Nimekwisha na UKIMWI

Nimekwisha na UKIMWI

Pole kwa yaliyokukuta. Hapo kua mkeo alizaliwa nao na alikua hajui kuna mashaka, ukipima virusi vya ukimwi unapata majibu kama vipo au havipo, kua viliingia kwa njia gani huwezi kujua kwa kutumia vipimo labda kwa kutumia historia ya mwathirika unaweza kukisia.
Ushauri: ni kweli ukimwi unatisha lakini ni ugonjwa kama magonjwa mengine, kwa teknologia ya madawa ilipofikia unaweza ishi miaka mingi sana hadi uzee wako ukiwa na maambukizi ya virusi hivyo, na ndani ya hiyo miaka teknologia inaendelae kukua kwahiyo kuna uwezekano mkubwa ikapatikana tiba kabisa au dawa itayovifanya visiwe na madhara mwilini mwako. Hivyo usivunjike moyo na kudhani ndio mwisho wa maisha.
Kama ukikutwa hauna maambukizi (ni kitu kinacho wezekana) mtaalamu atakushauli jinsi ya kuishi na mkeo bila yeye kukuambukiza na mta mlea mtoto wenu salama kabisa na utaendela ku enjoy ndoa yako.
Wish you luck!!
Nina amini sana kuwa huyu akipima atakutwa yupo vizuri sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana kaka. Zingatia ushauri chanya huko juu na uufate.
 
Kitakachokuuwa ni mawazo hayo uliyoyaandika kwenye kichwa cha mada ila sio ukimwi

Tulia kama hujui kinachoendelea vile
 
Nakuombea Mungu kwa yote mema
Mwangalie mwanao na mkeo.
Usitumie madawa yao kama utakuwa nao
Kula vizuri na usiwazie kabisa huo ugonjwa maana ukiuwazia tu ndio unaanza kuwa na msongo wa mawazo na kuiona dunia sio mahali pako.

Ukimwi ni uongo
 
Pole sana
Usikate tamaa hilo ni jaribu la kawaida sana kumbuka kuna mtu umri wako amepata ajali kakatika miguu yote hawezi kutembea na mwingine amepofuka macho umri Kama wako hawezi kuona tena jiangalie je wewe na wao wapi ni bora zaidi usikufuru wala usihuzunike jipe moyo huwezi juwa mipango ya Mungu akakuinua kupitia hilo jaribu
 
Kuishi na mwanamke miaka mi3 bila ndoa ni uzinzi,Mungu hapendi uzinzi,ametukataza katika vitabu vyake vyote tunavyoviamaini,ulimkosea mungu wako kwanza muombe msamaha.Huwezi kumuamini mtu bila kupima miaka yooote hiyo,Hapo ulipo najua umechanganyikiwa sana,lakini njia rahisi kuliko zote nikupata majibu ya vipimo vyako mwenyewe,ingawa majibu mimi na wewe tunayahisi ni mabaya tu,lakini heri kuupata ukweli.Kukaza mwanamke aliyeathirika miaka yote hiyo kavu kavu hakujawawahi kumuacha mtu salama.Omba Mungu Amigo,then kapime kwani nini?Kwa imani ya dini maisha yetu yalishapangwa yooote hatubadilishi japo kidogo.MKUU GOODLUCK!
mkuu usijifanye kama upo smart sana,haya yamenikuta ila na wewe siku yako inakuja hasa kama una aamini ukiwa kwenye ndoa ndio utakuwa salama,nimekiri makosa yangu,lkn pia kuishi nae miaka 3 nilimaanisha kuwa nae kwenye mahusiano,sikuwa sawa kipindi naandika,nilipanga kuanza kuishi nae baada ya ndoa,naomba usinihukumu hasa kama bado upo hai,lolote nawe laweza kukutokea,tena huwenda likawa baya zaidi ya hili la kwangu,kinachonipa moyo ni kwamba wiki tatu zimepita kuna mdogo wa rafiki yangu nilimtolea damu,na nahisi hadi wakaniruhusu nitoe inamaanisha ilikuwa salama,kesho ndio siku ambayo tajua mbivu na mbichi,nahisi kwa sasa nahitaji faraja zaidi na si kejeri,hii ishu haina mwenyewe,tuombe uzima kesho nitarejesha nitakachotoka nacho maabara...all in all nimefarijika sana kwa wana JF wengi kwa kuwa watu dynamic,mnajua jambo la utani na jambo ambalo ni serious,imenipa moyo sana na narudia kushukuru kwa wote mliooonyeshwa kuguswa na tatizo langu,ki`zaidi mlionifuata PM na kunipa msaada wa mawazo na kila kitu...
 
