Kwenu wazazi mnaosomesha Watoto, Msisitize watoto wasomee Udaktari, Sheria, Engineer ama Uhasibu. Soko la ajira ni gumu ila huku kuna Nafuu

R-K-O

JF-Expert Member
Jun 27, 2023
482
2,138
Doctor, engineer au Lawyer ikishindikana angalau somea uhasibu.

Niseme tu ya kwamba wapo wanaosomea hata degree ya kichina wanapata ajira hapahapa Tanzania lakini Probability (makadirio ya uwezekano) ya kupata hizo kazi ni ndogo.

Lakini hizi kozi tajwa angalau zina Probability (makadirio ya uwezekano) nzuri ya kuajiriwa sambamba na malipo mazuri, vijana wengi tu wapo makazini kwenye hizi kazi na hali zao kiuchumi si haba. Haimaanishi kwamba wooooote wanaajiriwa ama kujiajiri, LA HASHA!! wengine wanasugua benchi mtaani lakini kozi hizi angalau zina nafuu kwenye Probability (makadirio ya uwezekano) ya kuajiriwa ama kujiajiri, Mambo hayana formula lakini ni vema kufanya kitu walau kina Probability (makadirio ya uwezekano) nzuri, hata kwenye muziki yupo Diamond platnumz lakini probability ya mtu aliemaliza form 4 aanze kuimba ategemee muziki pekee kuendesha maisha ni ndogo sana, ni heri adungue mgahawa wake angalau kuna Probability nzuri ya uhakika wa kuendesha maisha yake.

Madaktari wana bodi yao Medical Council of Tanganyika, lazima ufuzu mitihani ya bodi hii ukiachana na ile ya chuo, jina la daktari linaanza kwa Md flani. Afya ndio mtaji jamani, Uhitaji wao ni mkubwa, mishahara yao si haba, na mtu akiweza kujiajiri afungue hata sehemu yake kama zahahanati ni jambo la neema kwa jamii maana huduma za afya bado zipo chache.

Engineers wana bodi yao, Engineers Registration Board, lazima ufuzu mitihani ya bodi hii ukiachana na ile ya chuo, jina la daktari linaanza kwa Eng, flani. hawa ndio mafundi mitambo, wahandisi wa barabara, wanaojenga majengo, wahandisi wa computer, n.k. huku waliojaa wengi ni wanaume tofauti na kwengine, kwa wanawake nadhani huwa wanapata upendeleo maalum kwenya ajira.

wanasheria wana bodi yao, Tanganyika law society, lazima ufuzu mitihani ya bodi hii ukiachana na ile ya chuo, jina linaanza kwa wakili flani. hapa wapo wale mapilato wanaotembelea gari zimeandikwa J, wapo washauri wa sheria wa kulipwa, wapo mawakili, wapo wenye law firms zao, n.k. asikwambie mtu yani watu wapo tayari kutoa chochote kukwepa maisha nyuma ya nondo, kudai haki zao, kujitetea, n.k. wanasheria ndio wanufaika hapa.

wahasibu wana bodi yao, National board of accountants and auditors, lazima ufuzu mitihani ya bodi hii ukiachana na ile ya chuo, jina la mhasibu linaanza kwa Cpa flani. ndio wanaohusika na usimamizi wa fedha kuanzia mapato, matumizi, faida , n.k. wapo kwa wingi karibu kila shirika maana pesa bila usimamizi ni hatari, kwa cpa kima cha chini cha mshahara inasemekana ni milioni 1.3, kwenye kujiajiri kuna accounting firms hawa ndio wanahusika na kusimamia hesabu za makampuni, kusaidia watu kupeleka tax returns TRA, n.k. pesa ipo.

Ni kipimo cha kuonyesha uzito wa haya mambo, bodi hizi zipo tangu zamani na ili uwe mwanachama inabidi ufanye mitihani yao.

Pia ni inapendeza kuanza kusomea taaluma mapema vyuoni baada ya kuhitimu form 4, diploma miaka mitatu kisha unaingia degree pamoja na wale waliotokea sekondari form 6, kumbuka form 6 ni elimu ya sekondari wala sio elimu ya taaluma ndio maana mtu aliesoma form hawezi kuajiriwa bila degree lakini mwenye Diploma anaweza kupata ajira bila degree, Pia kazi za degree ni za wote waliotokea form 6 kwenda degree na wale form 4>diploma>degree lakini kazi za diploma ni maalum kwajili ya walioanza kusoma chuo baada ya form 4, nchi zilizoendelea kama Kenya walishafuta form 5 na 6 ni moja kwa moja kuanza kusomea taaluma chuoni.

Wanaijeria ndio jamii ya waafrika walioelimika zaidi wanasisistiza watoto wao wasomee Doctor, Lawyer ama Engineer, waisrael na wahindi ndio makundi yenye wasomi zaidi wanasisitiza watoto wao wasomee Doctor, engineer ama Lawyer,
 
Doctor, engineer ama Lawyer ikishindikana angalau somea uhasibu

Wengi wakiwa sekondari husomea masomo hushindwa kujua hata wanataka kusomea taaluma ipi ila kwa kurahisisha hizo ndio taaluma kuu zenye unafuu katika career path aidha kuajiriwa ama kujiajiri.

