Katavi
Platinum Member
- Aug 31, 2009
- 41,983
- 12,702
Kwa hiyo inaweza ikawa ametunga hiki kisa??Ikiwa umeweza kumdanganya mkeo kwanini nisishindwe kukiamini hiki kisa chako ambacho hakiingii akilini?
Kwa hiyo inaweza ikawa ametunga hiki kisa??Ikiwa umeweza kumdanganya mkeo kwanini nisishindwe kukiamini hiki kisa chako ambacho hakiingii akilini?
Inamaana hii kitu hapa kwenye jiko ni"dogi"au?!nimeshakula sana mishikaki yake...walioishi CHINA wanajua hili huku tunaita "gourouchuan"
Kwa hiyo inaweza ikawa ametunga hiki kisa??
iwe fundisho kwa wasio na heshima kwa wake zaoLeo kwenye hangaika zangu za kutwa nzima nikaamua nirudi nyumbani. Mama watoto hakutaka nitoke hivyo basi akaniambia mechi ya Brazil Vs Mexico niiangalizie nyumbani. Nikakaa nyumbani nikiangalia mechi mwenyewe kama jini Njabagumu. Katikati ya mpira nikaona siinjoi chochote, nikaaga kuwa naenda kununua vocha dukani. Nikaingia taratibi baa ya jirani, nikaagiza Serengeti moja baridi sana, nikaipiga fasta kama mwanariadha aliyetoka kumaliza marathon akutanapo na jagi la maji. Haikunitosha niaagiza ya pili, kabla haijaja mara ghafla mama watoto akapiga simu "vp darling mbona unakawia?" ndio lililokua swali lake, nikamjibu niko na mwenyekiti wa mtaa tuna mazungumzo. Nikaagiza mbuzi, daima huwa napenda jembe (wataalam wa mbuzi wanaelewa ninachokiongea). Baada ya nusu saa ikawa mezani. Nikapiga kama vipande kumi, nikaagiza Serengeti nyingine ya baridi. Nikiwa katikati ya zoezi la pombe nyama, mara wakaingia Polisi wakiwa na sare zao na kuelekea jikoni. Huko wakawaweka chini ya ulinzi watumishi wote na kufanya msako mkali. Jikoni vimekamatwa vichwa viwili vya mbwa na ngozi mbili. Na t ayari mie nsha kula huyu kiumbe mlinzi jamani. KUlia nataka, kucheka nataka, najitapisha sitapiki. Kuweni makini wenzangu, yasije kuwakuta yaliyonikuta.
Kwani dar ndio wanaukulaka"ulinzi shirikishi"huko lazima ni dar
Mmmh! Mkuu hujamtafuna huyo mbuzi kucha kweli?? Lol!Kalenga iringa wanagonga sana hii kitu,mbona hawafi?
Mc Tilly Chizenga wee! Shauri yako utajajikuta unakula mbwa kwa kutamani-tamani hivyo!
dah....mbwa huyu huyu ninayemjua.....kudadeki wallah......
Inamaana hii kitu hapa kwenye jiko ni"dogi"au?!
pamoja,my id is my real name,mc nimeongezea kwa vile mimi ni mc ktk sherehe,niko pande za arusha,hata pande za facebook natumia same id!
nawe pia id yako iko familiar mno na mimi.....natumia sana lily flowers kupambia!mimi ni mpambaji pia
Leo kwenye hangaika zangu za kutwa nzima nikaamua nirudi nyumbani.
Mama watoto hakutaka nitoke hivyo basi akaniambia mechi ya Brazil Vs Mexico niiangalizie nyumbani.
Nikakaa nyumbani nikiangalia mechi mwenyewe kama jini Njabagumu.
Katikati ya mpira nikaona siinjoi chochote, nikaaga kuwa naenda kununua vocha dukani.
Nikaingia taratibi baa ya jirani, nikaagiza Serengeti moja baridi sana, nikaipiga fasta kama mwanariadha aliyetoka kumaliza marathon akutanapo na jagi la maji. Haikunitosha niaagiza ya pili, kabla haijaja mara ghafla mama watoto akapiga simu "vp darling mbona unakawia?" ndio lililokua swali lake, nikamjibu niko na mwenyekiti wa mtaa tuna mazungumzo.
Nikaagiza mbuzi, daima huwa napenda jembe (wataalam wa mbuzi wanaelewa ninachokiongea). Baada ya nusu saa ikawa mezani.
Nikapiga kama vipande kumi, nikaagiza Serengeti nyingine ya baridi.
Nikiwa katikati ya zoezi la pombe nyama, mara wakaingia Polisi wakiwa na sare zao na kuelekea jikoni.
Huko wakawaweka chini ya ulinzi watumishi wote na kufanya msako mkali. Jikoni vimekamatwa vichwa viwili vya mbwa na ngozi mbili.
Na t ayari mie nsha kula huyu kiumbe mlinzi jamani.
KUlia nataka, kucheka nataka, najitapisha sitapiki.
Kuweni makini wenzangu, yasije kuwakuta yaliyonikuta.
Sawa kabisa I was on the right route, nimepitia phone book yangu na namba yako pia ninayo (kama utakuwa hujabadilisha) tutatafutana kwenye mashuguli then.
Ulevi kumbe haufai...mwaweza kula watu wenzenu.Wakati mwingine taste za nyama hazitofautiani tena ukiwa na kilevi kichwani.
Na nguruwe je ? mbona Biblia inasema kuwa "Nguruwe ni najisi kwenu.
Msiile nyama yao, wala msiiguse mizoga yao" ?
Biblia inasema hivi,
"Na nguruwe, kwa sababu yeye anazo kwato, ni mwenye miguu iliyopasuka kati, lakini hacheui, yeye ni najisi kwenu.
Msiile nyama yao, wala msiiguse mizoga yao; hao ni najisi kwenu." (Mambo ya Walawi 11:07-08)
Kachome sindano ya kichaa cha mbwa,