Usipanic,ukimwi ni ugonjwa kama magonjwa mengine,sikuhizi watu wanaogopa kansa na kisukari na mgonjwa ya INI na mioyo yakutibia India,Pima fuata ushauri utaishi vizuri mno na familia yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naandika huku hali yangu ya akili ikiwa mbaya sana, mchumba wangu niliyeishi nae kwa miaka mi 3 amejifungua jana kwa upasuaji, na mwezi November mwaka huu ilikuwa tufunge ndoa.

Ndugu jamaa na marafiki wote tushawatangazia na vikao viwili vya ndugu kujiweka sawa vishafanyika, nimeenda leo asubuhi nimekutana na habari tofauti kuwa mke wangu ni MUATHIRIKA na kibaya ni kwamba alizaliwa nao.

Nimemuuliza kwanini hakuwahi kuniambia tangu mwanzoni, anasema na yeye alikuwa hajui, kesho na mimi nataka nikapime kama hospital 5 hivi ili nijue hali yangu, mwenye lolote la busara naomba anishauri na kunipa moyo, hivi inawezekana majibu ya kesho yakaniacha salama kweli?

Kubwa nawakumbusha wote kamwe usirudie kosa nililofanya mimi la kumwamini huyu mwanamke, tayari nimeshafanya kosa naomba nisilaumiwe.

Nishaurini vizuri nifanyaje kwa sasa, bado sijamwambia ndugu wala rafiki yeyote juu ya hili, nasubiri nipime kwanza ili nijue hatima yangu, nikipima nitareta mrejesho kwa litakalokuwa nimelipata huko.

Ahsanteni
Hujaisha Mkuu.

Kapime kwanza, kuna probability kubwa tu ya kutembea na mtu aliyeathirika several times na bado ukabaki kuwa salama.

Nimekutana na kesi zaidi ya 5 (uhalisia siyo story ya kutunga) ambapo mke ameathirika lakini mume ni mzima.

Usiwe na hofu Mkuu. Hata ikitokea umeathirika bado una muda mrefu tu wa kuishi hapa duniani. Kuna mtu (namfahamu) ameathirika tangu mwaka 1992 lakini hadi leo ni mzima mwenye siha njema kabisa.

Mungu akupiganie Mkuu, maisha ni mlolongo wa matatizo mengi yenye chembechembe kidogo za furaha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kwa nini unasema una ukimwi? Je vipimo fake hospitali ndo vinakufanya useme una ukimwi?
Je umedhoofu?
Ngoja nikuambie ndugu, Ukimwi upo na unasababishwa na lishe duni tu pamoja na matumizi mabaya ya mwili kama Pombe, ngono nyingi, na baadhi ya dawa za hospitali ukizitumia unapata Ukimwi.
lakini ukimwi hausababishi na kirusi cha HIV kama tulivyoamanishwa. Huyo mkeo hana anaweza kuwa na Ukimwi lakini asiwe na HIV.
Tena nakuonya usijaribu kuanza kutumia ARV ndo utaanza kuugua kweli ukimwi, anza lishe bora na ufuate kanuni za afya ili uepuke mtego wa ARV.
Hizo dawa ni mtego wa kibiashara ya madawa ya Viwanda vya madawa. Chunga sana na ujifunze zaidi kuhusu hiyo kitu.
Jaribu ku google na ujifunze zaidi kuhusu "Aids is a hoax".
Aisee saidia kuelimisha watu nimependa hii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe nenda kapime ataukipatikana nao wewe hutakuwa wa kwanza,la mhimu kubali hali utakayokutana nayo,kwa wakati huu huna haja yakuogopa dawa zipo ukijikubali na kutumia dawa utadunda tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom