Habarini wakuu,
Wiki hii nimeoa single mom, mtoto wake ana miaka 2 tangu azae jamaa alikimbia na hajulikani alipo hadi sasa hakutoa hata mia kwenye malezi ya mtoto, alisaidiwa kulea mtoto na mama yake, mtoto kamuacha kwao na mimi sitaki kuishi na huyo mtoto wake na yeye ashalikubali hilo maana tangu uchumba wetu wa mwaka mmoja, nishamwambiaga sitokaa na mtoto wako.
Ananipenda sana tena ile sana sijawahi kupendwa kama hivi kwa huu umri wangu wa 29 years nimewaacha wengi sana nimeamua yeye kumuoa nimeona hatasumbua kwa chochote maana ni mpole na msikivu sana.
Nimekuja tu humu kuwapa hiyo taarifa na kuja kuona mnaniusia wosia gani, kwa hiyo karibuni kwa maoni ya jinsi ya kuishi nae, na vitu gani nijitahadhari navyo, ushauri wowote pia unaruhusiwa na chochote ulichonacho cha kuniambia hata kiwe kibaya sawa tu karibu sana.