Nimekuwa mlevi, nisaidieni jamani

Habari za mchana huu wapendwa, ni muda mrefu nimekuwa nikinywa maji ya moto. Yaan 90% ya maji ya kunywa ninayokunywa ni ya moto. Nimekuwa zaidi ya mlevi, yaan hata nikipatwa kiu nikinywa maji ya baridi lazima nipate na ya moto!

Nimesikia ya kwamba maji ya moto yana madhara kama kukausha mwili, je ni kweli na je nitakuwa nimepata madhara kwa kunywa maji ya moto???

N.B. Maji ya moto ninayokunywa ni yale yaliyochemshwa yakapoa kidogo kiasi kwamba hayaunguzi mdomo.

Ushauri wenu ni muhimu sana kwangu.

Asanteni....

Mimi nikidhani ni ule ulevi original (I mean wa pombe) ili nami nikopi tiba utakayopewa! I hate drinking am struggling to stop hadi mke wangu Kongosho anakaribia kunipiga kibuti!
 
Ulevi wako ni mzuri kwako, ila ni mbaya kwa pato la taifa.
Mimi nilidhani ulevi wako ni ule wa kupata bidhaa za TBL na SBL.
Kuza pato la nchi, badilisha aina ya ulevi wako.

Mkuu mbona maelezo yako yanakinzana?? Kama ulevi wangu ni mzuri nitaubadilishaje??
 
Faida za kunywa maji ya moto/vuguvugu.

1.Changanya na limau au asali mbichi kiasi kidogo,
a.Husaidia kuondosha
heart attack.

b.Huboresha uyeyushaji
wa chakula.
c.husaidia kuondoa
sumu mwilini.
d.husafisha tumbo
e.husaidia kuyeyusha
mafuta yasiotakiwa
mwilini hivyo kufanya
blood circulation
ifanyike kwa wepesi
zaidi.
f.Husaidia kupata
kuondosha vijiwe ktk
kidney.
g.Husaidia kupata haja
kubwa yenye afya
kiulani.
Kama ukiweza kunywa maji ya uvuguvugu kila asubuhi kabla ya kula chochote.

Asante kwa ushauri mkuu... Nitajitahidi kutafuta asali mbichi!
 
Mkuu charminglady,

Natumaini unamaanisha maji vugu vugu, Pia tunashauri watu watumie maji mengi(yakiwa ya moto au baridi), lakini tunapemdelea zaidi maji ya moto(yaliyochemshwa kisha kupoa) yaani yasiyo na ubaridi wa Friji/'Friza au Barafu, ingawa katika baadhi ya sehemu mfano, baada ya kumalizq mchezo maji yenye ubaridi 'husuuza' koo.

Hivyo kwako wewe sioni shida yeyote kwa kutumia kiasi kingi/kikubwa cha maji, lakini si sahihi kusema maji ya moto "yanakausha" mwili mkuu.
 
Last edited by a moderator:
Faida za kunywa maji ya moto/vuguvugu.

1.Changanya na limau au asali mbichi kiasi kidogo,
a.Husaidia kuondosha
heart attack.

b.Huboresha uyeyushaji
wa chakula.
c.husaidia kuondoa
sumu mwilini.
d.husafisha tumbo
e.husaidia kuyeyusha
mafuta yasiotakiwa
mwilini hivyo kufanya
blood circulation
ifanyike kwa wepesi
zaidi.
f.Husaidia kupata
kuondosha vijiwe ktk
kidney.
g.Husaidia kupata haja
kubwa yenye afya
kiulani.
Kama ukiweza kunywa maji ya uvuguvugu kila asubuhi kabla ya kula chochote.

Mhudumuuu, LETE YA MOTO NA LIMAU NIPATE AFYA DAKTARI WETU KAAGIZA ZITOE ZOTE KWENYE FRIJI
 
Mkuu charminglady,

Natumaini unamaanisha maji vugu vugu, Pia tunashauri watu watumie maji mengi(yakiwa ya moto au baridi), lakini tunapemdelea zaidi maji ya moto(yaliyochemshwa kisha kupoa) yaani yasiyo na ubaridi wa Friji/'Friza au Barafu, ingawa katika baadhi ya sehemu mfano, baada ya kumalizq mchezo maji yenye ubaridi 'husuuza' koo.

Hivyo kwako wewe sioni shida yeyote kwa kutumia kiasi kingi/kikubwa cha maji, lakini si sahihi kusema maji ya moto "yanakausha" mwili mkuu.

Nashukuru kwa kunitoa wasiwasi, make nilikwua na wasi wasi sana! Barikiwa
 
Habari za mchana huu wapendwa, ni muda mrefu nimekuwa nikinywa maji ya moto. Yaan 90% ya maji ya kunywa ninayokunywa ni ya moto. Nimekuwa zaidi ya mlevi, yaan hata nikipatwa kiu nikinywa maji ya baridi lazima nipate na ya moto!

Nimesikia ya kwamba maji ya moto yana madhara kama kukausha mwili, je ni kweli na je nitakuwa nimepata madhara kwa kunywa maji ya moto???

N.B. Maji ya moto ninayokunywa ni yale yaliyochemshwa yakapoa kidogo kiasi kwamba hayaunguzi mdomo.

Ushauri wenu ni muhimu sana kwangu.

Asanteni....
Nimechelewa uzi..hayana madhara kabisa kwa sababu siyo yale ya moto kabisa kama ulivyosema..yatakuwa absorbed kama maji mengine tu
 
Back
Top Bottom