Nimeshangaa kule Tanzania kumbe kuna shule za serikali ambazo ni English medium,. Wenzetu mbona huwa wanajikanganya hivi?

Wewe jamaa lofa sana. Hujui english medium schools ziko kwenye nchi zote ambazo zinathamini lugha zao za asili? Hebu search hata haya maneno matatu tu: english + medium + schools halafu uone majibu.

huyu jamaa ni kama zile nyama zinzitwa bawasiri, anawashwa balaa na issue za TZ.
 
Hizo shule hapa Bongo zipo. In fact binti yangu anasoma kwenye Gov't English Medium school ila sasa tatizo, quality of education ipo chini sana. Kingine ni idadi ya wanafunzi wanaosoma kwenye hizi shule kwa kila darasa ........... wueh!!!!!!!!! Acha tu!!!
Kiingereza kinapanda lakini kwa kijana, au na chenyewe chini sana?a
 
Kuna uzi nimekutana nawo humu unaongelea kuhusu shule za serikali ambazo ni English medium, nikawa nachanganyikiwa, maana Watz haswa walalahoi wote huwa wameaminishwa Kingereza ni cha mkoloni mara sijui ni cha malkia, hivyo watoto wao wapelekwe kusomea kwenye shule za st Kayumba, ilhali wenye hela zao na hata viongozi wapeleke watoto wao kwa shule binafsi za English medium, ila kumbe kunazo pia za serikali na zinazotumia mtaala mmoja japo zina ada ya gharama.

Ndugu zetu hiki kingereza mtakizunguka na kukitukana na kujifanya kukichukia ila hakikwepeki kwenye utandawazi wa leo, mambo ya "sizitaki mbichi" yamepitwa na wakati.... suluhisho ni kucaha uzembe na kukisomea

Shule za English medium za serikali | JamiiForums

Kuna huu uzi mwingine ambao naona jamaa ameandia kwa uchungu sana kuhusu hilo hilo JAMHURI YA WOGA! | JamiiForums
Ubongo wako bado umetawaliwa na wazungu, Lughayetu ya taifa ni kiswahili, umeshawahi kumcheka Mzungu kwa sababu hajui kiswahili?? Tafakari
 
Hatuwacheki kwa kutokujua Kingereza (japo inapaswa mchekwe, utasomeaje kitu miaka yote na kikushinde), ila hizo mbwembwe zenu kwamba kikiwashinda mnaanza kusema hata hakina maana, ni cha mkoloni, mara nyie sio watumwa, sizitaki mbichi ze ze ze.....

Inapaswa uwe mjanja wa lugha, Kiswahili nakipenda, na ndio lugha yetu ya taifa ila kina mwisho wake, nikitaka kupiga dili na Mghana au Mchina inabidi tuhamie kwenye Kingereza, sasa ukiwa na changamoto kama namna huwa kinawapiga chenga huko inakua majanga.
 
Inapaswa uwe mjanja wa lugha, Kiswahili nakipenda, na ndio lugha yetu ya taifa ila kina mwisho wake, nikitaka kupiga dili na Mghana au Mchina inabidi tuhamie kwenye Kingereza, sasa ukiwa na changamoto kama namna huwa kinawapiga chenga huko inakua maja

Hahaaa, no deal there brother
 
Kiingereza kinapanda lakini kwa kijana, au na chenyewe chini sana?a
Yuko poa ingawa namfanyia coaching nyumbani. Isingekuwa hivyo, anfefanya madudu tu shuleni kwa sababu pia sio walimu wrote wako poa kiingereza. Wengine wanalipua tu.
 
Hatuwacheki kwa kutokujua Kingereza (japo inapaswa mchekwe, utasomeaje kitu miaka yote na kikushinde), ila hizo mbwembwe zenu kwamba kikiwashinda mnaanza kusema hata hakina maana, ni cha mkoloni, mara nyie sio watumwa, sizitaki mbichi ze ze ze.....

Inapaswa uwe mjanja wa lugha, Kiswahili nakipenda, na ndio lugha yetu ya taifa ila kina mwisho wake, nikitaka kupiga dili na Mghana au Mchina inabidi tuhamie kwenye Kingereza, sasa ukiwa na changamoto kama namna huwa kinawapiga chenga huko inakua majanga.
Ni wazungu wengi pia hawajui kingereza, wengine hata cha kununulia soda dukani kinawapiga chenga. Lakini hawachekani
Ni nini hii waafrika?
Ukiacha hii ya wakenya na watanzania lakini pia ipo ya watanzania kwa watanzania.
Ni vizuri kujifunza lugha ngeni, kuchekana kwa kutojua lugha ngeni nadhani ni ushamba tu.
 
Hao wazungu hawaendi shule kujifunza kingereza tangu utotoni, kwa mfano Urusi kingereza hakipo kwenye mtaala wao wa taifa. Lakini hapo Tanzania huwa hamueleweki eleweki, kuna wale wanasomea kingereza tangu chekechea huku wengine wakiambiwa hakina maana ni cha mkoloni, haswa walalahoi wa Tandale.
 
