Kinachoendelea kwenye akaunti za benki za watu ni umafia

Mwanafunzi mtoro

JF-Expert Member
Aug 3, 2021
223
797
Natanguliza salamu kwa unyenyekevu kabisa.

Juzi kati nilienda benki nje kwenye ATM kuuliza salio. Salio lilionesha laki kadhaa na elfu kumi. Sikutoa hata mia, nikajisemea moyoni hata kesho naweza kuzitoa kwanza zipo sehemu salama.

Siku iliyofuata nilienda tena ATM niliona bora nitoe pesa zote . Chakushangaza ikagoma nikaona acha niiache hiyo teni labda tozo inasababisha hata hiyo elfu kumi isitoke lakini napo hola.

Nikaona ngoja niulize salio, nilikuta elfu 10 na zaidi haipo. Nikatoa iliyopo na chenchi nilienda kutolea kwa wakala. Hapo imepungua kana elfu 13 hivi.

Basi nikapuuzia nikiamini labda ni mambo ya kitaalamu hayo haina haja kuwasumbua wataalamu. Niliamini huenda labda nilichukua bank statement ndio imekatwa sasa.

Sasa jana kuna mtu alitaka kunitumia vihela kidogo nifanye matumizi yangu ilikuwa kama laki kamili. Basi nikamweleza asiweke mpesa kutokana na mambo ya tozo. Basi nikampa acc. akaniwekea laki kamili.

Asubuhi nilipoamka nikasema sasa nikatoe. Ile kubofya laki ikagoma nkadhania kwakuwa pesa ilikuwa laki lazima igome. Nikatoa 90 huyo mbele.

Nikaenda hadi kwa wakala wa benk, nikamwambia naomba nitoe efu 7 ikawa hola. Jaribu elfu 6 hola jaribu elfu 5 hola jaribu elfu 4 hola alooooh. Kujaribu elfu 3 ikakubali.

Sasa swali nikajiuliza tangu lini gharama ya kutoa elfu 90 ikawa elfu 6, elfu 6 na miatano au 7 ??

Nikahisi benk wananizoea sasa ngoja niwafuate . Hapo ndio nilipewa maelezo nikachoka kabisa.

Hapo ndio niliona kumbe hawakuchukua benk yani niliambiwa sijui kuna money nini hiyo ya serikali walitangaza kumbe. Yaani nilikuta wamekata pesa hovyo hovyo timtim kama geto la chizi.

Dokezo 1
Kabla yangu juzi nilikuta dada flani nje ya benki analalamika elfu 25 hajui imekatwa ya nini. Nilihisi hayanihusu ni ishu binafsi kumbe ningezingatia maumivu yake huwenda ningeshtuka kupitisha pesa benki sio salama tena.

Dokezo 2
Wakati naeleweshwa kuhusu hayo makato mapya ghafla sura ya Ndugai ikanijia mbele yangu. Ndipo nilianza kuelewa kuwa kumbe aliposema kuna siku nchi itapigwa mnada hakumanisha kwamba raia tutafukuzwa bali tutaishi kwa mateso kama tupo nchi ya ugenini. Binafsi namuomba msamaha bwana ndugai . Hakika tulilewa mvinyo wa awamu mpya.

Twendelee
Sasa naanza kuhisi hata hizi post kodi kuna siku watu watakuja kusaga meno na kilio kikubwa . Lakini yote ya yote tumejifunza mara nyingi tumeona "Mungu huingilia kati popote kwenye malalamiko yaliyozidi". Anapolaumiwa kiongozi basi analaumiwa Mungu kwa kuwa wengi huamini uongozi hutoka kwa Mungu.
 
Juzi nilitoa kwa Wakala kupitia NMB mobile... Nilikuwa na 352,000 kwenye akaunti.. Nilijaribu 345,000 ikagoma, 335,000 ikagoma.. Ikakubali 330,000... Kucheki balance nikajikuta imebaki buku 7 tu.... Aisee.. Nilisaga meno. Ina maana nilikatwa zaidi ya elfu 20....
 
Kama vipi jamani tuandamane.
Tusikubali kuonewa na hawa wapemba na wa unguja. Nadhani wanatukomoa ili huu muungano tuuvunje.
 
Kama vipi jamani tuandamane.
Tusikubali kuonewa na hawa wapemba na wa unguja. Nadhani wanatukomoa ili huu muungano tuuvunje.
...Wenzetu wa Sri Lanka hawakukubali Uninga huu wa Tozo! Walichukua Hatua. Wakati Sasa Umefika wa Sisi kuacha Ubinafsi na Kuchukua Hatua! Shime ...!!
 
Natanguliza salamu kwa unyenyekevu kabisa.

Juzi kati nilienda benk nje kwenye ATM kuuliza salio. Salio lilionesha laki kadhaa na elfu kumi. Sikutoa hata mia , nikajisemea moyoni hata keshonaweza kuzitoa kwanza zipo sehemu salama.

Siku iliyofuata nilienda tena ATM niliona bora nitoe pesa zote . Chakushangaza ikagoma niona aaah acha niiache hiyo teni labda Tozo inasababisha hata hiyo elfu kumi isitoke lakini napo hola.

Nikaona ngoja niulize salio , nilikuta elfu 10 na zaidi haipo. Nikatoa iliyopo na chenchi nilienda kutolea kwa wakala. Hapo imepungua kana elfu 13 hivi.

Basi nikapuuzia nikiamini labda ni mambo ya kitaalamu hayo haina haja kuwasumbua wataalamu. Niliamini huenda labda nilichukua bank statement ndio imekatwa sasa.

Sasa jana kuna mtu alitaka kunitumia vihela kidogo nifanye matumizi yangu ilikuwa kana laki kamili. Basi nikamweleza asiweke Mpesa kutokana na mambo ya TOZO. Basi nikampa acc akaniwekea laki kamili.

Asubuhi nilipoamka nikasema sasa nikatoe. Ile kubofya laki ikagoma nkadhania kwakuwa pesa ikikuwa laki lazima igome. Nikatoa 90 huyo mbele.

Nikaenda hadi kwa wakala wa benk ,nikamwambia naomba nitoe efu 7 ikawa hola. Jaribu elfu 6 hola jaribu elfu 5 hola jaribu elfu 4 hola alooooh. Kujaribu elfu 3 ikakubali.

Sasa swali nikajiuliza tangu lini gharama ya kutoa elfu 90 ikawa elfu 6 au elfu 6 na miatano au 7 ??

Nikahisi benk wananizoea sasa ngoja niwafuate . Alooh hapo ndio nilipewa maelezo nikachoka kabisa.

Hapo ndio niliona kumbe hawakuchuku benk yani niliambiwa sijui kuna money nini hiyo ya serikali walitangaza kumbe. Yangi nikuta wamekata pesa hovyo hovyo timu timu kama geto la chizi.

Dokezo 1
Kabla yangu juzi nilikuta dada fkani nje ya benki analalamika elfu 25 hajui imektwa ya nini. Nilihisi hayanihusu ni ishu binafsi kumbe ningezingatia maumivu yake huwenda ningeshtuka kupitisha pesa benki sio salama tena.

Dokezo 2
Wakati naeleweshwa kuhusu hayo makato mapya ghafla sura ya Ndugai ikanijia mbele yangu. Ndipo nilianza kuelewa kuwa kumbe aluposema kuna siku nchi itapigwa mnada hakumanisha kwamba raia tutafukuzwa bali tutaishi kwa mateso kama tupo nchi ya ugenini. Binafsi namuomba msamaha bwana ndugai . Hakika tulilewa mvinyo wa awamu mpya.

Twendelee
Sasa naanza kuhisi hata hizi post kodi kuna siku watu watakuja kusaga meno na kilio kikubwa . Lakini yote ya yote tumejifunza mara nyingi tumeona "Mungu huingilia kati popote kwenye malalamiko yaliyozidi" anapolaumiwa kiongozi basi analaumiwa Mungu kwa kuwa wengi huamini uongozi hutoka kwa Mungu.
hatari sana hii mabenk yana obligation ya kutekeleza bila kufanya hivyo yatakumbwa na penalty na fine kutokana na hiyoo finance act ya 2022 july 1 (CAP 437). Ya kulahumiwa ni serikali na ilo wizara lake inaumiza sana hii ndugu zang
 
Juzi nilitoa kwa Wakala kupitia NMB mobile... Nilikuwa na 352,000 kwenye akaunti.. Nilijaribu 345,000 ikagoma, 335,000 ikagoma.. Ikakubali 330,000... Kucheki balance nikajikuta imebaki buku 7 tu.... Aisee.. Nilisaga meno. Ina maana nilikatwa zaidi ya elfu 20....
Pole san unajikuta jasho linavuja bila joto
 
Hila katika jambo hili serikali inachofanya Ni wizi wa dhahiri kabisa, Mimi binafsi nimepanga nikatoe kasenti kangu niangalie nitakaifadhi kwa namna gani, sijaenda kuangalia,hila najua Ni maumivu itakuwa , ningejua ningehamisha kabla........

Mwendazake alikuwa anaendesha Nchi ndivyo sivyo, kaiacha Nchi ikiwa mufilisi kabisa nasikia,

Kuna kajihela nilitaka nikakaifadhi Tangu week iliyopita,kwasasa sitothubutu kabisa
 
Lipa Kodi, hutaki katafute nchi ya kuishi.

Hakuna nchi iliyoachwa mufilisi, kila siku serikali inakusanya Kodi na haijawahi kusimama kukusanya Kodi na chote kinachopatikana kinatumika. Tena sasa hivi makusanyo yameongezeka maradufu.

Tuwe wazalendo
 
PESA ZIPO MABARABARANI HASA KWENYE MAGARI, MENGI YANA INCLUSIONS CHUNGU MZIMA, KUANZIA KWA MADEREVA MPAKA MAGARI YENYEWE, SIJUI KWA NINI LOOPHOLE HII HAWAIONI.
Awamu ya tano iliweka mkazo zaidi humo, awamu ya sita imelegeza,rushwa iondoshwe ili mashine za fine zifanye kazi zaidi kuliko hizo elfu tano tano zinazoishia mifukoni.
 
Back
Top Bottom