Nimerejea kutazama 'Video' mbalimbali za Hayati Rais Dkt. Magufuli niseme tu Samahani kwa 'Kumkosoa' ila Asante Mungu kwa 'Kutuzawadia' Rais kama yeye

Kwangu mimi JPM JPM alikuwa rais muuaji, mwenye chuki kali sana kwa wanamkosoa na kumpinga, mbinafsi aliyepitiliza kiwango cha kawaida na mungu mtu aliyependa kusujudiwa mpaka na nzi. MUNGU AMEWATENDEA HAKI WATANZANIA.
Hivi mungu anaipendea nini hii ccm ameiacha hadi leo?
 
Pimeni mambo vizuri. Ukisema magu ni mbaya lazima kuna utayesema ni mzuri. Na ukisema magu ni mzuri kuna unayemini ni mbaya.
Uzuri ni nini na ubaya ni nini?
Ukija na orodha ya mambo mazuri, mwingine ataorodhesha mabaya.
Msifike mahali kusema mtu ni malaika, hii kufuru.
Binadamu hawezi kuwa mzuri tu au mbaya tu kwa watu wote wakati wote.

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
Naunga mkono 100%
 
Kuna mambo tukiyatazama tunaju akabisa kweli watanzania hatujui tunataka nini, hatujui tunamtaka nani, aje kufanya nini, na kwanini, yani tuna macho lakini yanasiki, tunamasiki lakini yanaona, tuna mdomo lakini unanusa na tuna pua ambyo ndio inayokula, alotuloga bila shaka alikufa na ukimwi kama siyo kimeta.
 
Na bado hujalia siku ukipata mtu wa karibu nae akakusimilia kifo chake, utaenda chato mwenyewe kuona hata kaburi yake.

Siumii kwa nini amekufa maana kila mtu ataonja kaburi, kinachoniuma ni yale mazingira alokufa.
Umenitoa machozi Mkuu.
Mungu atakuja laani kizazi chetu.
 
Kweli ni mkombozi hasa maana mpaka dunia itaisha hatutosikia tena mtu kupigwa risasi 36 na kunyimwa matibabu na kufukuzwa ubunge huyu ndie aliye kua mkombozi wa nchi ambae hapeleki maendeleo kwenye jimbo la wapinzani
Unafikiri Dr Ulimboka ataona alichofanyiwa na Kikwete ni kidogo sana ukilinganisha na Lissu?
 
Kumpenda mtu siyo lqza awe mtu mzuri au awe alifanya mazuri, bali ni namna matwkwa yako yanavyokutuma.

Lakini nina uhakika mtu kama Tundu Lisu, ndugu na jamaa wa Ben Sanane, Azory, Kanguye, na wale waliobambikiwa kesi za uhujumu uchumi, madawa ya kulevya, utakatishaji fedha, na wale wote wanaothamini uhai na maisha ya binadamu, hawataacha kumkumbuka marehemu kama mtu mbaya kuliko wote maana hakuna aliyewahi kuwafanyia uovu kama huo katika maisha yao yote.

Binadamu tunatofautiana, wapo wakipewa nafasi wajengewe nyumba ila ndugu yao auawe, watakubali. Lakini wapo watakaosema aheri waishi kwenye kibanda kuliko ndugu yao kufa. Kwao uhai na heshima ya mwanadamu inazidi vitu vyote.
Ni kweli kabisa mtu kama Kikwete anaweza kuwa ni mtu mzuri sana kwa upinzani ila kwa Dr Ulimboka hali inaweza kuwa tofauti kabisa.
 
Hayati Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Asante kwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Kipindi chako chote na leo GENTAMYCINE bila Unafiki nasema Tanzania tarehe 17 March, 2021 tumempoteza "Malaika Maalum' aliyeletwa na Mwenyezi Mungu kuja Kutuamsha Watanzania, Kututhaminisha, Kutuheshimisha, Kutuaminisha na kutuletea Maendeleo ya haraka.

Kutoka Mwezi March 2021 hadi leo hii (Mwezi Oktoba 2021) nimeanza Kuiona Tanzania ya tofauti kabisa ambayo imeanza kurudi nyuma na 'Kusuasua' katika Sekta nyingi na Maeneo mengi hali ambayo imeanza Kunitisha huku Machozi ya Kumbukumbu ya Kuondokewa nae Hayati Rais Dkt. Magufuli yakianza 'Kunibubujika' tena.

Nisamehe Hayati Rais Dkt. Magufuli kwa Kukukosoa Kimihemko, nakukumbuka, nakulilia sana na namuomba Mwenyezi Mungu ailaze Roho yako mahala pema Peponi ila huko Chato ulikolala sasa jua kuwa Viatu vyako bado ni Vikubwa na Vinawapwaya wale waliodhani kuwa aina ya Uongozi wako ulikuwa ni rahisi wakisahau kuwa Umahiri wako wa Kiuongozi uliongozwa ma kutawaliwa zaidi na Kumtanguliza Kwako Mwenyezi Mungu na Malaika wake.

