Habarini wana JF wenzangu.
Mwenzenu yamenikuta leo, ile narudi home toka job nimepokewa na kilio kutoka kwa mke wangu kuuliza kulikoni mama ananijibu amechoka na maisha ya kukaa nyumbani, labda nieleze kwa kifupi ni kwamba mke wangu ni graduate ana degree ya leasure and hospitality toka makerere.
Kama miaka miwili iliyopita alipata kazi kwenye moja ya taasisi za kibenki hapa nchini wakati huo tulikuwa tunaishi Arusha, sasa kwa bahati nzuri mimi nilipata kazi nyingine ikabidi nihamie Dar yeye kwa upande wake alikataliwa uhamisho wa kuja huku Dar.
Ili kuiokoa ndoa yake ikabidi afanye maamuzi magumu ya kuacha kazi kwa kutegemea tukishahamia hapa Dar tutatafuta kazi nyingine tangia kipindi hiko hatujabahatika kupata kazi na juhudi zote tumezifanya ila bado hatujafanikiwa, na nilishatumaga uzi hapa atakaenisadia kumpatia mke wangu kazi nitampa asante ya milioni 1.
Nilimshahuri nimfungulie biashara akaniambia hawezi coz biashara ni wito, sasa leo ndo nimemkuta katika hali hiyo kwa kweli nimejiskia vibaya sana na hata kula hataki, naomba mnisaidie waungwana wenzangu nifanyeje kwa huyu mke wangu maanake kama juhudi zote nimetumia huu mwaka wa 3 sijafanikiwa.
Nakaribisha mawazo yenu wadau.
Hakuna kitu kibaya ktk hii dunia kama kuacha kazi mwenyewe, hapo ndipo alipoandikiwa na Muumba halafu akaiacha msoto wake ni wa ajabu, sina hamu, mpe moyo atapata kazi ila ndio iwe fundisho yaani ni bora uachishwe utapata nyingine haraka. Laah najua maumivu yake mpe pole
Akaombewe kwa Gwajima atapata tu ufahamu hutamuona akikulilia hovyo.