Jinsi nilivyomuokoa mzee mmoja na njama za kutaka kuuawa na kijana wake

Cosovo

JF-Expert Member
Jul 8, 2018
667
1,795
Miaka kama 13 imepita wakati huo tukiwa Ilboru sekondari nilikuwa na rafiki yangu mmoja ambaye tulikuwa tunaishi jirani kwenye jiji moja la kanda ya ziwa

Tulikuwa hatufahamiani kabla, tulifahamiana wakati tunaanza kidato cha kwanza tulipokuwa shule na urafiki ukaanzia hapo

Siku moja tumerudi nyumbani likizo alinikaribisha nyumbani kwao nami nikafika

Tukiwa pale nyumbani aliniambia kuwa mama yake mzazi aliondoka yaani waliachana na baba na hivyo baba yake akaoa mke mwingine ambaye hakuwa na umri mkubwa sana kama 24 hivi

Familia hiyo yenye asili ya kaskazini mzee alikuwa na gereji kubwa hapo jijini, maduka mawili ya vifaa vya ujenzi na spea za magari

Pia alikuwa na uwekezaji wa madini huko kahama sasa siku hiyo tunaondoka kutoka nyumbani kwao alinisindikiza ,alichukua ufunguo wa gari akanambia panda humu nikusindikize ,nilishangaa sana kwamba kwa umri miaka 15 anajua kuendesha gari

Basi akaendesha tulipofika mjini akanambia kwanza tupige misele mjini mara tunaenda kuwatafuta mademu waliokuwa wanasoma nao huko seminary primary

Katika urafiki wangu na yule kijana alipenda starehe sana kuliko kusoma na likizo nzima nikimwambia tuanze kusoma anakwambia yupo bize mara aende dukani kumsadia mfanyakazi wao, mara aendeshe gari mpaka kahama, Geita na hakuwa na leseni ila pesa kila kitu njiani

Hata tulipokuwa shuleni dogo yeye hana muda wa kusoma stories zake ni pesa, madem na magari

Tukiwa kidato cha tatu dogo walivurugana na walimu na wakamuita mzazi wake kama hamhamishi watamfukuza shule hivyo mzazi wake akaamua kumhamishia private moja huko Bukoba

Urafiki uliendelea na tulikuwa tunakutana nyumbani kipindi cha likizo na maisha yake ni kudrive magari ya baba yake

Baada ya matokeo ya kidato cha nne kutoka aliscore 0 wakati huo mimi nikiwa na 3 pia alichangia mimi kupata hizo alama kwa misele na stories zake

Baba yake alipopata habari kuwa mwanae aliscore 0 alimgombeza sana na wala kijana hakushtuka yeye aliendelea kula maisha na magari ya baba yake na pikipiki muda mwingine

Baba yake akamtaka amrudishe shule kijana akagoma baba yake akampeleka gereji yake afundishwe ufundi ,kijana akagoma mzazi akamtishia kumfukuza nyumbani lakini baadae kijana akakubali

Siku moja alichukua gari la baba yake akaondoka kusikojulikana na baada ya wiki moja akajikuta yupo lockup Dodoma kituo cha polisi kwa kuendesha gari bila leseni,mzazi wake aliambiwa akaenda akamtoa akamrudisha nyumbani na akamwambia mzazi wake hataki ufundi wala kitu chochote anahitaji akae nyumbani tu na hata kukaa dukani hataki

Basi mzazi wake akamuacha,kijana ni kudrive magari ya mzee mjini na kama hana hela ya mafuta anamuomba mama mdogo hela anaenda kujaza ,akaanza mazoea na mama mdogo wakaingia kwenye mahusiano ya kimapenzi

Baba yake akaanza kuwa na mashaka kati ya kijana wake na mkewe ,baada ya baba kuwatia mashakani,kijana na mama mdogo wakaanza kuandaa mikakati ya kumuondoa uhai

Wakapanga kuwa wakisha muondoa huyo mzee wanauza kila kitu wanahamia Mbeya au Tunduma lakini kabla ya hayo ili kuwarahisishia kuchukua mali zote lazima watumie mbinu ili mzee aandike wosia wa kuwagawia mali kijana na mama mdogo ,cha kukuongezea ni kwamba mama mdogo alikuwa amezaa na mzee watoto wawili wa kike na kijana alikuwa na mdogo wake mmoja wa kike ambaye muda mwingi anasomea Uganda

Mipango ya kutaka kuandaa wosia inaanza kufanyika na lengo la wosia ni kuwa baada ya kumuondoa uhai ndugu wa marehemu wasiwe na nguvu ya kuongelea mali na sasa na mimi nadokezewa hili dili kwa posho ya milioni 5 nikifanikiwa kufanya yafuatayo

Itaendelea................Nilienda kunywa maji sasa naendelea

Baada ya kupewa hilo dili la milioni 5 Dada(mama mdogo wa jamaa) aliniita hotel moja maeneo ya Ghana ilikuwa saa 12 jioni akaanza kunitaka nifanye yafuatayo

Kwanza ataniletea documents za mzee vitambulisho,leseni na vitu vingine niende nimtafute mwanasheria tuandike wosia kisha tutumie mbinu na huyo mwanasheria zipate muhuri wa mahakama na akanipa orodha ya mali kwenye karatasi na picha ya saini ya mzee ,passport za mzee,huyo mwanamke,passport za watoto wote ,akanipa na akanipa barua ya serikali za mitaa iliyogushiwa na vyeti vya kuzaliwa na cheti cha ndoa

Akanipa milioni moja kwa kuanzia na nikimpata mwanasheria aliyetayari tutampa kitu kidogo na mwanasheria asiwe wa Mwanza wala Shinyanga

Nikaingia kazini kumsaka mwanasheria, nilipokuwa nawahusisha wanasheria kama watatu hivi walikataa ,wakawa wanashauri kwa nini tusitumie mbinu za ushawishi wa kawaida yeye mzee aandike wosie kwa kigezo cha kuhofia ukoo kuwanyang'anya mali lolote likitokea kwa mzee?

Iliposhindana kwa hao watatu nikaamua kwenda chuoni SAUT nikampata kijana mmoja akawasiliana na ndugu yake akakubali kufanya hiyo kazi alikuwepo Tabora na akawataka hao wanafamilia ndo waende Tabora na nyaraka zote zinazohitajika na kiasi cha milioni 7

Nikamwambia mdada akakubali nikampa nyaraka zake zote akamwambia msela wake wakapanga tarehe ya kwenda Tabora

Kweli zoezi lilifanikiwa na cha kwangu wakanipa milioni mbili na nusu ikabaki milioni mbili na nusu ambayo wangenipa baadae baada ya Dada kudai hela ametumia yote nisubiri akusanye

Baada ya miezi kadhaa mdada alinipigia simu akinihitaji mara moja hotel moja maeneo Bwiru ,nikataka kujua kulikoni akanambia niende tu kuna mazungumzo,nikataka nijue mzee alipo kwanza akanambia yupo nje ya nchi basi nikaondoa wasiwasi nikaenda

Alikuwa na msela wake wanakunywa pombe basi nami nikajumuika pale mezani ,siku hiyo ndo nilijua malengo ya kutaka kujimilikisha mali hii ni baada ya kulewa kijana akawa anatamka wazi wazi kuwa ile mali ni yake na muda wowote atamuua mzee apishe ,asiwe kizingiti

Basi mwanamke akachukua laki tano akanipa ila akanionya kuwa nililosikia pale hata siku moja asije akalisikia sehemu nyingine na wakisikia nitakufa mara moja

Ilipofika saa 5 hivi dreva wao akawafuata na mimi nikachukua tax nikasepa zangu home

Asubuhi nilikuwa na mawazo sana kutokana na vitisho nilivyopewa ,nikataka niwareport polisi ila nikasema moyoni acha tu wakishanipa million 2 zangu zilizobaki naweza kuchukua hatua

Siku moja nipo zangu mjini nilipigiwa sim na mzee (baba yake msela) akanambia niende mahala fulani mtaa Fulani anambie,kwanza nilishangaa amepataje namba yangu ila nikawaza au deal limebuma au kuna nini ngoja nikamsikilizie

Alikuwepo Vila park kwa nje uwanja wa furahisha amepark gari lake pembezoni akanambia ingia ndani ,nikaingia nikakaa na yeye siti ya mbele

Mazungumzo yaakaanza,"Wewe ni rafiki yake sana R na tangu mkiwa sekondari,na pale kwangu nina mwanamke na unamjua vizuri ,hebu nambie nini kinachoendelea kati yako na yeye?

Nikapigwa na butwaa,nikanyamaza kidogo nikamwambia mzee yule mama J alikuwa ananiita maeneo mbalimbali hapa mjini kwa mambo kadha wa kadha ila naendelea kufanya uchunguzi yakikamilika nitakutafuta nikwambie"

Mzee akafyumu "Mambo gani,sema mambo gani hayo,yaani ujue kabisa nina abc zako kuhusu mke wangu,awali nilikuwa namuwazia R lakini nilipoongea na R kwa kirefu alikutaja wewe kuwa unatembea na mama J '"

Nikamwambia mzee siyo kweli,akanizaba makofi mawili akanambia nishuke na akaniambia nisipoachana na mke wake atanifanyia mbaya

Wakati narudi zangu R akanipigia sim kwamba amebanwa na mzee kuwa huenda mimi natembea na mama J ,nilivyoona yamefika shingoni nikaamua kukutaja ila cool down kesho nitakupa laki mbili ukapoze mikikimikiki "Nikamwambia poa

Kesho yake nikatumiwa hiyo laki mbili na ghafla mama yangu ananiita nyumbani ,kufika ananiambia kuna polisi wamekuja kukutafuta wamesema leo ufike kituoni kuna kitu wanataka kujua kutoka kwangu"

Awali mama alikuwa amenigombeza na akiwa anataka kujua nimefanya kosa gani basi nikamwambia hamna kitu

Nikaenda polisi kituo nilichoelekezwa nikaanza kuhojiwa kwa nini natembea na mke wa mtu

Nitaendele baadae.............

Basi polisi mmoja akaanza kunihoji kuwa natembea na mke wa mtu nikamuuliza "mke wa nani afande mbona simjui" Afande akaniambia "Bwana mdogo usijifanye hujui ,unamtesa mzee wa watu na tamaa ya pesa,na inasemekana yule mwanamke anakuhonga ,uongo kweli?" Nikawaza kidogo nikamwambia afande ngoja nikwambie ukweli "Mimi stembei na yule mama, yule mama anatembea na kijana wa yule mzee sijui kama unamfahamu?" Afande akajibu "Hapana simfahamu" nikaendelea kueleza ,"Yule mama si unamuona siyo aged siye mama yake mzazi wa huyo mama bali ,yule mzee walizinguana na mke wake akafukuza " Afande akasema "Mimi siwafahamu familia ya yule mzee ,tofauti na mzee mwenyewe siwafahamu wengine"

Basi mwishowe afande akanionya kuhusu kuwa na ukaribu na huyo mwanamke ila sikumdokezea swala la familia ya mzee kutaka kumfanyia unyama nilipiga kimya nikaondoka

Ilikuwa imefika saa 12 inaelekea saa moja nikiwa natembea barabarani gari haice ikaja ikasimama pembezoni barabarani ,akapiga honi dreva akaniita ,nikajiuliza labda ananifahamu,ile nafika mlangoni kwa dreva kumsikiliza,nikashtukia mlango unafunguliwa upande wa abiria narushwa ndani mlango unafungwa gari linaanza kukimbia

Mle kulikuwa na watu watatu wote sura ngeni,wakaninyang'anya sim yangu ,mle ndani kuna sit moja tu,nikapigwa makofi nikalazwa chini,nikafungwa na kamba mikono ,wakanifunika uso kwa kitambaa,ndo nikaanza kusikia mmoja ananiambia "Yule mwanamke ulishatembea naye mara ngapi na mpaka sasa alishakupa sh ngapi?

