Nimekuta Milioni 20 imewekwa kimakosa kwenye akaunti yangu

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Habarini wakuu!

Juzi usiku February 17, 2023 nilicheck balance kwenye akaunti yangu ya benki (Jina limehifadhiwa), nikakuta Milioni 20. Nilirudia kutizama balance mara 15 ni kweli hela ikawa imo.

Sikuamini macho yangu, nikapita bodaboda hadi kwenye ATM iliyopo jirani na ninapoishi, ni kweli hela ipo.

Nilikuwa simdai mtu yeyote wala taasisi yeyote.

Mara ya mwisho akaunti yangu kuwa na hela nyingi (Milion 2) ni 2015 au 2016.

Maamuzi niliyoyachukua ni kuanza kuhamisha hiyo hela kwa kutumia App, kutoa hela kwenye ATM na kwa Wakala. Sikuingia ndani benki kuichukua.

Hadi leo tarehe 19 February, imebaki shilingi 250,000 tu kwenye akaunti, zote nimevuta.

Liwalo na liwe. Hiyo benki hawataniona tena. Nimevunja na ATM Card.

Swali langu, je hiyo hela itakuwa benki ndo walikosea wakaihamisha?

Matukio kama haya huwa yapo? Maana mm sikutaka hata kuingia ndani benki kuchukua statement jana 18/2/2022.


UPDATES - 20 FEBR

Benki wamenipigia cm niende tawini kwao. Natafuta mwanasheria mzuri niende. Naombeni mawazo pia ndugu zangu.

Nina 5m tu Cash.

Tulianza pamoja, tumalize pamoja.
 
Mkuu Hongera sana mimi mwenyewe mwezi wa 12 nilitumiwa ml 4.5 kwenye no yangu ya Airtel money na nikaitoa na kuitumia cha ajabu hadi leo sijaulizwa na yoyote na Maisha yanasonga ushauli wangu na hicho kiasi kilichobaki benk kichukue hiyo ni Bahati yako mkuu
 
Hujatumia akili hata kidogo. Hiyo Hela utailipa na inaweza kukusumbua.. Mara kadhaa wafanyakazi wa bank hufanya makosa kama hayo. Ila Kaa ukijua wakifanya reconciliation lazima watagundua tu.

Maana kama umewekewe kimakosa Ina maana kuna mtu alipaswa kuwekewa kwa makosa ukawekewa wewe.

Bora ungeripoti na wairejeshe, kumbuka ulipofungua account taarifa zako zote uliwapatia.
 
Mkuu Hongera sana mimi mwenyewe mwezi wa 12 nilitumiwa ml 4.5 kwenye no yangu ya Airtel money na nikaitoa na kuitumia cha ajabu hadi leo sijaulizwa na yoyote na Maisha yanasonga ushauli wangu na hicho kiasi kilichobaki benk kichukue hiyo ni Bahati yako mkuu
Bado wanatrec your location kupitia taarifa zako za Nida. Wakikumanya tu ukwishile
 
Hujatumia akili hata kidogo.hiyo Hela utailipa na inaweza kukusumbua..Mara kadhaa wafanyakazi wa bank hufanya makosa kama hayo.Ila Kaa ukijua wakifanya reconciliation lazima watagundua tu.maana kama umewekewe kimakosa Ina maana kuna mtu alipaswa kuwekewa kwa makosa ukawekewa wewe.
Bora ungeripoti na wairejeshe.kumbuka ulipofungua account taarifa zako zote uliwapatia
Wewe ulitaka afanyeje, Hana uwezo kukamata 20m ya pamoja, na hata angetaka mkopo wenda ni ngumu kupata, chukua hela fanyia kazi zako, hilo swala kulipa ni lingine, ila vyako vimefanyika, Wamekosea kuweka, nimekosea kuchukua sote tumekosea.
 
Ukiwa unaweka milioni 2 kila mwezi na ghafla ikaingia milioni 20 kwenye akaunti bila maelezo maalumu ni lazima benki izuie hiyo fedha na kukuita kufanya mahojiano. Huu ndiyo utaratibu ambao mimi naufahamu, na nimeshawahi kukutana nao siyo mara moja. Nadhani hii geresha na changamsha genge kama geresha zingine tu....
 
Mwaka Jana mwezi wa Saba niliona milioni 4 kwenye account ya Airtel nikipigiwa simu na muhusika nikakiri nikamwambia apige simu makao makuu wairudishe kweli akafanya hivyo, wiki moja baadae nilipokea kiasi Cha laki tatu na hamsini toka namba ile akiwa ananishukuru kwa moyo wangu mzuri na akahitaji tuonane lakini nilimpiga chenga kwani sikuona ulazima wowote ila alishukuru sana.

My take,

Kwenye maisha hakuna cha bahati wala ngekewa zaidi ya mapambano hivyo msizoee urahisi, shauri zenu
 
Mnakumbuka ile ESCROW, watu walipokea pesa kwenye account zao hawajui zimetoka wapi mwishwo wa siku wakasota mahakamani kama wahujumu uchumi.

Jaribu kuangalia bank statement yako iyo transaction imetoka wapi, usije ukabebeswa mzigo wa pre bargain. Maana saivi wanatafuta mafisadi wapya kwenye hii game ya pre bargain usije ukaozea jela au kwa DPP

Au hii ni CHAI umeamua kuchangamsha genge???
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom