Maisha ya kila mwanadamu yana historia nzuri na mbaya; kuna historia mbaya zinawe kubadili maisha na kuwa mazuri na kuna historia nzuri zinaweza kubadili maisha na kuwa mabaya.
Mwanamke kuwa changuduo haimaanishi kwamba anapoteza haki ya kupenda au kupendwa, kuolewa na nyinginezo; muhimu kufahamu kwanini amekuwa changudoa, sikiliza simulizi za maisha ya watu na utagundua kuna wakati kuna jambo lilikwenda hovyo na kumfanya mtu kuanguakia katika aina ya maisha ambayo hakutarajia, lakini akitokea mkombozi katika maisha yake na kumsaidia kumuongoza katika njia au kumtoa katika giza nene anaweza kurudi katika ufahamu wake.
Mke wangu alikuwa changudoa na nilikutana nae CLUB; kuna wakati nilikuwa na mwanamke ambaye nilimpenda na nilitarajia kuishi nae, lakini katikati ya mahusiano yetu akanizingua na nikaamua kuachana nae, NILIUMIA SANA na kupelekea kwenda club karibuni kila siku. Nikiwa club sikuwa nashuhulika na wanawake zaidi ya kunywa na kucheza music nilikuwa na-enjoy kwa hayo, vile vile nilikuwa sipendi kuchukua changudoa kwa sababu ya tabia yao kwamba hutaweza ku-enjoy sex kwa sababu wanakuwa hawako kimapenzi zaidi na siyo rahisi kumletea hisia za mapenzi labda awe ameamua kwa siku hiyo.
Nikiwa club mara kwa mara nilikuwa nikimuona dada huyu ambaye alikuwa changudoa, lakini akifanya biashara hii kwa ustarabu sana na mara nyingi alikuwa anasimama tu pembeni huku akipata kinywaji na kucheza kwa taratibu, kutokana na uzuri wake wanaume wengi walikuwa wanajipendekeza wenyewe kumfuata. Nilianza kusimama pembeni yake mara kwa mara na kumnunulia kinywaji, anapopata mteja huniaga na kuondoka. Siku moja tulipokutana club kama kawaida, aliniambia leo nina furaha na nitakununulia wewe kinywaji na tutaondoka wote. Kwa kweli siku hiyo alihakikisha kila ninapokwenda yupo pembeni kwamba sitaweza kumtoroka na hatimae alinichukua na kwenda kulala kwake, sikutaka kumpeleka kwangu kwani sikutaka afahamu ninapoishi. Kwa kweli alionyesha ushirikiano mkubwa katika mchezo, tofauti na nilivyokuwa nawafahamu machangudoa. Baada ya hapo sikuwa na mpango nae na niliacha kwenda club kwa siku mbili, siku ya tatu alinipigia simu na kuniomba tukutane club kama kawaida, baada ya hapo tuliendelea kuwa wapenzi lakini akiwa bado anauza; kwa kweli nilijitahidi kutokuonyesha kwamba sipendi yeye kujiuza, nilikuwa nakwenda naye club na akipata mteja namwacha anakwenda nae. Vile vile muhimu kufahamu kwamba machangudoa wengi hawako kwa biashara ya kuuza mwili sana, bali wanatafuta wateja ambao wanfikiri wanazo ili mwisho wa siku waweze kuwaliza na hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa huyu, alikuwa akiondoka na mteja club, tunapokutana siku ya pili ananiambia kiwango gani amepiga kutoka kwa huyo ***** na tutafurahia ushindi. Taratibu nilikuwa naongea nae kwa lengo la kumtoa huko aliko na hatimae baada ya takribani miezi miwili nilifanikiwa, kwani alitokea kunipenda sana na hatimaye akaanza kujisikia vibaya kunisaliti. Tulianza kuwa na uhusiano wa karibu sana na hatimae tulianza kuishi pamoja hadi yeye kuamua kuhamia kwangu. Mpaka leo sasa ni mke wangu; tunapendana na kushirikiana katika maisha na tumebarikiwa watoto wazuri. Tunasali katika makanisa ya ki-pentecost na imetusaidia sana kujenga maisha yetu ya kiroho.
Tusiwadharau wanadamu wenzetu tunapowakuta katika mazingira ambayo wewe kwa mtazamo wako unaweza kuyaona hayafai; nimejifunza kuwaheshimu watu wote kwa huwezi kufahamu kwani yupo katika mazingira hayo kwa wakati huo, kila jambo lina sababu. Kuna wanaume wana tabia mbaya zaidi ya wanawake tunaowaona machangudoa, kuna wanawake sio machangudoa lakini ni zaidi ya machangudoa.