Nikawajibu huku nimelazwa kifudifudi kuwa" Mbona hakuna mwanamke ambaye nimewahi kutembea naye" Nikashushiwa fimbo matakoni kama 20 hivi nikiambiwa dogo usiposema unaenda kufa

Nikawambia "Jamani mimi stembei na mwanamke yeyote hapa mjini ,ila kuna mwanamke wa tajiri mmoja anaitwa mama j ndo mme wake ananituhumu "

Ndo mwingine akadakia "Tayari amekiri kuwa anatembea naye kwa hiyo tuache kumpiga huyo dogo"

Wakaacha kunipiga ,gari likakimbia muda mrefu kweli na sijui ninapoenda

Baada ya masaa mengi tu,gari likasimama ,nikasikia kalipe kivukoni",Nikawauliza sasa mnanipeleka wapi jamani ,"mmoja akanambia "Dogo kaa tulia la sivyo utapotezwa"

Nikanyamaza ,gari likazidi kuchanja mbuga sijui tunaenda wapi,nikawaza sasa hapo kuwa lipia kakate ticket kivukoni ni wapi hapa,kwa masaa yote kweli hapa ni Busisi kweli

Gari likaenda masafa kweli kweli ,baadae wakanifungua kama na kitambaa wakaniambia shuka upesi,kufika nje wakasema hilo ni onyo ukirudia hiki utakachokutana nacho hapa ni kidogo

Gari likaondoka wakaniacha ,kuangalia naona mistu tu,giza kali kweli na hata sijui nilipo ni wapi ,

Nikaaa pembezoni mwa njia ndogo sijui hata ni saa ngapi ,nasikia tu kelele za wadudu wapiga kelele vichakani nyakati za usiku

Nikawaza acha nitembee nielekee popote liwalo na liwe kama nitakutana na wanyama wakali humu hamna shida

Kadri nilivyokuwa natembea nikawa nasikia mlio wa mashine kama jenereta kwa mbali,nikawaza ngoja nifuate hiyo mashine ilipo ,mstu mnene kweli kweli

Nikasogea nikakuta majengo mengi na umeme umewaka hilo eneo,nikawaza ngoja niende hapa niombe msaada ,kufika nikaanza kubisha hodi kwa sauti kubwa sana,mlinzi akajitokeza akaniamrisha kaa chini,nikaaa akaniambia tembelea magoti uje mpaka huku muda huo tochi ipo usoni kwangu

Nitaendelea
Nikajikokota chini nikafika kwenye kibanda chake

Akawa ananiuliza wewe ni nani na usiku huu unatoka wapi ,nikamwambia afande nimevamiwa na watu wasiojulikana na kuniweka kwenye gari mpaka huku hata sijui hapa nipo wapi

Muda huo mlinzi yupo ndani ya kibanda mimi nimepiga magoti nipo kwa nje ila ananihoji akiwa kwenye kibanda chake kupitia dirishani

Akaniuliza unaitwa nani nikamwambia jina langu," wewe ni mkazi wa wapi ? Nikajibu Mwanza " akauliza kwa hiyo umetekewa Mwanza au eneo lingine nikajibu " Hapo hapo Mwanza mjini" akaniuliza" Huko Mwanza unajishughulisha na nini mpaka utekwe" Nikamwambia " Mimi ni mjasiriamali na sajajua sababu ya kutekwa"

Baada ya dakika kama kumi akafungua mlango akatoka nje akasema nisimame akachukua kiti tukakaa pembezoni mwa kile kibanda ,basi nikamuuliza "Afande hapa ni wapi eti" Akasema dogo upo Ukerewe kijiji cha murutunguru na hapa ulipo sasa ni chuo cha ualimu

