Thank you dada akipata kazi nitaleta mrejesho mdau
Kweli ndoa zina yake...
Kazi hapati na biashara hataki japo umetaka kumfungulia
Jaribu kumfungulia ofisi kuendana na fani yake kama unaweza..
Habarini wana jf wenzangu, Mwenzenu yamenikuta leo, ile narudi home toka job nimepokewa na kilio kutoka kwa mkewangu kuuliza kulikoni mama ananijibu amechoka na maisha ya kukaa nyumbani, labda nielze kwa kifupi ni kwamba mke wangu ni graduate ana degree ya leasure and hospitality toka makerere, kama miaka miwili iliopita alipata kazi kwenye moja ya tasisi za kibenki hapa nchini wakati huo tulikuwa tunaishi Arusha, sasa kwa bahati nzuri mi nilipata kazi nyingine ikabidi nihamie dar yeye kwa upande wake alikataliwa uhamisho wa kuja huku dar, ili kuiokoa ndoa yake ikabidi afanye maamuzi magumu ya kuacha kazi kwa kwa kutegemea tukishahamia hapa dar tutatafuta kazi nyingine tangia kipindi hiko hatujabahatika kupata kazi na juhudi zote tumezifanya ila bado hatujafanikiwa, na nilishatumaga uzi hapa atakaenisadia kumpatia mkewangu kazi nitampa asante ya milioni 1, nilimshahuri nimfungulie biashara akaniambia hawezi coz biashara ni wito, sasa leo ndo nimemkuta katika hali hiyo kwa kweli nimejiskia vbaya sana na hata kula hataki, naomba mnisaidie waungwana wenzangu nifanyeje kwa huyu mkewangu manake kama juhudi zote nimetumia huu mwaka wa 3 cjafanikiwa. Nakaribisha mawazo yenu wadau.
Huyu Mama yoyoo anaona soko la ajira kwa sasa lilivyokuwa gumu mwambie baby wako asilie atulie ,mungu anatoa kwa wakati wake
Mwambie atafute kwa bidii iko siku atapata tu ,au unampa vimatumizi kidogo ukiweka na VAT anashindwa hata kununua Wax na kwenda Saloon?
Hapana mdau sema mi najitahidi tu kutimiza majukumu yangu ya kifamilia kama baba alaf we have 1 kid of 6yrs now.
Du. Ni kweli inachanganya unapokaa tu home bila kazi wakati unadhani unahaki ya kuajiriwa.
Nampa pole. Sie wanawake tukishashika hela baada ya muda tunaanza kusubiri pocket money ni utata mtupu.
Namuellewa.
Ila tafuta jinsi ya kumfahamisha kuwa depression au not ni hiari na attitude yake binafsi.
Asikuweke katikati. Ajipe jukumu la kuhakikisha kuwa furaha yake anajipanga mwenyewe.
Akiwa na raha na akiwa positive ndio furaha ya familia.
Ajipange. Kama hana life skills asome atafute marafiki ndugu vikundi semina ajitolee etc.asijifungie ndani.
Makosa wanayofanya wadogo zangu wengi ni kudhani kuwa na juhudi za kutosha chumbani kutampa satisfaction 100%. Maisha ya ndoa kwa mke ni much much more than the bed and kisses. Japo vina mchango mkubwa.
Future is always brighter unapoamua kufanyia kazi tatizo.
I hope na wewe una appreciate alivyojitoa kwa kVuacha kazi yake na kukufuata. Hakikisha anajua kuwa unathamini ile decision ya kisadaka alioifanya kwani siku hizi ni wachache wanakubali kuacha kazi zao kwa ajili ya ndoa na familia. Make sure anajua faida za ule uamuzi wake.
Ila asikae ndani. Msaidie kwa kumtoa aende akatumie akili yake.
that's good because you know ur responsibilities....but its not enough wat if mkeo nae angekua na kajikipato kokote tu si ingekua vizur jamani au unapenda mwanamke tegemezi.....???????
Hapana mdau sema mi najitahidi tu kutimiza majukumu yangu ya kifamilia kama baba alaf we have 1 kid of 6yrs now.
Habarini wana JF wenzangu.
Mwenzenu yamenikuta leo, ile narudi home toka job nimepokewa na kilio kutoka kwa mke wangu kuuliza kulikoni mama ananijibu amechoka na maisha ya kukaa nyumbani, labda nieleze kwa kifupi ni kwamba mke wangu ni graduate ana degree ya leasure and hospitality toka makerere.
Kama miaka miwili iliyopita alipata kazi kwenye moja ya taasisi za kibenki hapa nchini wakati huo tulikuwa tunaishi Arusha, sasa kwa bahati nzuri mimi nilipata kazi nyingine ikabidi nihamie Dar yeye kwa upande wake alikataliwa uhamisho wa kuja huku Dar.
Ili kuiokoa ndoa yake ikabidi afanye maamuzi magumu ya kuacha kazi kwa kutegemea tukishahamia hapa Dar tutatafuta kazi nyingine tangia kipindi hiko hatujabahatika kupata kazi na juhudi zote tumezifanya ila bado hatujafanikiwa, na nilishatumaga uzi hapa atakaenisadia kumpatia mke wangu kazi nitampa asante ya milioni 1.
Nilimshahuri nimfungulie biashara akaniambia hawezi coz biashara ni wito, sasa leo ndo nimemkuta katika hali hiyo kwa kweli nimejiskia vibaya sana na hata kula hataki, naomba mnisaidie waungwana wenzangu nifanyeje kwa huyu mke wangu maanake kama juhudi zote nimetumia huu mwaka wa 3 sijafanikiwa.
Nakaribisha mawazo yenu wadau.
Hapana dada najitahidi kumtafutia kazi ila sifanikiwi ingawa chuo alifanya vzr sema bado riziki haijafunguka na ofcoz wakati niko kazini nilikuwa naenjoy sana coz na yy hana roho mbaya huwa tunashirijishana sana i wish apate hata leo kazi aisee