Kwenu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

JipuKubwa

JF-Expert Member
Jun 1, 2013
2,311
2,324
Habari wana jukwaa, moja kwa moja kwenye hoja.

Katika pitapita zangu hapa mjini 'Daslam' juzi jioni nikapita kwa wauzaji wa maandazi, keki,vitumbua na michapati kama yote. Baada ya malipo nikafungiwa bidhaa zangu huyo hadi home. Baada ya kufungua...hamad !,nilistuka baada ya kugundua mfuko uliotumika ni barua ya mwana chuo wa UDSM anayeishi Mabibo Hostel tena imeandikwa mwezi huu 02/03/2020 kwa warden na imepokelewa pamoja na kugongwa muhuri.

Maswali ninayojiuliza; hivi barua hazitunzwi baada ya kupokelewa kwa wahusika?

Barua zinafikaje kirahisi hivi mtaani?

Nchi inauhaba sana wa karatasi kutengeneza vifungashio?

Je nini kifanyike kuondokana na hii hali?

Naamini kupitia uzi huu,wanabodi tunaomba mawazo yenu ili tukisaidie chuo changu pendwa miaka hiyo enzi za 'Revo square'.

#Corona#

Nawasilisha.


ice_2020-03-23-23-16-32-849.jpeg
Screenshot_20200326-155831.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Labda me ndo nimesahau, nimekaa Block C Mabibo 2016-2018 two years pale ndani, mwaka wa mwisho nlitokea home....

Ikifika time ya kufunga chuo ( either likizo ya semester I au mwaka mzima) wakati wa kutoka na vitu nje ya hostel unatakiwa uwe na hiyo barua yenye muhuli wa warden kuonyesha kama amekuruhusu kutoka nje ya block lake na vitu vyako ulivyoorodhesha na kumuonesha...

Good enough barua humuachii auxiliary pale getini, unasepa nayo after showing them kwahiyo sio mbaya kama alifika nayo hadi nyumbani akampa bi mkubwa wake akafanye vifungashio.... labda kama ziko nyingi basi hapo ndo zinapoishia

labda uniambie system wamebadilisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiki c huo nilikiona ni taka taka baada ya kumleta Meko

Yani hatutakuja kukisamehe hiki chuo.
Kimetuletea 🚮
 
kifusi boy,
Siku hizi utaratibu ni kwamba wale vijana wa Suma JKT wa getini wanapaswa kuzikusanya hizo barua na kuzihifadhi sehemu salama na sio kila mwenye barua kuondoka nayo.
 
Nimegundua hawa wamama huenda kukusanya makaratasi pale getini baada ya kukusanywa na wale walinzi kutoka kwa wanafunzi. Ni vizuri utaratibu huu ukaangaliwa upya.
 
Back
Top Bottom