Nimerejea kutazama 'Video' mbalimbali za Hayati Rais Dkt. Magufuli niseme tu Samahani kwa 'Kumkosoa' ila Asante Mungu kwa 'Kutuzawadia' Rais kama yeye

Afrika jinsi ilivyo na Watu ( Raia ) walio 'Goi Goi' inahitaji akina Hitler kama 60 tu ili Kuiamsha na Kuichangamsha Kimaendeleo na Kiuchapakazi.
Mbona wewe usiwe Hitler wa familia yako Ili mpate maendeleo? It will never happen again,and he used to be there as political mistake thus why his term ended in that way.

Kama kawaida unathibitisha how panthetic you are.
 
Aisee haitakaa itokee ,wewe na mtoa mada licha ya kujiandikia maelezo meeengi ya kijinga hamna ushahidi wowote wa kuthibitisha maelezo yenu mwisho wa siku inakuwa ni chuki ya kukosa uteuzi basi.
Yaani GENTAMYCINE ninataka Uteuzi?
 
Nilikuwa ninakuheshimu kumbe ni bure.

Nitasema kweli daima fitina kwangu ni mwiko....Ahadi za mwana TANU.

Siwezi kupindisha maneno kwa kumfurahisha mtu,Jiwe aliendesha nchi kwa mkono wa chuma,kila binadamu ana mazuri na mabaya yake ,bashite,jambazi sabaya,wewe mtaangalia mazuri tu ila Lissu alichapwa risasi 38 au Familia ya ben saa8 hawawezi kuangalia mazuri.
 
Mkuu kuhusu Kifo chake kimetokana na nini wala usijali kwani huenda nami kwa niliyoambiwa na Mchongo mzima ulivyokuwa hadi Kufa Kwake nimeanza kuuamini ule Msemo usemao KIKULACHO KI NGUONI MWAKO na nina Watu Watatu katika hiyo 'List' huwa nikiwaona tu katika Tv ( Runinga ) huwa nazima kwa Hasira na kubaki Kuwasonya na Kuwatukana tu Kimoyomoyo na Kufuta Machozi ya kutuwahishia Udongoni Chato Mkoani Geita huyu Mwamba wetu.
Hutakiwi kuzima kwa maigizo Zima mazima Ili utuondolee uchuro kama mkuu wa uchuro alivyoshindiliwa chini ya vifusi..
 
Mkuu kuhusu Kifo chake kimetokana na nini wala usijali kwani huenda nami kwa niliyoambiwa na Mchongo mzima ulivyokuwa hadi Kufa Kwake nimeanza kuuamini ule Msemo usemao KIKULACHO KI NGUONI MWAKO na nina Watu Watatu katika hiyo 'List' huwa nikiwaona tu katika Tv ( Runinga ) huwa nazima kwa Hasira na kubaki Kuwasonya na Kuwatukana tu Kimoyomoyo na Kufuta Machozi ya kutuwahishia Udongoni Chato Mkoani Geita huyu Mwamba wetu.
Wewe acha tu nakumbuka mwalimu wangu aliwahi kuniambia kuwa mtu akitenda ubaya sura yake uwa inaongea. Siku ya mazishi ya JPM nimwona mmoja wao akijikanyaga na hotuba uchwala anauma midomo nikamwangalia nikajisemea kimoyoni kwamba " huyu "
 
Wewe acha tu nakumbuka mwalimu wangu aliwahi kuniambia kuwa mtu akitenda ubaya sura yake uwa inaongea. Siku ya mazishi ya JPM nimwona mmoja wao akijikanyaga na hotuba uchwala anauma midomo nikamwangalia nikajisemea kimoyoni kwamba " huyu "
Utaishia kujisemea kimoyo moyo hivyo hivyo hadi tunafukia
 
Tangu mwaka uanze nahisi huu ni uzi wako wa maana kuliko zote.

Anyway binafsi jpm nillikuwa namkubali kawaida tu hasa nikiwa sehemu ya changanyikeni kama humu, nilikuwa simchukii kama wengine, kuna vitu alikuwa akifanya nasema huyu kweli rais hata kama sisem ila moyoni nasema hili jembe.

