hivi kama ni lazima kutukana hakuna tusi lingine zaidi sehemu nyeti hasa za jinsi ya ke? huyo mkeo anahitaji kufunguliwa akili tu. Si kweli kuwa hawezi biashara ila ni vizuri kumvumilia maana wengi wetu tuna woga. Siku atakaposema anaweza, atajifunza na kitaeleweka. Mtafutie cd na vitabu vya motivation (sijui kama atapenda kusoma au kusikiliza), aende kwenye semina au kozi fupi za ujasiriamali kama pale udec-udsm. Lakini nakubali kuna watu wanaweza kufanya vizuri zaidi wakiajiriwa kuliko kujiajiri.
Kwa kuwa ameng'ang'ania sana kuajiriwa basi muelewe mpeleke kwa hii taasisi ia IMED iko Ilala jengo la walimu (
Welcome to IMED Official Website) wana program inaitwa BRIDGE watamtafutia sehemu ya kufanya kazi kama intern na watamsaidia kujitambua zaidi na labda itamrahisishia kupata kazi. Inawezekana taaluma anayo ila hana vigezo vinavyokidhi ushindani kwenye soko la ajira. Nawashauri na vijana wengine wanaohangaika kuajiriwa au kujiajiri muende.