Nimetapeliwa jamani

Nimetapeliwa jamani

imenibidi nicheke sana kwani watu hawa nawajua sana hata majina yao, wapo pale kwa empress cinema, IPS, na samora kule juu, hawa ndio kazi yao kubwa wamejenga wameo wanawake wazuri wengine wana magari, hawa jamaa wanaibia hata makomandoo wa kimarekani, picha hii nilikuwa nazishuudia laivu wakati nipo samora, wamewahi kumuibia mkapa akiwa wazir, ukitaka kuwapata waulize wale waandishi wa habari pale kijiweni kwao watakupa majina unaweza kumkumbuka aliyekuibia
 
Ila wewe babu ungeniambia nikusindikize si ningekusindikiza, unahisi wamekuwekea kalumanzila wakapunguza hilo salio.
 
Babuyao, pole sana!! Lakini wakati mwingine ni mipango ya kukuandaa kupata pesa nyingi zaidi!! kwa hiyo usisikitike sana. We chukulia tu kuwa hiyo pesa umeichange kwa exchange rate ya chini sana.

Una akili nyingi sana we jamaa,nimeipenda logic yako!
 
Unmgekuwa miji kama Johannesburg ambako bureau hakuna hapo sawa lakini kwa Dar tena city center hayo ni ya kujitakia ama wamekuwekea dawa ukapoteza akili zote
 
Mambo ya mazingaombwe yapo kama hayajakutokea wewe shukuru Mungu. Afadhali huyo ametapeliwa pesa ndogo. Mimi nilitapeliwa Dollar 2,100 nikajikuta nina 270,000 tu.

Asante kaka kulitambua hilo. Wapo watu hawaamini.
 
Yani watu wanatafuta pesa kwa juhudi kumbe bado kuna mijinga inakwenda kutupa pesa kwa watu wa Filmeee!!?? hiyo ndio inaitwa Wash kaka.

Asante sana kaka kwa jibu la kung'ata.
 
Unbelievable! hii lazima umetunga tu, no way, absolutely impossible.
Yaani leo, Machi 2013, uibiwe kiZOMBIE namna hiyo? no way.
Kama ni kweli basi AMKA!.

yaani Dar hata ikifungwa spika kila kona na kutangazwa uwepo wa matapeli, Mazombie hawaishi wataendelea kuingizwa mjini tu.
 
Nini bwana ... ''machingaombwe'' ''machingaombwe''. Ni umbulula wako tu ndio unakufanya uone kama yalikuwa ni mazingaombwe. Na UNA HAKI KABISA ya kuyaita mazingaombwe au uchawi kwani hujui kilichotendeka. Lakini mimi nakuhakikishia kabisa sio!
Asante sana. Mimi ni mbulula.
 
Nilivyomwelewa jamaa hakubisha au haamini kama hao watu wana exist. Yeye haamini kama kuna mtu anaweza kutapeliwa kimbulula namna hii miaka hii, kwani huo utapeli ni siku nyingi sana...

Wewe ndo tapeli wangu. Unaudhi sana kwa majibu yako.
 
Bi mkora amini nakuambia hakuna kiini macho wala kiini masikio. Ni kupelekwa chaka tu. Hii kwa kifupi tunaweza kusema wanakupiga ''ambush'' ya ki-akili. Kabla huja-recover wanakuwa wameshafanya damage.
Sasa ambush ya kiakili ndo nini kama si mazingaombwe? Au hypnosis?
 
Asante sana. Mimi ni mbulula.

Lakini usije tu ukafikiri mbulula ni matusi. Ni mtu ambaye amepitwa/hajui ujanja-ujanja unaotumiwa na watu katika mazingira anayoishi. Kwa mfano hapa umesema ulikuwa unaangalia bei mara akatokea wa kutokea na kukushawishi eti kuna duka wanabadilisha kwa bei nzuri. Na wewe wala hukujiuliza huyo jamaa katokea wapi na alikuwa nafanya nini pale na alijuaje wewe una shida hiyo na kwanini anapoteza muda wake kufanya usamaria wa kuelekeza watu wakati huu utapeli uko siku nyingi
 
Wewe ndo tapeli wangu. Unaudhi sana kwa majibu yako.

Ungejua ninavyochukia na kupiga vita wizi/utapeli usingeandika hivyo. Mimi naona umepatikana kirahisi mno ndio maana nimechukia. Mwizi anapow-win mimi huwa nachukia sana
 
Sasa ambush ya kiakili ndo nini kama si mazingaombwe? Au hypnosis?

Hapana. Ambush ya akili ni pale mtu anapokuingia kwenye angle ambayo usingetegemea. Mkuu Babuyao kama hii michezo ya mazingaumbwe kuna mingi ikionyeshwa Tanzania watu wengi wataamini na kusema ni uchawi kumbe ni ujanja tu. Hebu jaribu kuangalia kwenye bwana mmoja anaitwa Pauli daniel akifanya Pauli Daniel magic show. Kama hujui ujanja anautumia wewe utabaki kinywa wazi na usiku hutalala kwani utafikiria umekutana na jini. Kumbe ni ujanja tu. Baada ya hapo jaribu kuangalia ''Magic's Biggest Secrets Finally Revealed'' ambapo wanaonyesha ujanja unaotumika hapo utagundua mengi.
 
kuna rafikiangu moja alirudi kwao magomeni kwa miguu, alitapeliwa k.koo' wakachukua cheni pesa na cm! Chezea matapeli weye!
 
Hapana. Ambush ya akili ni pale mtu anapokuingia kwenye angle ambayo usingetegemea. Mkuu Babuyao kama hii michezo ya mazingaumbwe kuna mingi ikionyeshwa Tanzania watu wengi wataamini na kusema ni uchawi kumbe ni ujanja tu. Hebu jaribu kuangalia kwenye bwana mmoja anaitwa Pauli daniel akifanya Pauli Daniel magic show. Kama hujui ujanja anautumia wewe utabaki kinywa wazi na usiku hutalala kwani utafikiria umekutana na jini. Kumbe ni ujanja tu. Baada ya hapo jaribu kuangalia ''Magic's Biggest Secrets Finally Revealed'' ambapo wanaonyesha ujanja unaotumika hapo utagundua mengi.

Macho mdiliko nimekuelewa. Kweli nilipigwa ambush ya kiakili. Sina jinsi, nimejifunza kwa kweli. Nimeteseka sana nafsi yangu kufanywa mjinga. Na hili ndo limeniumiza zaidi kuliko hata pesa yenyewe. Asamte kwa ushauri wako.
 
Hao jamaa nami walishanipeleka pale ghorofani lakini bahati nzuri roho ilikataa kufanya nao biashara
 
Back
Top Bottom