Nimeshangaa kule Tanzania kumbe kuna shule za serikali ambazo ni English medium,. Wenzetu mbona huwa wanajikanganya hivi?

MK254

JF-Expert Member
May 11, 2013
31,517
47,756
Kuna uzi nimekutana nawo humu unaongelea kuhusu shule za serikali ambazo ni English medium, nikawa nachanganyikiwa, maana Watz haswa walalahoi wote huwa wameaminishwa Kingereza ni cha mkoloni mara sijui ni cha malkia, hivyo watoto wao wapelekwe kusomea kwenye shule za st Kayumba, ilhali wenye hela zao na hata viongozi wapeleke watoto wao kwa shule binafsi za English medium, ila kumbe kunazo pia za serikali na zinazotumia mtaala mmoja japo zina ada ya gharama.

Ndugu zetu hiki kingereza mtakizunguka na kukitukana na kujifanya kukichukia ila hakikwepeki kwenye utandawazi wa leo, mambo ya "sizitaki mbichi" yamepitwa na wakati.... suluhisho ni kucaha uzembe na kukisomea

Shule za English medium za serikali | JamiiForums

Kuna huu uzi mwingine ambao naona jamaa ameandia kwa uchungu sana kuhusu hilo hilo JAMHURI YA WOGA! | JamiiForums
 
Nyang'au unababaika na Kiingereza kama nyani na ndizi!

Asubuhi yote hii watu wanatafuta pesa wewe umeng'ang'ana na viingereza!

Kweli ukoloni umegota kwenye kundule! Hahahahaaa

Haswa wewe siku nyingi nakuambia ujifunze Kingereza maana huwa unatia huruma sana....raha ya kuandika na kuongea kingereza asikuambie mtu.

Wenzako wenye hela wanakesha wakijifunza ilhali wewe umeganda hapo Buza ukijiaminisha ni cha mkoloni.
 
Kiinglishi ni kwa watoto wa matajiri, kiswahili ni kwa watoto wa walala hoi. Inaitwa sisiemu hiyo.

Hehehe huwa wanaambiwa uzalendo ni kuchukia Kingereza, njemba linasoma kuanzia chekechea hadi shule ya upili ndio linashtukizwa na Kingereza, halafu matangazo ya ajira huchomekewa "Lazima ujue kusoma na kuandika Kingereza" Watoto wa matajiri wanapeta freshi tu, ilhali njemba linaganda na ze ze ze.

Halafu hawa hutia huruma maana hata lugha zao za asili hawazijui, unakutana na mtu mzima tena aliyeota mvi kichwani lakini hajui hata salamu kwa lugha yake ya asili, na ukiangalia uandishi wao hata wa Kiswahili, hutia kinyaa.
 
Hehehe huwa wanaambiwa uzalendo ni kuchukia Kingereza, njemba linasoma kuanzia chekechea hadi shule ya upili ndio linashtukizwa na Kingereza, halafu matangazo ya ajira huchomekewa "Lazima ujue kusoma na kuandika Kingereza"..... Watoto wa matajiri wanapeta freshi tu, ilhali njemba linaganda na ze ze ze.....
Halafu hawa hutia huruma maana hata lugha zao za asili hawazijui, unakutana na mtu mzima tena aliyeota mvi kichwani lakini hajui hata salamu kwa lugha yake ya asili, na ukiangalia uandishi wao hata wa Kiswahili, hutia kinyaa.
MK254 hamia Bongo mazima manake una nondo za huku hadi za Tandale!
 
MK254 hamia Bongo mazima manake una nondo za huku hadi za Tandale!

Hehehe ndio zangu hizo, unikute natiririka Kipemba au lafudhi ya Kimombasa Mombasa.... kwanza hizo lafudhi mbili Kipemba na Kimombasa hudatisha dada zetu sana huku, wanapenda.

Japo pia mimi hubadilisha kulingana na mazingira, nikiwa na vijana mjini huwa nalonga kwa sheng, nikikwenda kuwasabahi wazee nashushia kwa kilugha changu cha asili.

Lakini ofisini natema yai hadi raha.
 
Ikikushinda kisa uzembe wako....unaitusi.....
Ona ndugu zako Natetemeka/Kigugumizi nikiongea Kiingereza
Hii inatokea kwa mtu yeyote ambaye anafanya kitu asichokuwa na uelewa au na uzoefu nacho. Mfano wewe tukupe treni uendeshe na hauna utalaam nayo lazima ukose kujiamini. Sasa sioni ajabu sababu kingereza ni lugha tu kama ilivyo kirusi au kichina ni ninyi wakenya ndio malimbukeni kwa sababu vichwa vyenu bado vimekaliwa na Uingereza.
 
Hii inatokea kwa mtu yeyote ambaye anafanya kitu asichokuwa na uelewa au na uzoefu nacho. Mfano wewe tukupe treni uendeshe na hauna utalaam nayo lazima ukose kujiamini. Sasa sioni ajabu sababu kingereza ni lugha tu kama ilivyo kirusi au kichina ni ninyi wakenya ndio malimbukeni kwa sababu vichwa vyenu bado vimekaliwa na uingereza

Lugha yoyote usipojenga uzoefu unakua kama zezeta tu, binafsi kuna kipindi nilijifunza Kifaransa ila kwa kuwa sikukitumia yaani leo hii hata kuomba maji kwa Kifaransa sijui unaanza vipi.

Sasa nyie hapo mnashtukizwa kwa Kingereza mkianza shule ya upili, halafu baada ya hapo mnaingia mtaani unakuta hakuna anayejua kukitumia labda watoto wa matajiri. Unaishia kukisahau kisha baadaye unakuta vitu vingi ikiwemo sheria na mikataba imeandikwa kwa Kingereza, yaani mkataba wa kampuni ya madini umeandikwa kurasa 800 kwa kingereza huku ukiwaza wewe ni mtu wa ze ze ze unaomba uonyeshwe wapi pa kutia saini tu, na hapo ndio mnajikuta mkiliwa sana, nchi inakua na madini kuliko mataifa yote Afrika lakini ukata umetamalaki kote.
 
Kuna uzi nimekutana nawo humu unaongelea kuhusu shule za serikali ambazo ni English medium, nikawa nachanganyikiwa, maana Watz haswa walalahoi wote huwa wameaminishwa Kingereza ni cha mkoloni mara sijui ni cha malkia, hivyo watoto wao wapelekwe kusomea kwenye shule za st Kayumba, ilhali wenye hela zao na hata viongozi wapeleke watoto wao kwa shule binafsi za English medium, ila kumbe kunazo pia za serikali na zinazotumia mtaala mmoja japo zina ada ya gharama.

Ndugu zetu hiki kingereza mtakizunguka na kukitukana na kujifanya kukichukia ila hakikwepeki kwenye utandawazi wa leo, mambo ya "sizitaki mbichi" yamepitwa na wakati.... suluhisho ni kucaha uzembe na kukisomea

Shule za English medium za serikali | JamiiForums

Kuna huu uzi mwingine ambao naona jamaa ameandia kwa uchungu sana kuhusu hilo hilo JAMHURI YA WOGA! | JamiiForums
Tanzania haijawahi kudharau kiingereza, ni awamu hii tu ndo kumezuka hili jambo na hata sisi tunaona aibu usione tunajikakamua kubisha. Awamu tuna sababu ya msingi ya kukiponda kiingereza, hakuna nyumba inapika kitimoto wakati baba mwenye nyumba hatumii kisa kuna watoto wanatamani Kitimoto.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom