Nimekuta 74,549,940.36 kwenye account yangu

Naombeni msaada tafadhari!

Mauza uza haya nilianza kuyaona mwezi wa nne nilipokuwa nataka kusafiri kwenya Italia, kwa kuwa card yangu ya CRDB ilikuwa ni Tembo card na siku renew niliamua kwenda kuactivate account yangu ya STANDARD CHARTERD bank ambayo awali ilikuwa na deni la kama -63700. nilifanya hivi makusudi ili nipate card mpya (credit card) ntakayotumia Italia

Nilipofika benk nilijaza kwanza form ya kuangalia salio na kumpatia CASHIER ambapo aliangalia balance akajaza akanirudishia nikakuta 765,000 nikashtuka kidogo, afu nikataka kuuliza nikaona ngoja niuchune, nikaaa pale benk nikiwaza baadae nikaondoka zangu. kwa kuwa nilikuwa na hela sikudeal nayo sana ile hela. baada ya kama wiki nikaona nikacheck tena salio nikakuta 735000 nikaona nitoe 50000 kutest na kweli zikatoka nikatulia. nikasafiri zangu

Sasa juzi tar 02 nikasema ngoja niende ATM nikaangalie kama ile hela ipo, ile kuomba balance kwa ATM nikaona imenitolea karatasi inaonyesha salio 74,549,940.36, nikachanganyikiwa! sikutoa hata shilingi nikaogopa. leo tena nimeenda pale mikocheni nimeangalia salio nimelikuta hilo hilo duu nimechanganyikiwa na naogopa hebu nisaidieni nifanye nini na hizi hela

Niende police?
Nikariport bank?
Niuchune nitumie?

Nenda polisi na mchukue a senior police officer, halafu pia nenda Takukuru na pia usalama wa taifa na baada ya hapo uende benki...na ikiwezekana nenda na maofisa wote hapo benki...na Hapo Benki umuone Meneja wa benki
 
ripot bank usije fungwa bure huko mbelen

lakin hii stori tamu
umenikumbusha enzi zile za utoto nilitamani sana ndege ya WORLD BANK ianguke nje ya nyumba yetu
Mkuu mm hii stori imenikumbusha mambo mawili, la kwanza wakati nasota A'level kule Tosamaganga nguna ya shule na harage ilinichosha nilikuwa napata kiungulia kikali balaa, siku moja nina njaa kali ikapita gari ya pepsi nikatamani lidondoke nichukue soda halaf lipite gari la mikate nalo lipinduke hapo hapo

Issue ya pili ninayokumbuka wakati nipo chuo bodi ya mkopo waliniingizia bumu mara 2, sasa semister iliyofuata nilikuwa nimemaliza bumu mapema kuna jamaa yangu tupo nae room nikamwambia natamani TIRDO (wakati ule ofisi za bodi zilikuwa huko) namwambia natamani wakosee tena waniingizie bumu tena, jamaa akaniambia twende tukachungulie NBC, looh, kufika kweli wamekosea wamenitumbukizia, hatareee, , ila ndo hivyo tunalilipa now.
 
Bank huwa hawakosei. Huenda "zimehifadhiwa" hapo na mafisadi kwa muda baada ya kuona huitumii akaunti yako kwa muda mrefu.

Cha kufanya sasa. Vuta kama milioni 40 hivi ukaifungulie fixed account KCB/CRDB na uskilizie. Siku wenye nazo wakirudi watakuta hazipo na huenda wasikufanye kitu. Usiweke tena pesa kwenye hiyo account
 
Hizo pesa usitoe wala kufanya jambo lolote ila jaribu kumuuliza kwa meneja kuchek hiyo pesa imeingizwa lini( jifanye kuna mtu alisema atatuma pesa ili uweze kujua inatokea wap hiyo pesa ) na usiongee kwa mtu kwanza ili ufanye uchunguz wako . pia jambo la Pili inategemea kaz zako unazofanya inaweza ikawa unawekewa mtego ili kupate skendo au ufungwe kwa tuhuma za rushwa kikubwa hiyo pesa usitoe taarifa . fumba macho kama haipo vile kipind unaendelea na uchunguz wako ukiona zipo sawa mkuu tumia kwa kujengea nyumba au mradi wenye kuzalisha faida mfano kujenga nyumba za kupangisha , kujenga guest house na kununua mashamba . ila kikubwa zaid jitahid uchunguzee wewe mwenyewe kama imekosewa basi itakuwa bahat yako
Am kweli watanzania tuna nyota ya umaskini kabisa, Hakuna cha kujiuliza ni kubeba pesa tu, hayo mengine baadae.
Watu hatulali kutafuta pesa, mtu unayakuta mapesa unaanza kusita,this is crazy.
 
Acha mambo ya kijinga wewe, kadraw yote milioni 30 tutatumia kuhonga wakati wa kesi, profit milioni 45, nitafute nikupeleke bar yenye mademu wakali. hahahahahhahahahahhaha
 
Hizo ni hela za Simba sport club, huenda zimewekwa hapo kwa muda kukwepa kodi/ Takukuru, kwahiyo kama ni mwanachama wao ziache tu, kama wee ni Yanga zile zote, hata wakikukamata watajua unatania kwa kuwa wewe ni mtan wao ..!!

CC Aveva ...!!
Hahahajaha
 
Nitafute nikupe njia ya kufata na utafanikiwa kwassbabu iko kwenye akaunt yako mbona Hamna shida
 
Naombeni msaada tafadhari!

Mauza uza haya nilianza kuyaona mwezi wa nne nilipokuwa nataka kusafiri kwenya Italia, kwa kuwa card yangu ya CRDB ilikuwa ni Tembo card na siku renew niliamua kwenda kuactivate account yangu ya STANDARD CHARTERD bank ambayo awali ilikuwa na deni la kama -63700. nilifanya hivi makusudi ili nipate card mpya (credit card) ntakayotumia Italia

Nilipofika benk nilijaza kwanza form ya kuangalia salio na kumpatia CASHIER ambapo aliangalia balance akajaza akanirudishia nikakuta 765,000 nikashtuka kidogo, afu nikataka kuuliza nikaona ngoja niuchune, nikaaa pale benk nikiwaza baadae nikaondoka zangu. kwa kuwa nilikuwa na hela sikudeal nayo sana ile hela. baada ya kama wiki nikaona nikacheck tena salio nikakuta 735000 nikaona nitoe 50000 kutest na kweli zikatoka nikatulia. nikasafiri zangu

Sasa juzi tar 02 nikasema ngoja niende ATM nikaangalie kama ile hela ipo, ile kuomba balance kwa ATM nikaona imenitolea karatasi inaonyesha salio 74,549,940.36, nikachanganyikiwa! sikutoa hata shilingi nikaogopa. leo tena nimeenda pale mikocheni nimeangalia salio nimelikuta hilo hilo duu nimechanganyikiwa na naogopa hebu nisaidieni nifanye nini na hizi hela

Niende police?
Nikariport bank?
Niuchune nitumie?
yaani bora wewe mi kuna jamaa yangu alikuta 90m.....kumbe nasikia walikuwa wanatumia account yake kuibia hela....ikaenda ile 90m ikatoka, wakaweka 40m ikatolewa last year wamemuachia 24m na mpaka leo hakuna aliyeitoa
 
Aisee mimi ningezitoa zote, kama ni kifungo c nitafungwa kwa mzee wa Unaa nikafagie fagie tu M'nyamala hosptl (utani tu)......
 
Mkuu huo Mpunga bado upo? Usawa huu wa hapa kazi unauliza nini cha kufanya?
 
Toa mzigo wote fanya biashara ambayo ipo sensitive u generate hela then hata wakikutafuta miaka ijayo uwe na uwezo wa kurudisha.
Acha ujinga huo ni mtaji
 
Back
Top Bottom