati mwingine ni mipango ya kukuandaa kupata pesa nyingi zaidi!! kwa hiyo usisikitike sana. We chukulia tu kuwa hiyo pesa umeichange kwa exchange rate ya chini sana.

Mkuu hata kama ni kumfariji mwenzio si kwa mtindo huu! Kutoka laki 2 na elfu 22 hadi elfu 50 wewe unaiita hii exchange rate ya chini? Naona hapo ulitaka kutufurahisha tu!! Haina neno lakini manake pole yako ameipata!!
 
Mkuu pole sana ndiyo Dunia ilivyo.Ujumbe wako ni somo kwa wengine,ingawa kuna watu wanafikiri haiwezi kuwatokea.

Kabisa. Mimi haiwezi kunitokea katika mazingira kama hayo. Yaani maduka ya kubadilisha yalivyojaa halafu mtu anibadilishie fedha kwenye ngazi?
 
Pole sana mkuu, when the deal is too good think twice
 
Narudia tena. Mi nikuwa makini sana, na nilihesabu lwa mkono na macho yangu mwenyewe. Lakini baada ya hapo kilichotokea namwachia Mungu. Yeye ndo atashugulika nao ndo mana sikutaka hata kurudi kupambana nao. Mungu atawalipa kadiri ya matendo yao. By the way jengo alimo huyo tapeli ndipo ime pia ofisi ya dr. Lamwai na makampuni mengine. Hizi taarifa nilizisoma kwenye lango la kupandia ngazi. Maandishi yako ukutani kabisa.

Nini bwana ... ''machingaombwe'' ''machingaombwe''. Ni umbulula wako tu ndio unakufanya uone kama yalikuwa ni mazingaombwe. Na UNA HAKI KABISA ya kuyaita mazingaombwe au uchawi kwani hujui kilichotendeka. Lakini mimi nakuhakikishia kabisa sio!
 
Mambo ya mazingaombwe yapo kama hayajakutokea wewe shukuru Mungu. Afadhali huyo ametapeliwa pesa ndogo. Mimi nilitapeliwa Dollar 2,100 nikajikuta nina 270,000 tu.

Hayo utamkikishia na kumwaminisha mtu/watu wako huko kijiweni. Si hapa kwenye forum ambako kuna watu wenye exposure na elimu za kila aina.
 
Ndugu yangu amini usiamini hao watu wapo, hata mimi nilishawahi kukutana nao, wakaniambia kuwa kuna mtu ana change kwa bei nzuri, nikawajibu asante nikaishia zangu. Sasa wewe unayesema unbelievable subiri mpaka yakukute ndio uta believe. Hata hivyo jamaa ametoa tahadhari tu kwa vile yamempata yeye yasije yakampata mwingine.

Nilivyomwelewa jamaa hakubisha au haamini kama hao watu wana exist. Yeye haamini kama kuna mtu anaweza kutapeliwa kimbulula namna hii miaka hii, kwani huo utapeli ni siku nyingi sana...
 
Nilivyomwelewa jamaa hakubisha au haamini kama hao watu wana exist. Yeye haamini kama kuna mtu anaweza kutapeliwa kimbulula namna hii miaka hii, kwani huo utapeli ni siku nyingi sana...

Hao watu nahisi wanatumia kiini macho, ni kama wale ambao walikuwa Mlimani City, anajidai nataka kwenda mahali sasa sipajui naomba unipeleke nina madini naenda kuuza, upuuzi mtupu, ukiwasikiliza tu umekwisha. Na hao ni hivyo hivyo ukiwapa muda wa kuongea nao tu tayari.
 
jamani sio kikondoo kwani sote tupo kwa ajili ya faida na si vinginevyo, hiyo ni bahati mbaya kwani nikatika utafutaji2.

Nini? bahati mbaya? Unapelekwa kwenye ngazi wakati umeacha maduka chungu nzima halafu unasema bahati mbaya?
 
Hao watu nahisi wanatumia kiini macho, ni kama wale ambao walikuwa Mlimani City, anajidai nataka kwenda mahali sasa sipajui naomba unipeleke nina madini naenda kuuza, upuuzi mtupu, ukiwasikiliza tu umekwisha. Na hao ni hivyo hivyo ukiwapa muda wa kuongea nao tu tayari.

Bi mkora amini nakuambia hakuna kiini macho wala kiini masikio. Ni kupelekwa chaka tu. Hii kwa kifupi tunaweza kusema wanakupiga ''ambush'' ya ki-akili. Kabla huja-recover wanakuwa wameshafanya damage.
 
Kuna jamaa yangu alikuwa ananiambia kuwa hawezi kununua kitu ambacho hakupanga kununua tokea akiwa nyumbani hata kiwe kizuri namna gani anakwambia sikupanga kununua hicho kitu kumbe alikuwa wa maana. Wewe umetoka nyumbani kwenda dukani kubadili fedha iweje ukabadili fedha kwenye ngazi?
 
Back
Top Bottom