Ninatamani 2025 aje tu Magufuli mpya.
Ndugu Gentamycine antibiotiqe popoma wa mapopoma.kwa thread hii ya leo.
Nakupa salute ya heshima ya juu zaidi.
Tulikuwa tunamwelewa JPM Na tutaendelea kuielewa Hadi mifupa yake ni wale pekee tulio naIQ kubwa tu.
Wazalendo na wafia nchi Kama Mimi.
Salute to the true son of Africa,the Great JPM
 
Tangu mwaka uanze nahisi huu ni uzi wako wa maana kuliko zote.

Anyway binafsi jpm nillikuwa namkubali kawaida tu hasa nikiwa sehemu ya changanyikeni kama humu, nilikuwa simchukii kama wengine, kuna vitu alikuwa akifanya nasema huyu kweli rais hata kama sisem ila moyoni nasema hili jembe.

Siku niliposikia habari za kifo chake trh 9 nilisikia maumivu ambayo sikujua yametoka wapi.

Miliogopa hata kumwambia mtu yeyote maana alienihakikishia kafa alinitaka nifunge mdomo wangu.
Nilikuwa nikiingia humu nakuta watu wanachangia nyuzi kibao eti jpm yupo wapi na mimi najilazimisha kuchangia as if sijui kinachoendekea.
Pili moyo haukuamini nilichoambiwa nikawa akisemea ' huyu mbwa nae mwongo jpm atakufaje kizembe hivi?

Siku moja nikataka kumwambia mama yangu moyo ukasema hapana yupo hai yule fala mzushi.
Trh 17 usiku nikaota eti kafa nikastuka usingizini nikajisemea hapana ni nawazo yaliyo kichwani mwangu coz nishapewa hiyo habari wiki moja kabla.
Niliamka nikapiga magoti nikasali mikasema hii ndoto isiwe kweli, nikaingia jf nikakuta mtu kapost eti kwa nini wasitangaze tu rais kashakufa kha! Ndo niliamini yale maneno.

Baada ya kutangaza nilipata maumivu ambayo sikujua yametoka wapi, maana niliona Tanzania ambayo jpm alikuwa akiitengeneza ikiyeyuka.

Niliona ujinga ukirudi kwa kasi, wizi, miradi yake ikifa, nidham ya watumishi ikirudi 0, ufisadi nje nje , majambazi wakirudi kwa kazi, unyanyasaji wa wanyonge, viongozi kula mishahara ya bure,kupewa kazi kwa kujuana, vyeti feki,
Nikaona lile genge sugu la majambazi wanaotesa nchi wakifurahia kifo chake, nililia sana nikasema Mungu alitupa malaika ila wengi tulichukulia poa.
Huko ulipo jpm ulale salama, hakuna siku imepita bila kukukumbuka. Binafsi nimekumiss sana.

Rip jpm.
Katika mawaziri wake wote,namuona Hussein Mwinyi anafanya kazi kule Zanzibar kama Magufuli.Zanzibar ukizingua tu,anakula kichwa.Hussein arudi bara 2025,huyu Mama hapana.
 
Hayati Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Asante kwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Kipindi chako chote na leo GENTAMYCINE bila Unafiki nasema Tanzania tarehe 17 March, 2021 tumempoteza "Malaika Maalum' aliyeletwa na Mwenyezi Mungu kuja Kutuamsha Watanzania, Kututhaminisha, Kutuheshimisha, Kutuaminisha na kutuletea Maendeleo ya haraka.

Kutoka Mwezi March 2021 hadi leo hii (Mwezi Oktoba 2021) nimeanza Kuiona Tanzania ya tofauti kabisa ambayo imeanza kurudi nyuma na 'Kusuasua' katika Sekta nyingi na Maeneo mengi hali ambayo imeanza Kunitisha huku Machozi ya Kumbukumbu ya Kuondokewa nae Hayati Rais Dkt. Magufuli yakianza 'Kunibubujika' tena.

Nisamehe Hayati Rais Dkt. Magufuli kwa Kukukosoa Kimihemko, nakukumbuka, nakulilia sana na namuomba Mwenyezi Mungu ailaze Roho yako mahala pema Peponi ila huko Chato ulikolala sasa jua kuwa Viatu vyako bado ni Vikubwa na Vinawapwaya wale waliodhani kuwa aina ya Uongozi wako ulikuwa ni rahisi wakisahau kuwa Umahiri wako wa Kiuongozi uliongozwa ma kutawaliwa zaidi na Kumtanguliza Kwako Mwenyezi Mungu na Malaika wake.

Ninatamani 2025 aje tu Magufuli mpya.
Wapenda maendeleo ya kweli na sio porojo tunaelewa magufuli alikuwa anafanya nini ,wengi tuliamini wacha tuumie kwa muda huu mchache lakini kesho vizazi vijavyo vingeneemeka r.i.p magufuli.
 
Back
Top Bottom