Nimekuta 74,549,940.36 kwenye account yangu

Naombeni msaada tafadhari!

Mauza uza haya nilianza kuyaona mwezi wa nne nilipokuwa nataka kusafiri kwenya Italia, kwa kuwa card yangu ya CRDB ilikuwa ni Tembo card na siku renew niliamua kwenda kuactivate account yangu ya STANDARD CHARTERD bank ambayo awali ilikuwa na deni la kama -63700. nilifanya hivi makusudi ili nipate card mpya (credit card) ntakayotumia Italia

Nilipofika benk nilijaza kwanza form ya kuangalia salio na kumpatia CASHIER ambapo aliangalia balance akajaza akanirudishia nikakuta 765,000 nikashtuka kidogo, afu nikataka kuuliza nikaona ngoja niuchune, nikaaa pale benk nikiwaza baadae nikaondoka zangu. kwa kuwa nilikuwa na hela sikudeal nayo sana ile hela. baada ya kama wiki nikaona nikacheck tena salio nikakuta 735000 nikaona nitoe 50000 kutest na kweli zikatoka nikatulia. nikasafiri zangu

Sasa juzi tar 02 nikasema ngoja niende ATM nikaangalie kama ile hela ipo, ile kuomba balance kwa ATM nikaona imenitolea karatasi inaonyesha salio 74,549,940.36, nikachanganyikiwa! sikutoa hata shilingi nikaogopa. leo tena nimeenda pale mikocheni nimeangalia salio nimelikuta hilo hilo duu nimechanganyikiwa na naogopa hebu nisaidieni nifanye nini na hizi hela

Niende police?
Nikariport bank?
Niuchune nitumie?
Asikudanganye mtu, sikuhizi freemanson wanatumia chaneli za mabenki...tafakar chukua hatua
 
Kumbuka hata Siku moja pesa benk huwa haipotei. Kama ni ya benk wamekosea wakiamua kuitrace lazima watajui ilipo

Ni vema labda uombe bank statement llil kujua ni wapi ilipotokea mkuu ili uwe na amani
ushauri mzur..i hope atautendea kazi
 
Hizo pesa usitoe wala kufanya jambo lolote ila jaribu kumuuliza kwa meneja kuchek hiyo pesa imeingizwa lini( jifanye kuna mtu alisema atatuma pesa ili uweze kujua inatokea wap hiyo pesa ) na usiongee kwa mtu kwanza ili ufanye uchunguz wako . pia jambo la Pili inategemea kaz zako unazofanya inaweza ikawa unawekewa mtego ili kupate skendo au ufungwe kwa tuhuma za rushwa kikubwa hiyo pesa usitoe taarifa . fumba macho kama haipo vile kipind unaendelea na uchunguz wako ukiona zipo sawa mkuu tumia kwa kujengea nyumba au mradi wenye kuzalisha faida mfano kujenga nyumba za kupangisha , kujenga guest house na kununua mashamba . ila kikubwa zaid jitahid uchunguzee wewe mwenyewe kama imekosewa basi itakuwa bahat yako

Kumbuka imeingia kimakosa, Bank siku likibuma watatrace na kumtafuta muhusika, unapoamua kuchukua hela kama hiyo tegemea baadae umeshajitaarishia kitu katika maisha na unakitegemea sana kikachukuliwa na kuuzwa kufidia hiyo pesa. Ila kama utatumia kuizalishia na kuirudishia hapo ukala faida yaweza kuwa ni dili.
 
jilie tu hiyo pesa!,toa nunua kajumba ka milioni 60,hiyo kumi tafuna ,likija kuwaka unawaambia OK ni kweli and no way out I have to sell my asset and pay! inauza kamjengo tena huenda kakawa kameshapanda na thamani / unapeta mwanawane!!!
usiibonye tu we! /
 
Mwenye upele Hana ukucha...
Unasali kwa kakobe au Mzee wa upako, maana unaonekana mlokole Sana...!!!
 
Hapo ndugu usiguse hata mia,nenda bank report kuwa kuna muamala huulewi umetokea wapi.Kama kuna mtu/institution ilikuwekea watacomfirm nao ila kama wamekosea wata reverse hiyo transaction.Ukiitumia cku ikibainika itakula kwako,watakutupia money laundring case afu iwe shida.
 
Chai yako hebu ngoja kwanza Mkuu. Sukari bado inshu kitaa.

Stop selling smokes!

-Kaveli-
 
Huyu Jamaa atakuwa tapeli Tu, kwa usawa huu wa Magu huwezi kupata muda wa kuja kuposti ishu kama hiyo JF. Wajinga ndiyo waliwao
Mkuu nakubaliana na ww jamaa ana ongopa hv kuna waza mala.mbilimbili.hapo wkt pesa nmewekewa

Km.n.kweli.jamaaa anamatatizo basi..nngetoa zoote
 
Tafuta "Mangi" uende nae athibitishe kama ni kweli zipo halafu atakushauri. Inaonekana wewe ni Mmakonde hujui hela!
 
Stori ya mama mmoja,,,
Jamaa alikua akiendesha pikipiki kwa kasi kubwa, ghafla kufika kwenye kona flan ivi amaizing akapunguza mwendo.
Hapo ndo alipodondosha kibegi kilichokua kimejaa mifedha, huyo mama hakua mbali na barabara, alipata nafasi ya kuona lile begi la fedha, na moja nyekundu ilipeperuka hapo ndipo alijua lilikua begi la fegha.
Yule mama kwa ukarimu wake, alitupilia mbali shida zake na kumwita kwa sauti kubwa yule jamaa mwenye pikipiki alodondosha lile begi.
Hamad, yule jamaa kwakua alikua kwenye kona na alikua kapunguza spidi, alimsikia yule mama akimwita kwa nguvu. "we baba" "we baba" jamaa alikata kona na kurudi pale alipokua yule mama, alipofika yule mama akamwambia, "mzee umedondosha begi lako" jamaa alichukua lile begi, baada ya hapo ALIMPIGA kibao cha maana yule mama,kisha akamwambia "utakufa maskini".
 
ACHA UPUMBAVE TAKE ALL MONEY AND RUN AWAY HUKU UNASIKILIZIA MAANA PESA NYNGNE NI ZAKIFISADI VIONGOZI WANAOGOPA KUTUMBULIWA WANAZITUPIA KWENYE AKAUNTI NYNGNE KUEPUKA MSARA
 
Ni wafanyakazi wa Benki,wanaiba pesa kutoka domant account na kukuwekea. Wa najua zipo kwenye hio account ,wanatafuta Namna ya kuzikipua. Kuwa makini usishiriki.
 
Hii ina walakini japo inaweza kutokea pia.
Incidency kama hii hutokea kwa inter account cash transferring hasa kwa corporate accounts.
Mathalani a/c kama ya TRA kila mwisho wa mwezi kampuni nyingi hudeposit cheque nyingi sana hivyo ikitokea teller akakosea kupost a/c na validator wa cheque akashindwa kudetect hiyo mis-posting basi lazima hiyo hela ireflect kwenye akaunti iliyokesewa mpaka pale TRA au depositor wa hiyo cheque watakapofanya reconciliation baada ya kuchukua bank statement.
Mleta mada ni kosa kutumia hiyo hela.
 
Back
Top Bottom