Madaktari wa bodi yao, engineers wana bodi yao, wahasibu wana bodi yao, wanasheria wana bodi yao. Ni kipimo cha kuonyesha uzito wa haya mambo.

Wanaijeria ndio kundi la waafrika wenye maendeleo marekani na ulaya wanasisistiza watoto wao wasomee ikishindikana angalau uwe accountant, waisrael na wahindi ndio makundi yenye mafanikio zaidi Marekani wanasisitiza watoto wao wasomee Doctor, engineer ama Lawyer ikishindikana angalau uwe accountant
Bado Sana Dr sio kitu kwa sasa.

Kuna Dental,radiology,nurse anesthesia,opthalmologist,
 
Doctor, engineer ama Lawyer ikishindikana angalau somea uhasibu

Wengi wakiwa sekondari husomea masomo hushindwa kujua hata wanataka kusomea taaluma ipi ila kwa kurahisisha hizo ndio taaluma kuu zenye unafuu katika career path aidha kuajiriwa ama kujiajiri.

Madaktari wa bodi yao, engineers wana bodi yao, wahasibu wana bodi yao, wanasheria wana bodi yao. Ni kipimo cha kuonyesha uzito wa haya mambo.

Wanaijeria ndio kundi la waafrika wenye maendeleo marekani na ulaya wanasisistiza watoto wao wasomee ikishindikana angalau uwe accountant, waisrael na wahindi ndio makundi yenye mafanikio zaidi Marekani wanasisitiza watoto wao wasomee Doctor, engineer ama Lawyer ikishindikana angalau uwe accountant
Ili iwe.fani ya afya lazima iwe na bodi.

Course zote za afya ni markatable.
 
kwamfano mtoto akienda chuo mojakwamoja akitokea kidato channe bila kwenda five vipi anaweza kuajiriwa naatakuwa ameiva viziri mana anaenda kusomea udaktari.
Peleka chuo, hizo 5 & 6 sioni mantiki yake isipokuwa tu kama mtu hana uwezo wa kulipa ada chuoni basi apitie huku

Form 5 na 6 ni elimu ya sekondari, Chuoni ni elimu ya Taaluma, mtu akianza chuo mapema anakuwa ameanza kujifunza taaluma mapema, huko form 5 na 6 watu wazima wanatembezewa bakora 🤣🤣 hawanaga hata field za kufanya kazi kwa vitendo maofisini, Anaeanzia chuo baada ya form 4 anaweza kupata ajira akishindwa kuendelea degree lakini form 6 hawezi kupata ajira akishindwa kuendelea degree, alafu ni kwamba mtu akianza chuo baada ya form 4 ana uwanja mpana wa ajira kuliko anaeenda degree baada ya form 6
 
Computer engineering ina soko kubwa zaidi, ndio kozi baba kwenye mambo ya computer ikifuatiwa na hizo zingine.

Compuuterengineer anaweza kuwa fundi mitambo pia kwenye hardware, ama hata fundi wa simu na laptops upande wa software na hardware.

Computer haina hela kwenye hard ware.

Computer ina hela kwenye digital ama softwares.

Watengeneza apps, watu wa digital security, system administrators hawalali njaa hata siku moja.

Hata hii jamiiforums kuna wahuni kibao wanapiga nayo hela kwa kuilinda iwe hewani tu kina sisi tu comment
 
Kuna wanaosoma hizo course na bado wanasugua benchi mtaani au la wanafanya vitu tofauti na walivyosomea. Na kuna wengine wamesomea course ambazo hazina nafasi nyingi za ajira lakini wao wameajiriwa kwa transcripts tu bila ya cheti official kutoka..

Kiufupi muhimize mtu kwa chochote anachokichagua awe nondo na sio kwa GPA tu, akipata vilikizo aende field hata kwa kujitolea ili awe exposed na skills zinazohitajika lakini pia kutengeneza CV yake mapema. Nilichogundua ni rahisi ofisi kutoa nafasi kwa undergraduates kuliko wale waliomaliza ili kuepuka attachment na demands za pesa..

Kingine ni soft skills, asitumie Wi-fi ya chuo kudownload movies, kuna course kibao anaweza kujifunza tena for free na zikampa cha kuanzia street kuliko degree yake 🙏🏽🙏🏽

By the way kwa course ulizozitaja, hata nikiamua kurudi darasani, ni kheri nikachukue hata IT maana ndo dunia inapoelekea
 
Computer haina hela kwenye hard ware.

Computer ina hela kwenye digital ama softwares.

Watengeneza apps, watu wa digital security, system administrators hawalali njaa hata siku moja.

Hata hii jamiiforums kuna wahuni kibao wanapiga nayo hela kwa kuilinda iwe hewani tu kina sisi ku comment
computer engineering wana piga hadi hizo software lakini wao cha ziada wanajifunza hardware na umeme kwahio wana advantage zaidi, wanaweza kuomba kazi za kozi nyingine hizo lakini hao wa kozi zingine ni ngumu kuomba kazi za computer engineers

Mfano kazi za hii mitambo ya mitandao ya simu ni computer engineers na wale wa telecommunications ndio wana sifa.

Mafundi wa electronics hawa wanaendesha maisha vizuri tu kutengeneza simu, laptops, tv, radio, n.k.
 
Kuna wanaosoma hizo course na bado wanasugua benchi mtaani au la wanafanya vitu tofauti na walivyosomea. Na kuna wengine wamesomea course ambazo hazina nafasi nyingi za ajira lakini wao wameajiriwa kwa transcripts tu bila ya cheti official kutoka..

Kiufupi muhimize mtu kwa chochote anachokichagua awe nondo na sio kwa GPA tu, akipata vilikizo aende field hata kwa kujitolea ili awe exposed na skills zinazohitajika lakini pia kutengeneza CV yake mapema. Nilichogundua ni rahisi ofisi kutoa nafasi kwa undergraduates kuliko wale waliomaliza ili kuepuka attachment na demands za pesa..

Kingine ni soft skills, asitumie Wi-fi ya chuo kudownload movies, kuna course kibao anaweza kujifunza tena for free na zikampa cha kuanzia street kuliko degree yake 🙏🏽🙏🏽

By the way kwa course ulizozitaja, hata nikiamua kurudi darasani, ni kheri nikachukue hata IT maana ndo dunia inapoelekea
Makumbusho na Kariakoo zimejaza wauza simu wengi wenye MD zao na ajira hawajapata sijui nani anapata audacity ya kumshawishi mtu asome kitu fulani sababu kuna ajira ya uhakika. Msimamo wangu kwa wanaosoma ni huu:

1. Soma kitu unachoweza. Usisome kitu kigumu kisa umaarufu au kuonekana gangwe, utatumia gharama nyingi, muda mwingi na uwe average tu kwenye industry. Utakuwa yule daktari anafanya kazi hospitali ya serikali tu hana vituo vya pembeni sababu ni very average kwenye competitive market.

2. Soma unachopenda na uwe na vision nacho. Ukipenda kitu unakifanya kwa ufanisi zaidi, unafaulu kirahisi na unajua potentials zake, future yake, vitu visivyoonekana kwa wengine. Passion ni muhimu kuliko kulazimisha. Usifuate ndoto za wazazi. Mzazi unakuta alitamani awe Engineer masomo yakampiga sasa analazimisha uwe Engineer wakati uwezo huna, mzazi anataka cheo cha kutamkika akatambe kwenye jumuiya wakati wewe ni matter of life. Unless huyo mzazi ni 'muelewa' wa situation ilivyo na atachangia kukua kwako, kama yuko sekta fulani akikushawishi basi anamaanisha.

3. Soma kitu ukijua kuna kuajiriwa au kutoajiriwa. Ukisoma kwa kutegemea kuajiriwa ndio yaleyale ya Petroleum Engineering mtu ana ufaulu wa juu sana ila ana njaa mfukoni kisa hakuna ajira. Mtu aliyesoma Accounting ana uwezo mkubwa sana kujiajiri kuliko aliyesoma Pharmacy. Nina jamaa yangu alisoma Accounting akaiva akaenda kwa ndugu yake nani uko kufundishwa Auditing na vitu vya hivyo, anapiga Audit ya mtaani na anaenda ofisi kwa ndugu yake yuko certified kuchukua mhuri na saini. Hela nyingi anapata (mfano una kampuni uchwara zile mnafungua kwa kiherehere haijauza nusu mwaka unataka kufile tax ile kitendo cha kuthibitisha hujauza kitu unamlipa sijui 50,000 sijui 30,000), yeye alikosa kazi akaamua aongeze skills chache kwenye fani yake. Sasa Pharmacist ukikosa kazi utauza dawa za kienyeji kama application ya ulichosoma?
Mtaji wa kufungua Pharmacy ni mkubwa, huyo jamaa alianzia ghetto kwake na meza, kiti na laptop na vitabu vyao.

4. Usisome kitu kimoja kama unatafuta ufalme wa mbinguni. Soma alafu kuwa na skill nyingine kama graphics, photography, drawing, beautician kama ni mtoto wa kike, n.k. Nina mate wangu alisoma diploma ya Engineering ila ni DJ na analipwa vizuri kwenye u-DJ kuliko kwenye kulishwa vumbi uko kwa mafundi mchundo, na anafanya kazi sehemu nyingi. Side hustle inakusaidia kupata hela wakati umekosa ajira mwanzoni na inakusaidia ukiwa kwenye ajira vilevile. Hata ukipata hela unajua business gani ufanye, kama ni binti anajua ususi akienda kwenye ajira akapata hela anajua mtaji kiasi gani ananunua nini na nini anaanzisha kiofisi anaweka mtu.

N.B: Wakati namaliza chuo Magufuli alishafariki. Ushauri wangu 'ni wa kisasa' unaendana na mazingira ya sasa.
 
Number 4 📌📌📌
 
Back
Top Bottom