Jimbi
JF-Expert Member
- Aug 16, 2010
- 3,951
- 4,264
watu kama wewe ndio mnatupa taabu na ID zenu nyingi nyingi, afadhali "wamekunyamazisha", argh!!nashukuru mkuu. Jamvini niko muda mrefu, ID tu ndo nimekuja nayo kuwapea taarifa...
watu kama wewe ndio mnatupa taabu na ID zenu nyingi nyingi, afadhali "wamekunyamazisha", argh!!nashukuru mkuu. Jamvini niko muda mrefu, ID tu ndo nimekuja nayo kuwapea taarifa...
Kwema wanajamvi?
Kama kichwa kinavyojieleza, nilipokea ujumbe kutoka ofisi ya Mshauri wa Wanafunzi saa 3 hivi asubuhi, ikinitaarifu kuwa nisubiri chumbani kwangu niletewe barua yangu. Karibu saa 7 hivi, baada ya kusubiri sana uvumilivu ukaniisha, nikaenda Nyerere Campus, nikapata barua yangu pale Auxilliary Police, iliyoeleza, nanukuu, "RE: SUSPENSION FROM STUDIES PENDING INVESTIGATION
Be informed that following your participation in the making of an illegal USRC desicion to defy Council orders, you have been suspended from studies pending futher investigation...", mwisho wa kunukuu. Nikakabidhi kitambulisho cha chuo kwa askari, tukaonana na viongozi wenzangu wa DARUSO, tukafarijiana na kuelekezana cha kufanya wakati huu mgumu.
Saa 11 jioni nikawa Mabibo Hostel kufanya taratibu zote za kuondoka chuoni, saa 11:30 hivi nikaondoka maeneo ya hostel kurudi nyumbani, ninakoishi.
Hii ni ID mpya, anayehitaji taarifa zaidi ani-PM.
nashukuru sana mkuu kwa kunijali. Mimi ni Mtanganyika, usitishike na hayo maneno hapo juu...
Tatizo la watu wazembe wa kufikiri. Nenda UDSM ukafanye research u will get the truth na usitegemee taarifa kutoka kwa TBC1, Star TV na n.khahaha :lol::A S 465::lol::lol: mimi nasindwa hata kuhukumu au kulaumu sielewi maana ya kugoma ni nini maana cha zaidi nasikia uhribufu wa mali kumwagia chakula michanga kuwachapa viboko wenzao wanaoingia madarasani kujisomea na mengine neyo yanayoudhi. hivi ndio maana ya migomo na kudai haki kwa kufanya uharibifu? hapohapo wakati wengine wanagoma wengine wa EAC wanasoma je soko la ajira hapo baadaye litakuwa na uwiano wakati kutwa kucha ni migomo na uharibifu.
Usife moyo, utarudi shule, kwa sasa tafuta shughuli ya kufanya ujipange upya
nashukuru kwa upendo wako mkuu. Ila hata nikirudishwa masomoni, itanifaa nini endapo wenzangu 98+41 hawatarudishwa, itanifaa nini endapo umma wa UDSM, ambako kulitakiwa kuwa kitovu cha mafikara, utaendelea kugandamizwa kimawazo na watawala wetu wakishirikiana na wakuu wa vyuo?
Nadhani ipo jinsi mkuu, zaidi ya kutegemea huruma ya MUUMBA.
Watanzania ni uvumilivu...ujinga kama huu ungefanyika elsewhere mambo yangekuwa ni magumu sana.Otherwise stand firm brother,hope you will stand!! Naumia wakuu natamani hata kufa,hali hii mpaka lini?
Wanafunzi lazima kila siku mkumbuke kuwa kile kilichowapeleka chuoni ni kusoma. Hicho ndicho kitu cha kwanza. Mambo ya siasa yapo uraiani mtayakuta mtakapomaliza shule. Mimi siungi mkono hata siku moja njia mnayotumia kudai haki zenu kama vile kwa kuwalazimisha wanafunzi wasioafiki matakwa yenu kwa kuwafukuza madarasani.
wewe kijana wa nape, inatosha sasaHivi bado hamjamstukia huyu Sobhuza? hata lugha yake inaonesha kabisa kuwa huyu si Mtanzania na yupo hapa kutia fitna. Nawashangaa sana ambao bado mnamuunga mkono.
Mimi nnapinga huyu si mwanafunzi wa UDSM na wala hajafukuzwa chuo.