Akaniuliza umetekwa saa ngapi na hao watu nikamwambia ilikuwa saa moja kasorobo jioni

Basi yule mlinzi alimpigia simu polisi jamii wa ule mtaaa akaja lile eneo akanihoji na kwa kuwa alikuja na gari akanambia ngoja nikupeleke Nansio kituo cha polisi wakupe msaada

Tukaondoka mpaka Nansio mjini akanikabidhi polisi,muda huo ilikuwa saa 7 za usiku

Afande akanihoji hapo nikatoa maelezo ,wakaniandikia pf3 wakanipa wakanipeleka kwenye nyumba fulani nikalala mpaka asubuhi nikarudi polisi ,wakanipeleka mpaka kwenye meli wakaomba nisafirishwe kwenda Mwanza ,afande akanipa sh 2000 ya kunywa chai

Nikafika Mwanza nikaenda nyumbani hata sikutaka nimueleze mama kilichotokea

Baada ya siku moja nikaenda kituo cha polisi nikamtafuta yule polisi wa siku ile bahati mbaya hakuwa zamu basi nikaamua kumweleza afande wa zam A to z na kunipa pole sana na alisikitika sana baada ya kumweleza story ya mzee huyo kutaka kuuliwa na mke na mtoto

Baadae yule afande akampigia afande ambaye walikuwa wanafahamiana na yule mzee akampa namba ya sim akampigia mzee bahati nzuri alikuwa mazingira ya karibu akatupa nusu saa atakuwa amefika kituoni hapo

Baada ya dakika chache mzee akawa amefika akagonga mlangoni akaruhusiwa akaingia ndani

Akanikuta nimekaa nikamsalimia hakuitikia ,afande akamsalimia akaitikia ,afande akamuomba akae ,akakaa huku akinitazama kwa hasira na dharau kali

Afande akaanza kumweleza" Mzee huyu kijana amefika hapa kukuomba msamaha nimeongea naye muda mrefu ,amekiri kuwa hana mahusiano na mke wako ila kuna vitu ameniambia vya kijinai inapaswa nivichunguze,nikimaliza nitakujulisha"

Baada ya mzee kusikia kuna jinai inataka kuchunguzwa mzee akapanic

"Wewe afande ,huyu kijana asiniletee ujinga,na kama amekudanganya mambo kadhaa unataka kunichunguza nawambia hamfui dafu,yaani nimekosewa mimi halafu mnichunguze"

Mzee akashauti huku amesimama "afande nakwambia huyu kijana asipoachana na mke wangu nitamuua,nyie endeleeni kunichunguza"

Mzee anaondoka kwa hasira licha ya afande kumtuliza ili amweleze vizuri,mzee ni kugomba na kuhisi anataka kuchunguzwa mimi baada ya kutekwa

Nikabaki na afande akaniambia "Sasa dogo wewe nenda nyumbani,huyu mzee kapanic na hata kutekwa kwako huyu mzee atakuwa amehusika maana alivyosikia tutachunguza jinai amehisi ni yeye amepanic,sasa wew nenda nitamtafuta na afande W ndo wanafahamiana zaidi tuongee vizuri ili tumueleweshe vizuri"

Nikajibu "Nashukuru afande mi ngoja niende zangu," ila akanionya nisije nikawasiliana na mtu yeyote kwenye ile familia

Nikaendelea na shughuli zangu mtaani ,huko mtaani nilikuwa na rafiki yangu mmoja ila yeye hakuwa mzuri kitabia,alikuwa anajihusisha madawa ya kulevya na uporaji nikawa nimejitenga naye ila mke wake tulikuwa bado tunaendelea kuwasiliana tu vizuri

Siku moja huyo shemeji yangu alinipigia sim na kuniuliza kama mume wake anajua kutumia bunduki,nikamuuliza kulikoni shem!?

Akanijibu" Yaani shem yule rafiki yako R wa mzee boss,wako naye siku hizi bega kwa bega, siwaelewi,nimesikia wanataka kwenda Serengeti kumuua tembo ,sasa nikawa najiuliza amejifunza lini bunduki "?

Nikamwambia" Shem nina siku nyingi hatukai pamoja na Mr wako sijui kama anajua bunduki"

Ila nikamuomba siku wanaenda Serengeti uje kunambia shem ila usimwambie kuwa mimi najua hiyo safari akakubali na kuagana

Niliwaza" Ushirikiano wa R na M ulianza lini huu,au si ndo kutaka kumuua mzee,huyo tembo hatakuwa yule mzee kweli " Ngoja tusubiri

Siku moja nikiwa nimekaa mitaa ya liberty na rafiki yangu mmoja mke wa M alikuwa anapita yale maeneo ,nikamuita ,akaja tukasalimiana kisha akanambia " Shem afadhali nimekukuta haya maeneo twende pembeni nikwambie

"Shem nikwambie ,yaani kuna mikakati inapangwa mle ndani ,mikakati ya hatari ,sijui wanapanga vitu gani "

Yes Shem endelea "Yaani yupo M,R na kijana yule mabangi,nikasikia kwa mafumbo wanaongea" mara yule tembo mara mzee,mara watumie madawa,sijui watumie bunduki,sijui R aje kuzima taa za nje baada ya tukio ziwashwe ,mara mlinzi anyweshe pombe,yaani Shem ile mipango hata sielewi ni ujangili au ujambazi"

Nikamwambia"Shem wewe cha msingi wewe nenda utulie,wala usimhoji sana kuwa anataka kufanya nini ,piga kimya,jifanye huna muda nao ,ila siku ukisikia wanaenda na najua atakuaga,nitumie sms kama watakuwa wanaenda kufanya mambo mabaya nije kumpigia sim aache" Shem akakubali na kisha tukaagana

Alipoondoka tu! Nikachukua sim nikampigia Afande",sasa kuna mipango inapangwa na yule kijana wa mzee kuhusu ile misheni ya kumuondoa, siku nyingi hatujawasiliana,vipi mlimtafuta yule mzee" Afande akajibu" yule mzee tulimpigia sim siku moja aje kituoni hakupokea tukatemana naye"

Nikamwambia'Sasa mipango ilishasukwa na hii mipango nahisi itakuwa inamhusu mzee" Afande akanambia "Sasa kesho njoo kituoni " Sawa afande" nikakata sim

Kesho yake asubuhi muda wa saa mbili nikafika nikawakuta maande wale wawili wapo wakaniita nje kwenye miti miwili tukakaa pale ,nikawasimlia kila kitu ,mipango yote

Basi maafande wakasema tutamuita mzee rasimi na tutamueleza vizuri tu na kisha tutamwambia asiwe na papara ili tutengeneze mtego tuwanase hao watu

Basi nikaondoka kwenda zangu mtaani ,ilikuwa Jumamos mvua zinanyesha na zikilindima na radi saa 1 usiku ,sms ikaingia kusoma"Shem nimeagwa kuwa wanaenda kahama,na kuna begi waliliacha hapa lilikuwa na maski na mapanga na wameondoka nalo ,nililikagua kwa siri" Nikajibu "OK Shem,ety wapo Wangapi "akajibu "watatu wale wale na R amekuja na gari kuwachukua na mama mdogo wa R alikuwemo niliwachungulia dirishani"

Ile Sms nikafowadi kwa afande,sekunde afande akanipigia sim ,Sasa uko wapi" nikamwambia "nyumbani " akanambia " sasa wewe tulia nyumbani usitoke na piga kimya usiseme kwa mtu " nikajibu "Sawa"

Maafande wakampigia mzee sim na kumuiliza atakuwa mitaa gani kwa sasa" mzee akajibu "nyumbani" afande akamuuliza "vipi mkeo na mwanao yupo "? Mzee akajibu " kuna mfanyakazi wangu yupo Bugando hospitali anaumwa wamepika hapa na kumpelekea chakula"

Afande akauliza" saa ngapi ilikuwa,mzee akajibu "muda si mrefu'

Afande akamwambia" sasa chukua usafiri ,usije na gari lako ,panda hata boda na usiage nyumbani njoo kituoni na usiwapigie sim mama na kijana"

Mzee akasema" sawa"

Mzee akafanya haraka na kuchukua boda mtaani fast akafika kituoni ,alipofika maafande wakamwambia misheni yote na mzee hakuamini

Basi wakakubaliana kuweka ambush wawanase ,wakamwambia mzee "sasa afande mmoja atakusindikiza mpaka nyumbani ,ukishaingia ndani ,afande atarudi ,wewe utakaa attention baada ya kusoma mazingira pale nyumbani ikiwezekana ingia chumba cha ofisi jifanye kama uko bize na makabrashi ya biashara yako muda huo unachunguza harakati za watu hao wawili"

Mzee akakubali na sekunde chache mke wake akampigia sim akimuuliza yupo wapi akajibu yupo duka la jirani anakuja

Basi mzee akaondoka na afande aliyevaa kiraia na silaha akamsindikiza akamfikisha nyumbani,akagonga mlinzi akamfungulia na kuingia ndani

Alipoingia ndani moja kwa moja mpaka chumba cha ofisi yake kilichopo nyumbani, mke wake akafika akagonga mlango akamfungulia ,akamletea chakula,akamwambia kiweke dining room nakuja muda si mrefu

Mzee akawa kama bize lakini akichungulia nje kutumia upenyo dirishani wako bize,mkewe na kijana wako bize na mlinzi wanapiga stories,akapiga sim kwa afande akamweleza anayoyaona nje

Mara kijana wake atoke na kuingia kwenye geti dogo(anaenda nje ghafla anarudi) mzee akaanza kuamini hapa usalama ni zero

Mke wake akamfuata mzee akamwambia kuna shughuli kubwa anayo leo ,akimaliza ataenda ale aje kulala yeye akalale muda huo

Basi mzee akakomaaa ikafika saa 7 usiku,akamuona mlinzi kama yupo hoi pale getini kama amelewa vile,akatuma sms kwa maafande,maafande nao wakiwa sita wakawa wamefika mtaani kwa mzee wapo doria ya miguu

Mzee yupo bize kwenye upenyo ,anaona geti linafunguliwa wanaingia vijana watatu na wanaanza kuvaa maski,akawashtua polisi" wameingia"

Ndo mapolisi wakaingia getini wakawaweka chini ya ulinzi

Maafande wakawauliza R yupo wapi. Wakasema hawajui ,wakaingia ndani milango ipo wazi,wakaenda chumba cha R wakamkosa ,,wakaweka ambushi baada ya dakika kama 10 hivi R akawa anakuja na gari ,ile ameshuka wakamteka ,basi wakamwambia mzee toka nje na wakamchukua na mke wake mpaka kituo cha polisi

Baada ya vibano vya mle ndani wakaeleza A to Z na mapanga yao na visu vikakamatwa na sh milioni moja ambayo walikuwa wamelipwa ili baada ya shuguli wapewe milioni moja na laki mbili zilizobaki

Kesi ikaunguruma wakakiri wakapokea mvua ya miaka

Mzee alinishukuru sana,hakuamini ningeweza kumuokoa kiasi kile na akaamini walikuwa wanashea penzi na kijana wake wa kumzaaa

Shukrani ya mzee kwangu ni kumuomba anisaidie niende chuo,nikaenda chuo na kumaliza nipo mtaani ,ila bado tupo mabest na mzee ,

Mzee anaishi na watoto wake wa kike watatu

Mwisho

Nb unaruhusiwa kuuliza ambapo ungependa upewe ufafanuzi
 
Back
Top Bottom