Mphamvu
JF-Expert Member
- Jan 28, 2011
- 10,702
- 3,288
Kwema wanajamvi?
Kama kichwa kinavyojieleza, nilipokea ujumbe kutoka ofisi ya Mshauri wa Wanafunzi saa 3 hivi asubuhi, ikinitaarifu kuwa nisubiri chumbani kwangu niletewe barua yangu. Karibu saa 7 hivi, baada ya kusubiri sana uvumilivu ukaniisha, nikaenda Nyerere Campus, nikapata barua yangu pale Auxilliary Police, iliyoeleza, nanukuu, "RE: SUSPENSION FROM STUDIES PENDING INVESTIGATION
Be informed that following your participation in the making of an illegal USRC desicion to defy Council orders, you have been suspended from studies pending futher investigation...", mwisho wa kunukuu. Nikakabidhi kitambulisho cha chuo kwa askari, tukaonana na viongozi wenzangu wa DARUSO, tukafarijiana na kuelekezana cha kufanya wakati huu mgumu.
Saa 11 jioni nikawa Mabibo Hostel kufanya taratibu zote za kuondoka chuoni, saa 11:30 hivi nikaondoka maeneo ya hostel kurudi nyumbani, ninakoishi.
Hii ni ID mpya, anayehitaji taarifa zaidi ani-PM.