Tupeane mbinu za ku-save: Unaweza kurudi na posho za kazi za field nyumbani?

Liverpool VPN

JF-Expert Member
Aug 29, 2020
5,839
13,094
Introduction
Haya matokeo ya Mpira yameniuma balaa. Liverpool kapigwa. Yanga holaaaaa. Tuachane na hilo, turudi kwenye mada.

Scenario
Ngoja niongee kwa mifano halisi ili uweze kunielewa. Mimi kwa mwaka huu tu nimepata kazi nyingi sanaa za field ila jana niliangalia account nakuta kuna 500k na elfu nane tu. Sijui hela zimeenda wapi. Dah Ujana nomaaaa.

1. Safari ya Dom
Mwezi wa pili mwishoni nilipata safari ya kwenda kwenye kikao kimoja hivi cha shirika la wazungu. Shirika hilo kwa kushirikiana na Wizara inayonihusu (idara yangu) walituita Dom. Tulikaa siku 5 (Juma3 mpaka ijumaa).
Ila Dom niliondoka jumapili nikiwa sijui na hela ya chai tu. Sasa najiuliza nani kamaliza hela zangu.
Ni ile guest niliyolala pale makole, ni ile bar ya Shangwe, Rainbow pale au Bambalaga? HATA SIJUI!

2. Kazini
Narudi kazini nikakuta zoezi la kwenda kukusanya mapato mtaani. Namsikia kiongozi fulani "Lazima uende wewe ni kijana mmoja wapo tegemeo la timu ya mapato". Tukapewa posho yetu fullll, sasa kwa level ya mshahara wangu (miaka 13 kazini) nikapewa posho nzuri tu (usisahau hapo nimetoka Dom Juzi yake).
Kazi ikaanza juma5 jioni. Kufika jumapili tunaambiwa turudishe gari ofisini maana kuna ugeni mkubwaa unakuja na hilo gari ni muhimu kwenye huo msafara. Tukarudi, sasa sijui hela hata ziliishia wapi ile posho?

3. Mkoani kikao
Juma 5 ya wiki nyengine naambiwa mkoani kuna kikao hivyo natakiwa kuwepo kutoka halmashauri yangu.
Basi bwana alhamisi nikatimba na Inumaa kikao kikaisha na nikalipwa. Ila bana, kutoka mkoani mpaka home ni masaa 2 tu, Ila huwezi amini gheto nilirudi jumapili usiku. Jumamosi na Jumapili sijui nilikuwa nafanya nini kule mjini.

4. Mbeya
Tokea juma5 iliyopita nipo Mbeya. Na hii kazi iliyonileta ni ya siku 23. Hivyo nipo Sanaa Mbeya. Kuna Wizara china ya Taasisi yake imetuita. Sasa bana, jana nimekaa John liquor palee (mbele ya Ilembo jirani na Mbeya pazuri), nilifika na na Msimbazi tu, nikacheki game ya Liverpool #YNWA. Nikaona "ngoja nichukue boda niwahi Kabwe nika-draw kwenye ATM halafu nikaangalizie Mpira wa Team yangu (YANGA) Mbeya pazuri"

Sasa kufika ATM, kuna sauti ikaniambia "hebu angalia kwanza salio" Mamaaaaaaa ile kucheki naona nina 500k tuu na kaelfu nane. Nikarudi, Mbeya pazuri na mawazo yangu "Posho yoteee niliyolipwa miezi hii miwili IKO WAPII? Mbeya pazuri penyewe palikua pachunguu maana Mzize kakosa Sanaa magoli.

Problem
Kuna jini limekula hela yangu au pesa za per-diem sio za kujengea au ndio...

Big Problem
Hapo usisahau hizo hapo juu ni posho za safari tu. Bado kuna posho za:
1. Vikao
Kama vi 5 au 6 hivi nilihudhuria na kusaini hii miezi miwili.
2. Extra duty
Mimi bwana ikifika tu saa 15:31 nataka unilipe, huwezi basi acha niende home. Mwisho wa kazi ni 15:30.
3. Kuna zile unakuta, hujui kitu Mara mwana aliandika jina lako kwenye activity fulani hivi kisa anakuelewa au ulimshauri vizuri kazi yake ikaenda, unalamba posho.
4. Kuna zile "Asante afisa, kutoka kwa mteja"

Conclusion
Hivi nani anakula hela za vijana?

Anyway maisha ndio hayahaya, STAREHE MUHIMU na KUJIPA RAHA LAZIMA. Maisha yenyewe Mafupi.

#Yanga Bingwa
#YNWA
 
Inabidi uwe na laini ya simu ya kibabe ya kuwekea hela zako zinazoingia bila mfumo rasmi tofauti na mshahara!!

Unapopata fedha zimeingaia Kwa akaunti unacheki Kwa mobile halafu unaziingiza kwenye laini yako ya kibabe!!

Yaani kama imeingia 500000/= unarusha 200000/=kwenye laini Yako ya kibabe!hasa ya tgo au Airtel!halafu hizo zilizobaki ndio zako nenda kafanye vurugu zote!!

Zile zilizopo kwenye lain ya kibabe unaziacha mle Kwa malengo ya baadae !!

Savings inaanza hata 5000/= siyo lazima uwe na mamilioni!!

Zile za mshahara unapigianbajeti zako kile kinachobaki rusha kwenye laini ya kibabe!!

Nimejaribu hiyo naona ipo vizuri kibubu kinakua!!

LAINI.YA KIBABE KWELI KWELI!! CHUKUA HIYO!!
 
Save kwanza ndio uanze matumizi mkuu. Kwa mfano ukipewa 2M ya safari ya siku 5. Weka 500k kwenye fixed account iliyobaki tumbua yote.

Usitumie ukitegemea utasave kitakachobaki.
 
Binafsi naona risk sana kiweka fedha nyingi kwenye line ya simu. Likitokea la kutokea, hiyo fedha itakua zawadi kwa mtandao husika. Kuna dogo dada yake alifariki akiacha line ya simu ina fedha ya kutosha, hakuwahi kuipata. Bank inafaa zaidi...
 
Inabidi uwe na laini ya simu ya kibabe ya kuwekea hela zako zinazoingia bila mfumo rasmi tofauti na mshahara!!

Unapopata fedha zimeingaia Kwa akaunti unacheki Kwa mobile halafu unaziingiza kwenye laini yako ya kibabe!!

Yaani kama imeingia 500000/= unarusha 200000/=kwenye laini Yako ya kibabe!hasa ya tgo au Airtel!halafu hizo zilizobaki ndio zako nenda kafanye vurugu zote!!

Zile zilizopo kwenye lain ya kibabe unaziacha mle Kwa malengo ya baadae !!

Savings inaanza hata 5000/= siyo lazima uwe na mamilioni!!

Zile za mshahara unapigianbajeti zako kile kinachobaki rusha kwenye laini ya kibabe!!

Nimejaribu hiyo naona ipo vizuri kibubu kinakua!!

LAINI.YA KIBABE KWELI KWELI!! CHUKUA HIYO!!
Asante mkuu kwa ushauri.
 
Mtoa mada umeshaonesha tatizo ulilonalo kupitia paragraph ya 2 na hiyo ya 4.

Kwa kifupi fedha yako inapotelea kwenye Starehe.

Umetaja hapo Rainbow,Bambalaga, John Liquor na Mbeya Pazuri.

Sasa hatuna Uhakika huko Viwanja vya Starehe unakunywa Pekeyako ama ndiyo wale Wakiingia Baa wanamwambia waiter "Mpe Kila mtu humu anachokunywa alafu Bill Juu yangu"

Ama ndiyo wale ambao wakiingia Baa wanamwambia Waiter "Nipangie Creti za bia kulingana na Urefu wangu"

Ama ndiyo wale ambao hawawezi Kulala peke yao hadi waondoke na wale Malaya ya Baa

Najua utakuwa umeshajua wapi ilipo weakness yako.

Hujachelewa, Fanya maamuzi sasa.
 
Introduction
Haya matokeo ya Mpira yameniuma balaa. Liverpool kapigwa. Yanga holaaaaa. Tuachane na hilo, turudi kwenye mada.

Scenario
Ngoja niongee kwa mifano halisi ili uweze kunielewa. Mimi kwa mwaka huu tu nimepata kazi nyingi sanaa za field ila jana niliangalia account nakuta kuna 500k na elfu nane tu. Sijui hela zimeenda wapi. Dah Ujana nomaaaa.

1. Safari ya Dom
Mwezi wa pili mwishoni nilipata safari ya kwenda kwenye kikao kimoja hivi cha shirika la wazungu. Shirika hilo kwa kushirikiana na Wizara inayonihusu (idara yangu) walituita Dom. Tulikaa siku 5 (Juma3 mpaka ijumaa).
Ila Dom niliondoka jumapili nikiwa sijui na hela ya chai tu. Sasa najiuliza nani kamaliza hela zangu.
Ni ile guest niliyolala pale makole, ni ile bar ya Shangwe, Rainbow pale au Bambalaga? HATA SIJUI!

2. Kazini
Narudi kazini nikakuta zoezi la kwenda kukusanya mapato mtaani. Namsikia kiongozi fulani "Lazima uende wewe ni kijana mmoja wapo tegemeo la timu ya mapato". Tukapewa posho yetu fullll, sasa kwa level ya mshahara wangu (miaka 13 kazini) nikapewa posho nzuri tu (usisahau hapo nimetoka Dom Juzi yake).
Kazi ikaanza juma5 jioni. Kufika jumapili tunaambiwa turudishe gari ofisini maana kuna ugeni mkubwaa unakuja na hilo gari ni muhimu kwenye huo msafara. Tukarudi, sasa sijui hela hata ziliishia wapi ile posho?

3. Mkoani kikao
Juma 5 ya wiki nyengine naambiwa mkoani kuna kikao hivyo natakiwa kuwepo kutoka halmashauri yangu.
Basi bwana alhamisi nikatimba na Inumaa kikao kikaisha na nikalipwa. Ila bana, kutoka mkoani mpaka home ni masaa 2 tu, Ila huwezi amini gheto nilirudi jumapili usiku. Jumamosi na Jumapili sijui nilikuwa nafanya nini kule mjini.

4. Mbeya
Tokea juma5 iliyopita nipo Mbeya. Na hii kazi iliyonileta ni ya siku 23. Hivyo nipo Sanaa Mbeya. Kuna Wizara china ya Taasisi yake imetuita. Sasa bana, jana nimekaa John liquor palee (mbele ya Ilembo jirani na Mbeya pazuri), nilifika na na Msimbazi tu, nikacheki game ya Liverpool #YNWA. Nikaona "ngoja nichukue boda niwahi Kabwe nika-draw kwenye ATM halafu nikaangalizie Mpira wa Team yangu (YANGA) Mbeya pazuri"

Sasa kufika ATM, kuna sauti ikaniambia "hebu angalia kwanza salio" Mamaaaaaaa ile kucheki naona nina 500k tuu na kaelfu nane. Nikarudi, Mbeya pazuri na mawazo yangu "Posho yoteee niliyolipwa miezi hii miwili IKO WAPII? Mbeya pazuri penyewe palikua pachunguu maana Mzize kakosa Sanaa magoli.

Problem
Kuna jini limekula hela yangu au pesa za per-diem sio za kujengea au ndio...

Big Problem
Hapo usisahau hizo hapo juu ni posho za safari tu. Bado kuna posho za:
1. Vikao
Kama vi 5 au 6 hivi nilihudhuria na kusaini hii miezi miwili.
2. Extra duty
Mimi bwana ikifika tu saa 15:31 nataka unilipe, huwezi basi acha niende home. Mwisho wa kazi ni 15:30.
3. Kuna zile unakuta, hujui kitu Mara mwana aliandika jina lako kwenye activity fulani hivi kisa anakuelewa au ulimshauri vizuri kazi yake ikaenda, unalamba posho.
4. Kuna zile "Asante afisa, kutoka kwa mteja"

Conclusion
Hivi nani anakula hela za vijana?

Anyway maisha ndio hayahaya, STAREHE MUHIMU na KUJIPA RAHA LAZIMA. Maisha yenyewe Mafupi.

#Yanga Bingwa
#YNWA
Hakuna mchawi au jini anayekula hizo pesa, unakula wewe.

Huwezi kufanya starehe ulizotaja bila kutumia pesa

Umepata bahati ya kula viperdiem ila unaichezea sana.

Hata hivyo hilo ni jasho lako hatuwezi kukupangia.
 
Msaidieni na huyu mwamba anafanya kazi kwenye kiwanda fulani,kwa siku analipwa 4500
Kwenye hiyo hela kula na nauli hapo hapo!
Mpeni mbinu namna ya kusave

Ova
 
Hakuna mchawi au jini anayekula hizo pesa, unakula wewe.

Huwezi kufanya starehe ulizotaja bila kutumia pesa

Umepata bahati ya kula viperdiem ila unaichezea sana.

Hata hivyo hilo ni jasho lako hatuwezi kukupangia.
""viperdiem""
Umetisha mtumishi mwenye mijiperdiem

Mungu akuongoze.

#YNWA
 
Back
Top Bottom