Nimeoa single mama

Nimeoa single mama

Sio ndugu Kwa maana ya damu moja.
Ukishasema neno Baba unamaanisha chanzo.
Ukishaelewa hilo automatically kama hawatoki chanzo kimoja hawawezi kuwa Ndugu.

Tumbo ni sehemu ya kuhifadhia mtoto temporary na sio chanzo cha mtoto.
Mbegu ya kiume ndio chanzo cha mtoto

Na walochangia baba mama tofauti je?
 
Yote Kheri.
Amekuona huna pesa na zaidi hakukupenda Kwa dhati
Ni kweli sina pesa

Kwenye kunipenda ni kweli pia maana nilimdanganya nitampa connection ya job KITENGONI so alikuwa ananipa game kati hali ya utumwa Fran hvi
 
Habarini wakuu,

Wiki hii nimeoa single mom, mtoto wake ana miaka 2 tangu azae jamaa alikimbia na hajulikani alipo hadi sasa hakutoa hata mia kwenye malezi ya mtoto, alisaidiwa kulea mtoto na mama yake, mtoto kamuacha kwao na mimi sitaki kuishi na huyo mtoto wake na yeye ashalikubali hilo maana tangu uchumba wetu wa mwaka mmoja, nishamwambiaga sitokaa na mtoto wako.

Ananipenda sana tena ile sana sijawahi kupendwa kama hivi kwa huu umri wangu wa 29 years nimewaacha wengi sana nimeamua yeye kumuoa nimeona hatasumbua kwa chochote maana ni mpole na msikivu sana.

Nimekuja tu humu kuwapa hiyo taarifa na kuja kuona mnaniusia wosia gani, kwa hiyo karibuni kwa maoni ya jinsi ya kuishi nae, na vitu gani nijitahadhari navyo, ushauri wowote pia unaruhusiwa na chochote ulichonacho cha kuniambia hata kiwe kibaya sawa tu karibu sana.

Dha, kwanza una roho mbaya. Usitegemee baraka katika hiyo ndoa. Huyo mtoto kakukosea nini mpaka umemtenganisha na mama yake. Hivi ungefanyiwa hivyo, ungejusikiaje?. Ngoja nikwambie ukweli huyo mwanamke ni mskivu lakini Si mama mwemwa. Na baraka ambazo ungepata kwa kulea huyo mtoto na kuishi naye ni nyingi mno. Sasa, yanafuata ni machungu zaidi. Nakuhakikishia ndoa isiyo na amani wala baraka. Usichezee na Mungu.
 
Huyo mwamba akijua tu kuwa bidada kaolewa, chances za yeye kurudisha majeshi ni kubwa sana. Kama akili za huyi mkeo ni ndogo, lazima mwamba atamla, ndoa yako itaingia doa au kufa kabisa. Omba Mungu awe mke mwema.
hilo halina Shaka ni mke mwema sana tena sana hilo naomba muamini hata kama hamumujui
 
kivip fafanua
Ukioa mama mwenye mtoto wa kike ni rahisi kukop na mtoto wa kike,ila wa kiume anapokua kamwe haji kukuelewa and the same mwanamke akaolewa na single faza mwenye mtoto wa kike.

Ni wazo tu, usinichukulie serious
 
Siwezi na sitakuja weza kuishi na mtu akithubutu au kutamka au nikhisi anabagua mtoto wangu
Mtoto wangu kwanza
We hako katoto kanakupunguzia nin na watazaliwa ndugu zake hapo,ukishaamua kitu amua
Ukipenda boga penda na ua lake
Kwani huyo mtoto hana baba?

Hao watakaozaliwa nao watakuwa na baba yao, mkizaa na mtu mwingine na kuachwa usimtupie bwana mwingine wa/mtoto kisa ubaguzi NO!, Haipo hivyo
 
Kwani huyo mtoto hana baba?

Hao watakaozaliwa nao watakuwa na baba yao, mkizaa na mtu mwingine na kuachwa usimtupie bwana mwingine wa/mtoto kisa ubaguzi NO!, Haipo hivyo

Sijamtupia mtu ila ukioa mwanamke Ana mtoto hutakiwi bagua lasivyo oa ambae hana mtoto
 
Wanaume tuna wivu wa ajabu Sana

Nikuhakikishie TU
Huyo mzazi mwenzie yupo Hapa mjini
Na anajua kila kinachoendelea na mzazi mwenzie, sema kwasababu yupo yupo TU anateseka na dunia, jamaa anajikausha.

Ila kwasababu kaskia umemuoa,
ataibuka kwa Kasi ili kurudisha majeshi na mzazi mwenzie

Na sio anarudisha majeshi kwasababu anampenda Sana binti, Bali kukuonesha kua yeye Ni jemedari alikutangulia na anaweza kukuchapia kirahisi.
Lengo amharibie binti mahusiwno ili arudi Tena kweye msoto.

Na wanawake walivo dhaifu kwenye hili, Lazima TU Atanasa ktk mtego huu.

Na Hapo ndo kilio na majuto yako vitaanzia.

Sikutishi,
ila nakwambia ukweli,
Ili ujipange kisaikolojia Kama kweli unampenda uyo binti na umedhamiria
daah! apana siamini hayo unayosema mkuu na utaniwia radhi kutokubaliana na mawazo yako
 
Na walochangia baba mama tofauti je?

Hao ni ndugu.
Kinachoangaliwa ni mzizi/chanzo cha kiumbe,
Ndio maana wewe ukizaa na wanaume watatu, mchaga, Msukuma na Mhindi
Watoto hao watakaotoka watakuwa sio kabila au asili moja.
Bali watakuwa ni mmoja mchaga, mwingine msukuma na huyo wa mwisho ni Mhindi.

Lakini mwanaume akizaa na wanawake wa jamii hata kumi, watoto wote wataitwa Kwa asili yake(mwanaume).
 
Wewe na huyo baba aliekimbia mtoto hamna tofauti.

Kwanini umkatae mtoto, binafsi kama ntaoa singo maza(japo sitegemei hilo) ila kama ikitokea basi mtoto pia ntamchukua kama wangu iwapo baba yake kamtelekeza, ila kama baba anawajibika katu siwezi kua na huyo mwanamke.
msinishauri juu ya kuishi na kumlea huyo mtoto tafadhali hili ni reply yangu ya mwisho juu ya ushauri wa kuishi na mtoto ambaae so wangu,mtaniwia radhi sana
 
Back
Top Bottom