Nimekuwa mlevi, nisaidieni jamani

CharmingLady

JF-Expert Member
Apr 16, 2012
18,113
2,000
Habari za mchana huu wapendwa, ni muda mrefu nimekuwa nikinywa maji ya moto. Yaan 90% ya maji ya kunywa ninayokunywa ni ya moto. Nimekuwa zaidi ya mlevi, yaan hata nikipatwa kiu nikinywa maji ya baridi lazima nipate na ya moto!

Nimesikia ya kwamba maji ya moto yana madhara kama kukausha mwili, je ni kweli na je nitakuwa nimepata madhara kwa kunywa maji ya moto???

N.B. Maji ya moto ninayokunywa ni yale yaliyochemshwa yakapoa kidogo kiasi kwamba hayaunguzi mdomo.

Ushauri wenu ni muhimu sana kwangu.

Asanteni....
 

valid statement

JF-Expert Member
Sep 18, 2011
2,775
2,000
Ulevi wako ni mzuri kwako, ila ni mbaya kwa pato la taifa.
Mimi nilidhani ulevi wako ni ule wa kupata bidhaa za TBL na SBL.
Kuza pato la nchi, badilisha aina ya ulevi wako.
 

Makamee

JF-Expert Member
Nov 29, 2013
2,020
1,250
Faida za kunywa maji ya moto/vuguvugu.

1.Changanya na limau au asali mbichi kiasi kidogo,
a.Husaidia kuondosha
heart attack.

b.Huboresha uyeyushaji
wa chakula.
c.husaidia kuondoa
sumu mwilini.
d.husafisha tumbo
e.husaidia kuyeyusha
mafuta yasiotakiwa
mwilini hivyo kufanya
blood circulation
ifanyike kwa wepesi
zaidi.
f.Husaidia kupata
kuondosha vijiwe ktk
kidney.
g.Husaidia kupata haja
kubwa yenye afya
kiulani.
Kama ukiweza kunywa maji ya uvuguvugu kila asubuhi kabla ya kula chochote.
 

King'asti

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
27,757
2,000
Unaogopa mwili kukauka ukawa kaukau?
heh, inabidi upelekwe rehab mamii, ila ukitoka huko hukawii kuwa unakunywa wine tuu.
swali kwako, hebu google ujue temperature ya ndani ya tumbo lako la chakula kwanza ushangae
 

miss chagga

JF-Expert Member
Jun 7, 2013
57,917
2,000
Mi nakunywa ya moto sana nahisi kama ni ulevi tupo wengi aisee.. usinywe moto saaana at least ya vuguvugu..... mi nakunywa naweka na limao na wakati mwingine green tea
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom