Nimemeza pin imenikwama kooni nifanyeje

OME123

JF-Expert Member
Oct 4, 2010
1,498
605
Wanajamvini naomba msaada wenu kuna siku nilikuwa nachokonoa meno na stepple ikawa kipande cha stepple pin likavunjika nikaimeza imenikwama kooni napata maimivu makali sana nifanyeje ni wiki ya pili sasa maumivu yananitesa nombeeni msaada ndugu
 
Pole sana jaribu kunywa maji halafu unafanya kama unasukutua kwa kuinua kichwa juu kidogo na kusukutua sehemu ya koo. Pia kuwahi hospitali ni muhimu sana kabla hali haijawa mbaya zaidi.
 
Pole sana, nilidhani lugha ya picha. Wahi hospitali usijepata tetenasi.
Acha uzembe jali afya yako.
 
Wiki mbili ingekuwa imekukwama hiyo homa yake usingeingia JF.Itakuwa ni kidonda tu ama memory of pain that was registered in the brain.Kwa uhakika zaidi onana na ENT.Usirudie tena eeh
 
Tafadhari nenda hospital kama upo dar usiende hospital za ****** nenda regence au kairuki au mama ngoma
 
mkuu umemeza steppler? dah! hii inaitwa ofisi tumboni. wahi hospitali kabla hiyo stepler haijafanya zile shuhuli zake za kutoboa na kuunganisha huko stomach world
 
meza tonge kubwa la ugali.natania.
hamna pin,sema ni kidonda tu.maumivu yakizidi pata ushauri wa dr.unacheza na pin!?.
 
pole sana,,naamini umeshareport hosp,,,siku nyingine usirudie tafadhali,,,:car:
 
We sidhan kma una maumivu kweli! Coz kma ungekuwa nayo ungekuwa ushawahi hospital. Weka sumaku kwa nje itatoka bila kupenda!
 
Kama bado iko kooni na hujaenda kuonana na madaktari, basi inabidi upigwe chini pini itokee juu!
 
Uko kijiji gani wewe? Yaani wiki mbili bado hujaenda hospitali tuuu! Utapata inflammation ambayo itakuja kuziba koo kabisa ushindwe kumeza chochote na matokeo yake ni kufa. Hivyo wahi hospitali haraka ili waone ni jinsi gani ya kukusaidia! Siku nyingine usirudie kutumia pin, maana wachina wamewaletea tooth pick wewe unatumiaje pin?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom