Nimerejea kutazama 'Video' mbalimbali za Hayati Rais Dkt. Magufuli niseme tu Samahani kwa 'Kumkosoa' ila Asante Mungu kwa 'Kutuzawadia' Rais kama yeye

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,516
108,791
Hayati Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Asante kwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Kipindi chako chote na leo GENTAMYCINE bila Unafiki nasema Tanzania tarehe 17 March, 2021 tumempoteza "Malaika Maalum' aliyeletwa na Mwenyezi Mungu kuja Kutuamsha Watanzania, Kututhaminisha, Kutuheshimisha, Kutuaminisha na kutuletea Maendeleo ya haraka.

Kutoka Mwezi March 2021 hadi leo hii (Mwezi Oktoba 2021) nimeanza Kuiona Tanzania ya tofauti kabisa ambayo imeanza kurudi nyuma na 'Kusuasua' katika Sekta nyingi na Maeneo mengi hali ambayo imeanza Kunitisha huku Machozi ya Kumbukumbu ya Kuondokewa nae Hayati Rais Dkt. Magufuli yakianza 'Kunibubujika' tena.

Nisamehe Hayati Rais Dkt. Magufuli kwa Kukukosoa Kimihemko, nakukumbuka, nakulilia sana na namuomba Mwenyezi Mungu ailaze Roho yako mahala pema Peponi ila huko Chato ulikolala sasa jua kuwa Viatu vyako bado ni Vikubwa na Vinawapwaya wale waliodhani kuwa aina ya Uongozi wako ulikuwa ni rahisi wakisahau kuwa Umahiri wako wa Kiuongozi uliongozwa ma kutawaliwa zaidi na Kumtanguliza Kwako Mwenyezi Mungu na Malaika wake.

Ninatamani 2025 aje tu Magufuli mpya.
 
Kwani nini kimetokea jamani???si tulifunga mjadala humu kwamba alikuwa dikiteta!¡!!
Imekuwaje tena
JamiiForums-1171789414.jpg
 
Back
Top Bottom