Wakenya mnachachawa sana na lugha ya English ilhali huku bongo, wasomi wengi wanazidi kurealize we have to grow our own swahili, nyie bakini na ujinga wenu.
 
Hao wazungu hawaendi shule kujifunza kingereza tangu utotoni, kwa mfano Urusi kingereza hakipo kwenye mtaala wao wa taifa. Lakini hapo Tanzania huwa hamueleweki eleweki, kuna wale wanasomea kingereza tangu chekechea huku wengine wakiambiwa hakina maana ni cha mkoloni, haswa walalahoi wa Tandale.
Na acha uongo, urusi wanajifunza English, na ipo kwenye mtalala wao, na Kuna vyuo vinafundisha kwa English language.
 
Hehehe!! Umeweseka kuni-quote mara nyingi, tuliza moto....
Urusi huwapa wanafunzi uhuru wa kuchagua lugha ya kigeni wanayotaka kufundishwa, kingereza sio lazima, sio kama hapo kwenu miaka saba unahangaika st. Kayumba bila kingereza kisha unakuja kulazimishwa kwenye shule ya sekondari, huwa sijui mkoje kwa kweli, halafu kikikushinda unasema cha mkoloni kwamba wewe sio mtumwa, kisha ukipata kazi unaletewa limkataba kurasa 800 limeandikwa kwa kingereza unatia saini tu madini yanaliwa...http://worldenglishinrussia.weebly.com/education.html
 
Ngoja niandikie insha,
Ww ndugu huwaga ni zero brain kwenye hii area, na huo ujinga umesambaa Kenya, kitu napenda, Russian ni lugha ya kitambo sana kukilinganisha na kiswahili, huko tutafika tu, fuatilia #elimika weekend ya hii weekend ilopita, Twitter , Tz hakukuwa na namna ingine zaidi ya kusoma English, secondary education, bcoz the world was already too advanced technology wise na use of English ilishasambaa, on top of England kuwa mkoloni wetu designated one, na kiswahili kikiwa ni lugha changa sana, hatungeweza kuikwepa English.
But that was nyerere's era, we're catching up to the so called big language, sasa hivi kinazidi kukua, sasa hivi Tz ukibonga bonga English unakera watu. People ziko proud na kwao na lugha yao na vitu vyao, hata kama havitoshelezi, tunajiitaga maskini jeuri. Hakuna kitu kitakaa juu ya hiyo pride, kwa iyo, a normal Tz akiona venye mnakitukuza, huwaga tunawadharau tu, cha ajabu wakenya wengi ni viewers wa swahili music and drama from Tz. So it's like deep down your soul guts y'all know swahili is the og, lkn ile brainwashed soul ndio bado inapinga pinga. Ujinga mtupu.
 
So kumbe zwazwa unajua umuhimu wa English, tatizo kikiwashinda huwa mnasema cha mkoloni, sizitaki mbichi, halafu walalahoi kama wewe ndio huaminishwa huo ujinga, huku wenye hela wakituma watoto wao waje kusomea Kenya, wakirudi huko wanahodhi nafasi zote za ajira.
 
Hao wazungu hawaendi shule kujifunza kingereza tangu utotoni, kwa mfano Urusi kingereza hakipo kwenye mtaala wao wa taifa. Lakini hapo Tanzania huwa hamueleweki eleweki, kuna wale wanasomea kingereza tangu chekechea huku wengine wakiambiwa hakina maana ni cha mkoloni, haswa walalahoi wa Tandale.
Tanzania kingereza kinafundishwa shule tu. Mtaani lugha ni kiswahili. Mtu anajua kingereza kutokana na madarasa aliyohudhuria pamoja na mazingira.
Ni kwa sababu kama hizo uelewa wa lugha mbalimbali hutofautiana.

Wajerumani, Wafaransa, Waspaniola, wengi wasio waingereza kingereza chao ni tabu tupu. Ni wachache wachache kama Tz tu wanaoweza kuwa fluent.

Hukuti wanachekana zaidi ya kusifiana kuwa umejitahidi.

Ila waafrika ushamba si wa lugha pekee bali ni mambo mbalimbali.
 
Hao Wafaransa au Wajerumani wasio waingereza utakuta kwao huko kingereza hakitumiki kama lugha ya kwenye mikataba ya kiserikali, hawana ujuha huo wa kusuasua kwenye lugha, ambapo haieleweki kama itumike au isitumike, inafundishwa shuleni kwa baadhi yenu na bado inatumika kama kigezo kwenye baadhi ya ajira.

Kwa hao Wajerumani, Kingereza hakina umuhmu mkubwa kitaifa, wao hufanya maamuzi ya kila kitu kwenye lugha yao ya Kijerumani, kwa hivyo Mjerumani kujifunza Kingereza ni kama mimi niamue kujifunza Kisomali.

Sasa nyie hapo, mtu unajitutumua kingereza shuleni, kikikushinda unasema lugha ya mkoloni haina maana kwako, ilhali ndio hiyo hiyo inatumika kuwanyonya kwenye mikataba ya hovyo.
 
Mikataba mibovu ni kwasababu ya ufisadi siyo kingereza.
Kingereza cha kusomea na kuelewa mikataba hicho si tatizo kabisa.
 
Back
Top Bottom