Nimepigwa zongo wakati nikila chakula

Nimepigwa zongo wakati nikila chakula

...Unajuaje kuwa umepiga Zongo? Dalili za kuwa umepiga Zongo ni zipi, tofauti na hali ya kawaida ya mwili wako???
 
Samahani mkuu,na matabano ndio nini

Sent using Jamii Forums mobile app

Matabano ni kiswahili cha neno ruqyah yaani ni tiba ya mambo ya kijicho na sihri/uchawi itokanayo na aya za qurani na dua kutoka kwa nabii, sasa kwa sisi waislamu tunazo dua/adhkaar mbalimbali ambazo mtu ukifika katika mji ukazisema hizo hakuna mchawi au hasidi anaweza kukugusa..
 
Nilihisi utakuwa Arusha wana huo mchezo balaa,nliteseka sana kipindi cha nyuma nkaenda kupewa dawa na baba mmoja hivi wa Kiarusha,ndo nkapona
Arusha nako kuna mambo ya kisenge sana sometime!!!
 
Huu uzi unahusu watu wenye elimu ndogo kuanzia std 7 tena ambao wanaishi uswahilini
Ila wewe uliyesoma ST FRANSIACO UK na ukija likizo unafikia kwa wazazi wako Masaki huwezi kuelewa kitu
Kwamba elimu yake ndiyo itakayoagua zongo au? Usichokijua haimaanishi hakipo.
 
Nakumbuka Mpanda Katavi bibi alikuaga anakata bomba la mpapai anatuwekea kwenye njia ya haja kubwa.
Then anajaza dawa mdomoni anapulizia kwenye hilo bomba.
Maumivu yake, nilikua nalia sana.
Lakini baada ya hapo napona kabisa.
😂😂😂😂😂
 
mkuu sina hamu na wasambaa hawa wa lushoto walinipiga Zongo La Wiki Bila Mimi Kufahamu, Nkaokolewa Na Mwenyeji Wa Huku Kuwa Nimepigwa Zongo,
Wakati Ndo Mara Ya Kwanza Kulisikia Neno "ZONGO"
Jamani wasambaa wa Lushoto wana zongo hatari! Nilienda kwenye msiba huko Lushoto mfanyakazi mwenzangu alifiwa na mzazi wake nilipigwa zongo hilo matata nilikosa choo siku nne tumbo likajaa gesi baada ya hapo niliharisha sana
 
Ninahitaji msaada wa kitaalamu juu ya hili tatizo kwani linanisumbua sana na pia linaweza kumpata mtu bila kujua kwani huwa katika mazingira usiyoweza kuyaona kwa macho.

Hivyo kwa mtu yeyote anayefaamu kautaalamu kakutegua afanye kweli kuokoa jahazi. Siku hizi kila kona ni mawindoni

Sent using Jamii Forums mobile app
Kupigwa Zongo maana yake ni nini?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom