Mwl Mwakujonga
JF-Expert Member
- Jun 29, 2023
- 368
- 735
Miaka kadhaa mara baada ya kuangaika hapa na pale kutaguta ajira nikafanikiwa kuajiriwa ofisi moja ya umma
Kwangu lilikuwa jambo la heri sana kupata kazi, na kwa wazazi wangu walifurahi sana kijana wao kupata kazi.
Mara baada ya taaribu za ajira nilipangiwa kituo cha kazi mkoa jirani na nilipozaliwa
Nilimshukuru Mungu kwa kupata kazi na kituo changu kuwa karibu na wazazi wangu nikawa nina uwezo kila wiki kuwatembelea wazazi wangu
Furaha yangu haikudumu kwa muda mrefu kwani kiongozi ambaye alikuwa ndiye bosi wangu akitokea kutonikubari kabsa
Kitendo cha kukataliwa na bosi kilinisikitisha sana, kwanza ilikuwa ni kazi yangu ya kwanza ya umma lakini pili nilikuwa najua kwamba kazi za umma zinaulinzi sio rahisi kufukuzwa kazi nk
Kabla ya hapo nilifanikiwa kufanya kazi kwenye sekta binafsi , kwa kweli bosi wangu hakuwa na mambo ya kuwachukua watumishi. Yeye kama haufanyi vizuri anakutimua tu hakuwa na muda wa kupoteza na watumishi
Pamoja na ajira yangu hii kuwa ya kwanza lakini pia kazi ambazo nilitakiwa kuzifanya zilitakiwa nijifunze kwa sababu kila ofisi inautaratibu wake wa kufanya kazi
Mungu sio athumani msaidizi wa bosi wangu alitokea tu kunipenda na kunijali na kwa kuwa yeye ndiye alikuwa anawapangia watumishi wapya majukumu alinipagia majukumu yangu ambayo yalikuwa yapo chini ya kinogozi au msimamizi
Kazi haikuwa raisi kwa sababu licha ya jitihada zangu za kufanya kazi kwa bidii lakini matokeo kwa bosi wangu yalikuwa ni zero, hakuna kitu alichokikubali.
Kuna wakati nilifikiri kuacha kazi lakini nikawaza kwanza nikiacha kazi wazazi wangu wanaonitegemea itakuaje na sikuwa na kazi, je nikiacha kazi na familia yangu itakuwaje ndio kipindi hicho nilikuwa nimeoa tayari mke wangu itakuwaje nitawezaje kumtunza?
Miaka yangu 5 niliyofanya kazi chini ya huyo kiongozi haikuwa raisi kuna kipindi alikuwa anasema waziwazi hajui kwanini ofisi imeniajiri.
Kwa kweli nilivunjika moyo lakini sikuwai kumwambia mtu zaidi ha kukaa na Mungu wangu maana nilijua wazazi wangu wanayo ya kwao na nikiwashirikisha nitawaumiza kuliko navyoumia mimi.
Siku mmoja alikuja kiongozi kutoka makao makuu ya ofisi bahati nzuri yule kiongozi alikuwa muungwana sana akanialeza amepokea maelekezo kuja kikagua kazi yangu
Mimi sikuwa na shida kwa sababu siku zote nilikuwa nafanya kazi kwa weredi na uadilifu kitu ambacho nilimwaomba Mungu siku zote kaI zangu ziwe za weredi na uadilifu mkubwa
Ukaguzi ukifanyika na baada ya ukaguzi yule kuongozi alitoa mapendekezo mazuri sana kwangu akanisifia sana kwa kiongozi wangu
Jambo ilo halikuwa jema kwa kiongozi wangu, akawa anatafuta sababu kazi ambayo ilikuwa naweza kufanya alikuwa anaomba wataalamu kutoka ofisi kuu ili tu ofisi kuu wajue kule hakuna mtu mwenye weredi
Ni jambo ambalo lilikuwa likiniumiza sana lakini sikuwa na jinsi , walikuwa wanakuja nawapa ushirikiano wanakawa wanshangaa wakirudi ofisi kuu kutoa taarifa juu yangu zilikuwa taarifa nzuri.
Miaka ilienda, Mungu akawapamoja nami hadi siku moja wafanyakazi wenzangu wakaamua kuingilia kati na kumwambia ukweli bosi wangu juu yangu anachonifanyia kwa kweli alikiri nakuniomba msamaha na maisha yakaendelea
Haikuwa rahisi lakini namshukuru Mungu nilifanikiwa kuvuka, nikikumbuka kile kipindi
Kitu ambacho namshukuru Mungu pamoja na mambo yote hayo, nilijifunza kuwa mnayenyekevu sio kwamba nilikuwa mnyonge hapana
Nakumbuka kabla sijapata kazi ya umma kunasiku tulipishana mawazo na bosi wangu niliamua kandika barua ya kuacha kazi na kama asingekuwa mzee mmoja ambaye ndiye alikuwa msimamizi wangu labda ningekuwa niko nyumbani sasa sijui ningekuwa nafanya nini?,
Unapokutana na changaomoto ya kukataliwa usifane maamuzi ya haraka kama kuacha kazi, usiache kazi kwa sababu huna hasira au umekatiliwa hacha kazi kwa sababu umeona fursa nyingine umepata sio kukurupuka kuacha kazi ni hatari kwako na kwa familia yako.
Kutoa majibu ukiwa na hasira, nakumbuka siku moja bosi wangu alinikasirikia sana akanitamkia tusi languoni kwa kweli jambo hilo lilikuwa la wawili lakini nililipeleka kwa wenzangu lilimfanya bosi kuomba msamaha kwa sababu ni kinyumr cha kanuni za utumishi kumtukana mtumishi mwenzako
Kumjibu kiongozi vibaya , kutokana na changamto za maisha na kupata kazi , siku moja nilikuwa ninawaza hau ni mfate tu huyu bosi mtukane kwelie kweli kisha niache kazi? Lakini rohoni nikaona hayo sio mawazo ya Mungu ni kweli alikuwa anikwaza na alikuwa ananikwaza mbele za watu
Nilikuja kujua kwanini alikuwa ananikwaza mbele za watu, kwamba nihamaki ili niweze kujibu na mashahidi wapo ili nifukuzwe kazi nilipojua hiyo mbinu nilikubali matokeo nikamwomba Mungu anipe unyenyekevu nashukuru Mungu nilivuka
Nakumbuka mara baada ya mambo ayo ndipo milango ya kazi ikafunguka nikawa namuuliza Mungu miaka hii 5 nimepata kila aina ya shida sasa mambi yamekuwa mazuri kazi zingine zinakuja?
Kumbe sio kila kazi ni za kufanya kwa sababu kuna kusudi la Mungu katika kazi unayofanya
Unapokutana katika changamoto jiulize swali
Je hiyo kazi ni sahiho kwako, kama una uhakika uko eneo sahihi usiondoke tulia vumilia
Ukiona unapigwa vita ujue hupo sehemu sahihi usichoke