Nimekuta 74,549,940.36 kwenye account yangu

gango2

JF-Expert Member
Aug 31, 2011
1,941
2,256
Naombeni msaada tafadhari!

Mauza uza haya nilianza kuyaona mwezi wa nne nilipokuwa nataka kusafiri kwenya Italia, kwa kuwa card yangu ya CRDB ilikuwa ni Tembo card na siku renew niliamua kwenda kuactivate account yangu ya STANDARD CHARTERD bank ambayo awali ilikuwa na deni la kama -63700. nilifanya hivi makusudi ili nipate card mpya (credit card) ntakayotumia Italia

Nilipofika benk nilijaza kwanza form ya kuangalia salio na kumpatia CASHIER ambapo aliangalia balance akajaza akanirudishia nikakuta 765,000 nikashtuka kidogo, afu nikataka kuuliza nikaona ngoja niuchune, nikaaa pale benk nikiwaza baadae nikaondoka zangu. kwa kuwa nilikuwa na hela sikudeal nayo sana ile hela. baada ya kama wiki nikaona nikacheck tena salio nikakuta 735000 nikaona nitoe 50000 kutest na kweli zikatoka nikatulia. nikasafiri zangu

Sasa juzi tar 02 nikasema ngoja niende ATM nikaangalie kama ile hela ipo, ile kuomba balance kwa ATM nikaona imenitolea karatasi inaonyesha salio 74,549,940.36, nikachanganyikiwa! sikutoa hata shilingi nikaogopa. leo tena nimeenda pale mikocheni nimeangalia salio nimelikuta hilo hilo duu nimechanganyikiwa na naogopa hebu nisaidieni nifanye nini na hizi hela

Niende police?
Nikariport bank?
Niuchune nitumie?
 
Kumbuka hata Siku moja pesa benk huwa haipotei. Kama ni ya benk wamekosea wakiamua kuitrace lazima watajui ilipo

Ni vema labda uombe bank statement llil kujua ni wapi ilipotokea mkuu ili uwe na amani

duu hapa nimeshindwa nifanye nini ndugu yangu! naona bora nikae kimya kama sijaziona hata upite mwaka mzima, milion 70 mkuu?? nikariport
 
Hizo pesa usitoe wala kufanya jambo lolote ila jaribu kumuuliza kwa meneja kuchek hiyo pesa imeingizwa lini( jifanye kuna mtu alisema atatuma pesa ili uweze kujua inatokea wap hiyo pesa ) na usiongee kwa mtu kwanza ili ufanye uchunguz wako . pia jambo la Pili inategemea kaz zako unazofanya inaweza ikawa unawekewa mtego ili kupate skendo au ufungwe kwa tuhuma za rushwa kikubwa hiyo pesa usitoe taarifa . fumba macho kama haipo vile kipind unaendelea na uchunguz wako ukiona zipo sawa mkuu tumia kwa kujengea nyumba au mradi wenye kuzalisha faida mfano kujenga nyumba za kupangisha , kujenga guest house na kununua mashamba . ila kikubwa zaid jitahid uchunguzee wewe mwenyewe kama imekosewa basi itakuwa bahat yako
 
Hapo kuna mambo hayajakaa sawa. Money laundering inahusika hapo. Ingekua kweli ungekua umeshatafutwa na watu wa benk wakuulize iweje hela ingiie nyingi kwenye account yako wakati huna history ya kuweka kiasi kikubwa cha hela. Pia uulizwe umezipata wapi.
 
Hizo ni hela za Simba sport club, huenda zimewekwa hapo kwa muda kukwepa kodi/ Takukuru, kwahiyo kama ni mwanachama wao ziache tu, kama wee ni Yanga zile zote, hata wakikukamata watajua unatania kwa kuwa wewe ni mtan wao ..!!

CC Aveva ...!!
Mgao wa Emanuel Okwi!
 
Back
Top Bottom