Nimeshuhudia baadhi ya wachaga na wakinga wanaacha ajira nzuri wanaingia mazima biashara ambazo zina hatari ya hasara, huu ujasiri wanautoa wapi?

Ajira zina utumwa fulani ndani yake, pia huwezi kutajirika kwa ajira hasa usipofikia ngazi za umeneja au director katika taasisi kubwa.
 
Ni baadhi yao,,, sio wote

Wengi wetu tulitamani hata hizo ajira tuzipate tuwe na mishahara ya uhakika kila mwezi maana huku mitaani hakueleweki.

Kuna makabila yenye wasomi kama wahaya, wasukuma, wangoni, wanyakyusa, hawa wakilamba kazi shughuli imeisha, mshahara wa uhakika kwao upo sasa kwenda kwenye bishara ambako kuna hatari za hasara kuna maana gani ??

Tofauti na hayo makabila, kuna wachaga ambao wengi wameelimika na kuna hawa wakinga ambao kiwango cha walioelimika ni kawaida lakini unakuta hao walioelimika na kufanikiwa kupata ajira badala ya kutegemea mishahara kama wengine wao wanaacha kabisa ajira na kujiingiza miguu yote kwenye biashara ambazo zina hatari (risk) ya hasara..

Nimeona mkinga ni branch manager wa bank flani ana gari nzuri tu na ni kijana kaacha ajira kafungua duka lake.

Nimeona mchaga huyo alikuwa TRA, narudia jamani TRA, mshahara safi tu lakini akaacha kazi kwenda kwenye biashara ya restarants

Nimeona mkinga ni daktari, mshahara milioni na kitu kaacha kazi kaenda huko maporini anafuga mifugo ya nyama na maziwa.

Nimeona mchaga marehemu Mengi akiwa mhasibu wa kwanza kutambulika hapa nchini akiacha ajira nono.

Nimeona mkinga huyu kijana vunja bei kaelimika lakini aliacha ajira yake yenye mshahara wa uhakika, majuzi happ naskia alipata hasara kwenye ule mkataba wa bilioni 2 wa jezi za simba
Umeanza vizuri ukamaliza vibaya na vunjabei
 
porojo.....hizo story ndio kichaka cha wakinga wengi....huzitumia ili kuwahadaa baadhi ya watu wanaohoji chanzo cha biashara zao.

kama unadhani kupanda miti ndio kunawatajirisha wakinga, na wewe kijijini kwenu anza kumpandia miti mwanao wa miaka 5 ili akiwa mtu mzima aanzenayo kama mtaji wa biashara.

Miti ina mazingira yake.. mwingine kijijini kwao singida ama bariadi.. sasa anaanzaje panda miti ya mbao huko singida ama bariadi?
 
Back
Top Bottom