Siku niliposikia habari za kifo chake trh 9 nilisikia maumivu ambayo sikujua yametoka wapi.

Miliogopa hata kumwambia mtu yeyote maana alienihakikishia kafa alinitaka nifunge mdomo wangu.
Nilikuwa nikiingia humu nakuta watu wanachangia nyuzi kibao eti jpm yupo wapi na mimi najilazimisha kuchangia as if sijui kinachoendekea.
Pili moyo haukuamini nilichoambiwa nikawa akisemea ' huyu mbwa nae mwongo jpm atakufaje kizembe hivi?

Siku moja nikataka kumwambia mama yangu moyo ukasema hapana yupo hai yule fala mzushi.
Trh 17 usiku nikaota eti kafa nikastuka usingizini nikajisemea hapana ni nawazo yaliyo kichwani mwangu coz nishapewa hiyo habari wiki moja kabla.
Niliamka nikapiga magoti nikasali mikasema hii ndoto isiwe kweli, nikaingia jf nikakuta mtu kapost eti kwa nini wasitangaze tu rais kashakufa kha! Ndo niliamini yale maneno.

Baada ya kutangaza nilipata maumivu ambayo sikujua yametoka wapi, maana niliona Tanzania ambayo jpm alikuwa akiitengeneza ikiyeyuka.

Niliona ujinga ukirudi kwa kasi, wizi, miradi yake ikifa, nidham ya watumishi ikirudi 0, ufisadi nje nje , majambazi wakirudi kwa kazi, unyanyasaji wa wanyonge, viongozi kula mishahara ya bure,kupewa kazi kwa kujuana, vyeti feki,
Nikaona lile genge sugu la majambazi wanaotesa nchi wakifurahia kifo chake, nililia sana nikasema Mungu alitupa malaika ila wengi tulichukulia poa.
Huko ulipo jpm ulale salama, hakuna siku imepita bila kukukumbuka. Binafsi nimekumiss sana.

Rip jpm.
Sikuwahi kumpenda JPM, lakini honestly ilivyotangazwa usiku ule kuwakafariki machozi yalinitoka, nikakaa nje karibia saa nzima. Niliona kabisa yale magenge ya majambazi serikalini na chamani yayakavyorudi kwa nguvu.
 
GENTAMYCINE

2025 SSH 5tena
Mitano tena, Hii kauli imetugharimu kama chama

Watu walitukebehi sana hii kauli ya mitano tena, Kumbe kiroho ilikuwa kinyume chake kuwa hatamaliza mitano imeishia miezi kadhaa

Mitano tena, Ikawa miezi kadhaa na Kwaheri ya kuonana
 
Kama ulikuwa na tabia za wizi,utapeli na kuishi kwa ujanja ujanja mjini hakuna jema la Hayati JPM utakaloliona.
Pimeni mambo vizuri. Ukisema magu ni mbaya lazima kuna utayesema ni mzuri. Na ukisema magu ni mzuri kuna unayemini ni mbaya.
Uzuri ni nini na ubaya ni nini?
Ukija na orodha ya mambo mazuri, mwingine ataorodhesha mabaya.
Msifike mahali kusema mtu ni malaika, hii kufuru.
Binadamu hawezi kuwa mzuri tu au mbaya tu kwa watu wote wakati wote.

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Kama ilivyo kwa Binadamu yeyote yule hakosi "flaws" Basi ndivyo ilivyo kuwa kwa Jpm. R.i.p kwake.... Ila kwa sasa ndiyo gap kubwa zaidi tunaliona kutokana na uongozi wa sasa ni useless kabisa.
 
Kama ulikuwa na tabia za wizi,utapeli na kuishi kwa ujanja ujanja mjini hakuna jema la Hayati JPM utakaloliona.
Utakuwa upo mbali sana kutoka usawa wa nchi, mbona huku ndani sasa hata tuliokua tunajua kumbe ilikuwa wajinga wa kutupwa. (Nchi hii haijawahi kuwa na mwizi, tapeli, laghai, muongo, na katili wa mfano wake)
 
Back
Top Bottom