Nimemkopea pesa kwa mtu hataki kurudisha

Nimemkopea pesa kwa mtu hataki kurudisha

Ukifatilia maisha ya ma capitalist na jinsi walikuwa wana hustle kutafuta pesa zao.

Kitendo cha mtu kumrusha mtu pesa ni kitendo cha hatari mno, Ndo mana mara chache ufanye kitu na mzungu u mrushe halafu akuache.

Atakutafuta tu akunyooshe.. Na hiyo ndo dawa ya mdaiwa.. Ni kumnyoosha tu

Yaani dada angu usije ukasamehe hii hela huyu mtu itabidi akulipe. ikibidi kaa chini weka strategies kabisa.. Huyu usimwache kabisa.. Yaani khaaa ingekuwa ni mimi daaaah aiseeeee..

Mtu anakurushaje pesa yako?
 
Nikienda kwenye swala la msingi.. Huyu mtu unaweza ukafanya yafuatayo akilipe pesa yako..


1. Muoneshe umekasirika.. Vaa uso wa mbuzi kunywa hata bia tatu halafu muibukie kama chizi u mchimbe biti la ukweli na ikiwezekana na matusi juu.. Hapa unaweza ukanikodisha nikusindikize.

2. Mu expose kwa watu ili umtie aibu.

3. Nenda polisi uwaeleze vizuri hata umfungulie kesi ya utapeli.. Huko kwenye upelelezi itakuja kujulikana.. Hapo lazima polisi wamfanyie harassment.

4. Tenga wiki mbili za kumtafuta.. Yaani hata watu wa karibu wawe wanampa habar kwamba unamtafuta akulipe deni lako.

Lengo kuu hapo ni kumtia jamba jamba kwamba anatakiwa akulipe pesa yako na si vingine. Na umuoneshe kwamba umejitoa kufanya chochote mpaka akulipe..

Yafanye hayo utakuja kuniambia..

Ikishindikana kabisa huyu itabidi akodishiwe watu apewe kichapo atibiwe na hiyo milioni..
Huyu mtu hadi kumlilia nilishawahi ila ana moyo mgumu. La kumuexpose kwa watu ndo nililokua nalifikiria. Nitafanyia kazi ushauri wako mkuu.
 
Ukifatilia maisha ya ma capitalist na jinsi walikuwa wana hustle kutafuta pesa zao.

Kitendo cha mtu kumrusha mtu pesa ni kitendo cha hatari mno, Ndo mana mara chache ufanye kitu na mzungu u mrushe halafu akuache.

Atakutafuta tu akunyooshe.. Na hiyo ndo dawa ya mdaiwa.. Ni kumnyoosha tu
Huyu hata kama nitamlipia deni lake ila nitamnyoosha. Nitamtia aibu kweli. Maana anajifanya ana maisha ya kitajiri kwa watu halafu anashindwa nilipa hela kama hiyo.
 
Kuna mtu alikuja ana shida nimsaidie million moja atarudisha baada ya siku 3, nilimuamini nikamwambia sina ila nitamtafutia. Nikaipata kwa mtu nikampatia, ila sasa toka aseme anairudisha mpaka leo zimepita week 3 kila siku ananiletea story kuwa anatafuta ananiletea nyumbani ila haleti, juzi nilikutana na mtu akawa ananiambia huyo mdeni ni tapeli ameshaomba hela kwa watu wengine na aliniambia hivyo bila kujua na mimi nimeshampatia pesa. Sielewi hiyo hela naipataje na mimi sina hiyo hela kusema ntailipa mara moja tu. Nisaidieni nifanye nini huyu mtu arudishe pesa ya watu.
Andaa arrangement na huyo aliyekukopesha uweze kulipa million ya watu vinginevyo atakusumbua utakosa amani
 
Huyu mtu hadi kumlilia nilishawahi ila ana moyo mgumu. La kumuexpose kwa watu ndo nililokua nalifikiria. Nitafanyia kazi ushauri wako mkuu.
Daaah anyway nakuonea huruma.. Natamani ungekuwa na ujasiri kama wale wamama wakichaga.

Mtu kila siku anafatwa asubuhi nyumbani kwake ni unapigwa wimbo mtaa mzima unakusanyika kuja kusikiliza mtu anavodaiwa..

Na ndo hapo nilianza kujifunza ubandidu. Huyu mtu mfate asubuhi mpigie wimbo wiki nzima mfululizo ikibidi majirani waje..

Anyway, najua ni ngumu unaweza kuwa labda wewe ni mdada wa kisasa huwezi kufanya hivo na ndo mana jamaa anakuzungusha maana ashajua weakness yako ilipo.. Huwezi kumdai
 
Back
Top Bottom