Nipo mkoa wa Kilimanjaro kikazi, Idi imenikuta huku, nikasema nipate moja baridi bar ya jirani na hoteli nilipofika, nilikua mwenyewe kwenye Meza,Mara wakaja warembo wawili kukaa kwenye Meza yangu, mda ulivyozidi kwenda tukazidi zoeana, kama mtanashati nikawaagizia vinywaji, kwakua nilikua nimechoka Sana na kazi kwa siku ya Leo basi ilipofika saa nne nikawaaga kuwa nakwenda kupumzika, kuona hivyo wakaniambia kwamba kwakua Mimi Ni mgeni basi watanisindikiza mpaka nilipofika ili wanilinde, wakuu tulipofika barabara kuu nageuka sioni wale mabinti nilio kua nao, Nimeingia woga mpaka muda huu, ukizingatia kazi iliyonileta hapa Ni ya Siku 9 na hii Ni ya 3,