Nimesimamishwa masomo Chuo Kikuu cha Dar es salaam.

Pole sana Mkuu, usiwe na wasiwasi Chadema watakupeleka India ukasome ndio upambanaji hakuna haja ya kulia lia

hahaha :lol::A S 465::lol::lol: mimi nasindwa hata kuhukumu au kulaumu sielewi maana ya kugoma ni nini maana cha zaidi nasikia uhribufu wa mali kumwagia chakula michanga kuwachapa viboko wenzao wanaoingia madarasani kujisomea na mengine neyo yanayoudhi. hivi ndio maana ya migomo na kudai haki kwa kufanya uharibifu? hapohapo wakati wengine wanagoma wengine wa EAC wanasoma je soko la ajira hapo baadaye litakuwa na uwiano wakati kutwa kucha ni migomo na uharibifu.
 
Mkuu pole kwa kusimamishwa masomo. Naona umechanganyikiwa mpaka unaweka quotes zenye wrong spelling. Au hiyo barua ya chuo imekosewa hivyo hivyo? Mmesimamishwa wangapi so far?

Tiba

naona umekuwa FaizaFoxy wa muda. Usijali mkuu, tumesimamishwa 86, na waliofukuzwa ni 13... Ndio kwanza nigundue kuwa kuna waliofukuzwa ambao si wajumbe wa DARUSO.
 
hahaha :lol::A S 465::lol::lol: mimi nasindwa hata kuhukumu au kulaumu sielewi maana ya kugoma ni nini maana cha zaidi nasikia uhribufu wa mali kumwagia chakula michanga kuwachapa viboko wenzao wanaoingia madarasani kujisomea na mengine neyo yanayoudhi. hivi ndio maana ya migomo na kudai haki kwa kufanya uharibifu? hapohapo wakati wengine wanagoma wengine wa EAC wanasoma je soko la ajira hapo baadaye litakuwa na uwiano wakati kutwa kucha ni migomo na uharibifu.

trust me mkuu.
Prof. Mukandala amedanganya umma, maelezo ya barua zetu ni kama yalivyoandikwa hapo juu. Hayo ya kuzuia watu kuingia darasani si ya kweli, na kwa mujibu wa DARUSO, mgomo rasmi ulikuwa haujaanza.
 
pole ndugu yangu yatakwisha! Mwenyewe 2007 pale SUA niliwahi kusimamishwa kwa mambo haya ya uongozi lakin baadae tulipewa barua za kujinasua kwenye tuhuma zilizo tukabiri na baadae kujieleza kwa kamati ya nidhamu na niliruka kimanga kama kawa na tuhuma hizo.. Finally tulisamehewa na kupiga shule kama kawaida hakuna aliyefukuzwa jumla... Be firm usitetereke yataisha tu, wanachofanya viongozi wa chuo ni divide and rule tu otherwise wakikomaa itabidi wanafunzi wenzenu waliobaki wajitoe kwa niaba yenu. All the best
 
Nakupongeza sana kwa moyo wako wa kijasiri, nchi hii itajengwa na watu kama wewe, usikate tamaa, endelea na mapambano popote ulipo, waelimishe na wenzako wote wasikate tamaa, tupo pamoja.
 
nashukuru kwa kunitia moyo mkuu. Mungu awe pamoja nawe, na aangazie ulichokisema...
 
pole ndugu yangu yatakwisha! Mwenyewe 2007 pale SUA niliwahi kusimamishwa kwa mambo haya ya uongozi lakin baadae tulipewa barua za kujinasua kwenye tuhuma zilizo tukabiri na baadae kujieleza kwa kamati ya nidhamu na niliruka kimanga kama kawa na tuhuma hizo.. Finally tulisamehewa na kupiga shule kama kawaida hakuna aliyefukuzwa jumla... Be firm usitetereke yataisha tu, wanachofanya viongozi wa chuo ni divide and rule tu otherwise wakikomaa itabidi wanafunzi wenzenu waliobaki wajitoe kwa niaba yenu. All the best

inshallah Mungu atajalia...
 
Hivi we ritz ni mtu wa aina gani?

Ritz yeyeanawazia tumbo tu, kila jambo ambalo ni kinyume na Serikali kwake yeye linaashiria mkate unaponyoka na analihusisha na CDM (aibu gani!). Hata wanafunzi vyuo vikuu wakigoma ni CDM, Wahadhiri wakigoma ni CDM!
Ritz, fahamu kuwa migomo ni silaha ya wanafunzi wa vyuo (hata sekondari na primary), migomo imekuwepo kabla ya CDM, CCM nk. Migomo imekuwepo tangu enzi ya TANU, Mh Sitta, Warioba na Mkono nao waligoma enzi zao, je walikuwa CDM?
 
Pole sana..kwani naujua uchungu ulionao ila next time kuwa makini ukifukuzwa unakwenda kwenu peke yako wengine wanaenda nkurumah lecture...ila gonjwa la makunji udsm ni la kurithi toka enzi za Samuel sitta
 
Hawawezi kuwafanya werevu wajinga siku zote,pole endelea kupambana kudai haki yako.
 
Ritz yeyeanawazia tumbo tu, kila jambo ambalo ni kinyume na Serikali kwake yeye linaashiria mkate unaponyoka na analihusisha na CDM (aibu gani!). Hata wanafunzi vyuo vikuu wakigoma ni CDM, Wahadhiri wakigoma ni CDM!
Ritz, fahamu kuwa migomo ni silaha ya wanafunzi wa vyuo (hata sekondari na primary), migomo imekuwepo kabla ya CDM, CCM nk. Migomo imekuwepo tangu enzi ya TANU, Mh Sitta, Warioba na Mkono nao waligoma enzi zao, je walikuwa CDM?

Ritz yupo kazini.analipwa pesa ya wavuja jasho kwa kazi hiyo.So msimlaumu sana.
 
Hawawezi kuwafanya werevu wajinga siku zote,pole endelea kupambana kudai haki yako.

mwenye chuo alidai kuwa pale ni sehemu ya kukuza fikra, hivyo kutuondoa sisi ni sehemu ya kukuza hizo fikra na kufanya watu wafikiri kwa uhuru zaidi.
 
Back
Top Bottom