Nimekwisha na UKIMWI

Nimekwisha na UKIMWI

wamekupima na kipimo gani mkuu?
wamenitoa damu ya mkono mkuu nikaulizwa kama nina mke,umri wangu,na kama nimewahi kupima basi,nikaambiwa nisubirie majibu,na sehemu ya tatu nilienda kuna hivi vituo vya afya kinaitwa UMATI,napo wameniuliza tu maswali hayo hayo then wakanidonoa kidoleni,nikaambiwa nisubiri dk 3,nayo majibu yakawa negative,nimepewa kikadi nimeambiwa nirudi tena tar 7/9 mwaka huu huu...
saiv kwa yeyote anayetaka kujua lolote juu ya majibu yangu,anaruhusiwa kuuliza nitayajibu yote kwa ku`refer niliyokutana nayo huko sehemu nilizoenda kupimwa,kwa sasa ni muda wa zoezi so nitajibu usiku nikiwa nimetulia....sorry!
 
Naandika huku hali yangu ya akili ikiwa mbaya sana, mchumba wangu niliyeishi nae kwa miaka mi 3 amejifungua jana kwa upasuaji, na mwezi November mwaka huu ilikuwa tufunge ndoa.

Ndugu jamaa na marafiki wote tushawatangazia na vikao viwili vya ndugu kujiweka sawa vishafanyika, nimeenda leo asubuhi nimekutana na habari tofauti kuwa mke wangu ni MUATHIRIKA na kibaya ni kwamba alizaliwa nao.

Nimemuuliza kwanini hakuwahi kuniambia tangu mwanzoni, anasema na yeye alikuwa hajui, kesho na mimi nataka nikapime kama hospital 5 hivi ili nijue hali yangu, mwenye lolote la busara naomba anishauri na kunipa moyo, hivi inawezekana majibu ya kesho yakaniacha salama kweli?

Kubwa nawakumbusha wote kamwe usirudie kosa nililofanya mimi la kumwamini huyu mwanamke, tayari nimeshafanya kosa naomba nisilaumiwe.

Nishaurini vizuri nifanyaje kwa sasa, bado sijamwambia ndugu wala rafiki yeyote juu ya hili, nasubiri nipime kwanza ili nijue hatima yangu, nikipima nitareta mrejesho kwa litakalokuwa nimelipata huko.

Ahsanteni
HIV kisayansi inakua lalent kwa muda wa miaka mitano mpaka kumi na kuwa AIDs ambapo hapa magonjwa nyemelezi hufanya kazi yake na hapo anaposema kazaliwa nao inakua tofauti na ilovozoeleka ..ila kama ni kweli unamaambukizi ya hivo virusi usikate tamaa kwa sababu kwa kutumia antiretroviral drugs (ARVs)unaweza kuishi zaidi ya miaka 25 na kuendelea kwaiyo sio mwisho wa maisha ichukulie kama sehemu ya maisha na utaishi miaka mingi tu na huyo mkeo....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni Jambo la kheri hili mkuu lakini bado linaendelea kuzua maswali lukuki.

Anyway nitachangia mawazo yangu huko mbele, kwa sasa kuna shughuli nafanya kwanza
kama una swali ukitulia uliza tu,napenda kila mtu humu ajue miujiza nilokutana nayo,ushauri pia bado napokea coz najua hapa sijifunzi mimi tu,kuna wenzetu wengi humu,wengine mkiwa wachangiaji na mmeathirika,najua mtakuwa mnanielewa vizuri zaidi,kuna mtu ananishauri nimwambie mwanamke apime tena huenda hana wakati ndio yeye kaniambia anao,nahisi sijaelewa anachojaribu kukimaanisha,binafsi sitaki tena kuyazungumzia hayo mambo na yeye,hapa hapa nasaha zenu zitanifaa na kunijenga zaidi wakuu!
 
Hongera kwa kuponea kwenye tundu la simba,je upo tayari kumuoa huyo Muathirika?
 
WAKUU NILIENDA KUPIMA NA NIMEKUTWA MZIMA KABISA,NIMEPITA HOSPITAL 3,NILIANZA NA YA MKOA NA PRIVATE 2,KESHO TAMALIZIA 2,NAJUA HAMTOAMINI ILA NDIO UKWELI NA SI UONGO KWA ANAYEAMINI AAMINI NA KWA ASIYEAMINI AENDELEE KUTOKUKUAMINI,NILIJITOA MHANGA KWASABABU SIKUWA NA KWA KUTOKEA,SIKUWAAMBIA KUWA TANGU NIPATE ZILE TAARIFA SIKUWAHI KULA,NJAA NDIO IMENIUMA LEO,NJAA KALI,NATAMANI NINGEKUWA MLEVI HAKIKA LEO NINGETAMBAA,
UAMUZI NILIOUCHUKUA NI KWAMBA HUYU MWANAMKE SITOMUULIZA CHOCHOTE KUHUSIANA NA HILI AS LONG AS MIMI NIPO SALAMA,TAENDELEA KUMHUDUMIA YEYE PAMOJA NA MTOTO HADI ASHANGAE,NA YEYE NAJUA ATABAKIA NA MASWALI MENGI AMBAYO YATAKOSA MAJIBU JUU YANGU,NAWASHUKURUNI WOTE KWA UJUMLA,KWA MLIONIPA MOYO NA UZOEFU WENU NA PIA MLIONOKASHIFU NA KUNICHEKA,NAWAKUMBUSHA TU KUWA HAPA DUNIANI TUPO KWENYE MAPAMBANO,YEYOTE LINAWEZA KUMKUTA LOLOTE WAKATI WOWOTE,KIKUBWA TU NI KWAMBA NIMEJIFUNZA MAMBO MEEENGI SANA MAISHANI KWA WAKATI MFUPI SANA TANGU ILE JUZI HADI LEO,MWISHO NAAHIDI KUHESHIMU TATIZO LA YEYOTE KUANZIA SASA,NA KAMA NITAKUWA NINA MSAADA WA HALI AU MALI NITAJITAHIDI KUUTOA KAMA SHUKRANI YANGU KWA MUNGU NA WANADAMU WAKE,ASANTENI SANA WATANZANIA WENZANGU,NIPO HAPPY SANA KIASI HATA SINA UHAKIKA KAMA NAANDIKA SAWA...
Safi na hongera kwakua salama.

-Ndumilakuwili-
 
Hongera kwa kuponea kwenye tundu la simba,je upo tayari kumuoa huyo Muathirika?
hapana aisee,nitamlea tu,hasa mwanangu...kifupi kwa sasa sitamani hata kuwa na mwanamke,niwe tu mkweli,huyu mwenyewe angekuwa hana mtoto wangu ningempotezea tu jumla..
 
kama una swali ukitulia uliza tu,napenda kila mtu humu ajue miujiza nilokutana nayo,ushauri pia bado napokea coz najua hapa sijifunzi mimi tu,kuna wenzetu wengi humu,wengine mkiwa wachangiaji na mmeathirika,najua mtakuwa mnanielewa vizuri zaidi,kuna mtu ananishauri nimwambie mwanamke apime tena huenda hana wakati ndio yeye kaniambia anao,nahisi sijaelewa anachojaribu kukimaanisha,binafsi sitaki tena kuyazungumzia hayo mambo na yeye,hapa hapa nasaha zenu zitanifaa na kunijenga zaidi wakuu!
Hongera sana......Mungu aendelee kukulinda na kukupa afya njema zaidi.....Kuna watu wapo kweli kwa ajili ya kuharibu maisha ya watu Mungu aendelee kutulinda
 
Nimeona hapo juu watu wengine wanasema hakuna ukimwi/Hiv.Ukimwi upo na unaua.wako watu kibao ndugu zetu wamekufa na huo ugonjwa na wengine wako hoi vitandani wengine kwenye doze ya dawa kwa muda mrefu sasa sijui mnaosema huo ugonjwa ni uongo mnapata wapi huo ujasiri wakudanganya watu.Ninachojua kwa hakika nikwamba huo ugonjwa ni ugonjwa kama magonjwa mengine cha msingi ukiwa nao nikujali afya yako kwa maana ya lishe na mambo mengine ila Ukimwi/Hiv hupo.
 
hongera sana mkuu mungu ni mwema.ila siku ya kwanza mama kuanza clinic si mlitakiwa mpimwe wote? kwanini hukuenda?. nashauri umpeleke na yeye akapimwe labda hana
sio mke wangu ndio nilikuwa nataka nimuoe baada ya uhusiano wa muda mrefu,na baada ya kupata ujauzito nikaamua ni`process ndoa kabisa,na kipindi anaanza clinic sikuwepo around,kazi zangu ni za kusafiri sana,so suala la clinic sikulichukulia maanani kiivo,narudia hakuwa mke wangu bali nilikuwa natarajia kumuoa..
 
Back
Top Bottom