Siridhishwi na jinsi Serikali inavyoshughulika na sakata la uchafuzi na sumu katika maji ya Mto Mara

Apr 24, 2011
29
542
Ziwa Victoria, eneo la katikati ya Musoma na Kinesi, hapa ndipo unapopita mkondo wa Mto Mara, unaoingiza maji yake Ziwa Victoria. Ukiwa eneo hilo, unaweza kuona maji yalivyobadilika rangi na yamekuwa rangi nyeusi, sasa siyo lazima uekeke daraja la Kirumi, ili kuthibitisha hilo. Ni hatari. Nitaeleza baadhi ya mambo kwa kifupi sana.

Mto Mara unatiririsha maji yake kutoa katika milima ya Mau iliyopo nchini Kenya na baadaye kuingia Tanzania kuanzia katika Wilaya za Serengeti, kuingia wilaya ya Tarime, unakatiza katika wilaya ya Butiama na Wilaya Rorya kabla ya kuingiza maji yake katika Ziwa Victoria.

Kirumi, Ryamisanga, Kitasakwa (Butiama), Kwibuse, Kwibwe, Bisarwi, Kuruya (Rorya), Nyabichume, Matongo, Nyamongo, Bisarwi, Mrito (Tarime) ni sehemu ambazo zinatumia maji ya mto Mara na kwa namna moja ama nyingine vimeathirika kwa maji hayo kuchafuliwa kwa utando huo wa mafuta.

Mto Mara umezungukwa na wakazi mbalimbali katika vijiji hivyo nivyotaja ambao wanajihusisha na shughuli za kibinadamu za uzalishaji mali zikiwepo ukulima, uvuvi, ufugaji mifugo, na shughuli za uchimbaji madini (migodi). Tatizo hili ambalo leo limeundiwa kamati siyo Mara ya kwanza

Kamati aliyounda Waziri chini ya Mwenyekiti wake Profesa Samuel Manyele kutupia tuhuma kuwepo kwa kiwango kikubwa cha kinyesi cha mifugo mtoni pamoja na uozo wa mimea ndani ya mto hasa mimea vamizi kama vile magugu maji na matete na kwamba mgodi wa dhahabu wa Barrick North Mara

Profesa Samuel Manyele anasema wamebaini uwepo wa kinyesi cha ng'ombe zaidi ya tani 1.8 milioni na mkojo wa ng'ombe lita 1.5 bilioni uchafu uliotokana na kuwepo kwa ng'ombe zaidi ya laki 3 katika eneo oevu la mto Mara kwa kipindi cha miezi minane mwaka 2021 wakati wa kiangazi.

Kwamba mgodi hauhusiki na uchafuzi huo ni upotoshaji na wakazi wa Mkoa wa Mara hatukubaliani nao. Tunaikataa taarifa hii ya 'kamati ya michongo' na itakuwa siyo mara ya kwanza, tumewahi kukataa taarifa ya hovyo ya kamati aliyounda Profesa Sospeter Muhongo, huko Nyamongo.

Wananchi wanaoishi kuzunguka mgodi wa dhahabu wa Barrick North Mara gold mine, Nyamongo, Tarime, Mara, Mwaka 2016 waligoma kupokea matokeo yaliyotolewa na kamati ya Muhongo baada ya kamati kuthibisha maji yanayotiririka kutoka katika mgodi hayana madhara yoyote kwa viumbe hai

Prof Muhongo akachukua sampuli ya maji maeneo yanayotiliwa shaka, akaema kwa usimamizi wa kamati yake, sampuli zake atapewa Mbunge John Heche naye apeleke kuchunguzwa maabara yoyote ile ili naye apate majibu yake na zoezi kama hilo afanye Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Glorious Luoga.

Baada ya taarifa ya NEMC iliyosomwa na Peres Joshua kutoka makao makuu, Dar es Salaam, kukataliwa, wananchi wa eneo hilo walichukua sampuli ya maji hayo waliipeleka maabara ya Nairobi, Kenya na majibu yakatoka Machi 20, 2015 yaliyobaini kuwa yana sumu na hayafai kwa matumizi ya mifugo na binadamu.

Au litolewe agizo la kupimwa tena kwa maji yanayotoka katika vyanzo vinavyozunguka mgodi wa dhahabu wa Barrick North Mara ili kujiridhisha kuwa hayana athari kwa binadamu, mifugo na mazingira na kama yana viwango vinavyokubalika kwa matumizi ya binadamu, mifugo na mazingira

Viwango vinavyopaswa kutumika katika upimaji wa maji haya lazima viwe vya Shirika la Afya Duniani (WHO) hivyo zichukuliwe tena sampuli za maji wakati sahihi (kiangazi na masika, wataalam wanafahamu) na zipimwe tena na maabara huru. Sampuli hizo zigaiwe kwa makundi mbalimbali

Sampuli hizo, tuzipeleke katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo France, Germany na Belgium au pengine ambako kuna maabara za kisasa na zinazoaminika duniani. Siyo lazima kujifungia ndani na kulipana posho na kamati zisizokuwa na mantiki. Tuwasaidie wananchi siyo kuwaumiza.

Vyanzo vya maji katika sehemu nyingi zenye uchimbaji mkubwa na mdogo duniani vimekuwa vikiathiriwa na shughuli za migodi Mamlaka zinazosimamia Sekta ya Maji pamoja Mgodi ziwasiliane ili kupata chanzo mbadala cha maji na hivyo kuondoa malalamiko ya wananchi wanaozunguka mgodi huo.

Maji hayo ya Mto Mara yanayoua samaki hao yalibadilika na kuwa rangi nyeusi, juu kumetanda kitu mithili ya mafuta na yanatoa uvundo. Samaki wafu walianza kuonekana 8/3/2022 na wananchi wanaotumia maji ya mto Mara wakaanza kuwaokota na kuwapeleka sokoni kuwauza.

Pia, kwanini wataalam wa Wizara ya Nishati na Madini wasihakikishe kuwa kila baada ya miezi mitatu wanachukua sampuli za maji katika vyanzo vinavyozunguka mgodi huo na kuzipima ili kujiridhisha kuwa maji hayo hayana madhara kwa binadamu, mifugo na mazingira?

Tujadili hili la Mto Mara la hivi karibuni; Wavuvi waliokuwa katika shughuli zao, walikuta samaki wakielea mtoni, aina ya gogogo na sato. Na walippfikishwa sokoni au nyumbani, waliotumia, waliharisha sana na kutapika. Hali hiyo iliwakuta wakazi wa Bisarwi, Manga, Kirumi, Kembwi,

Wavuvi wakafikisha taarifa kwa uongozi wa vijiji hivyo kuwepo kwa maji yenye sumu, meusi kwa rangi, na kutanda kwa mafuta yakiashiria hatari kwa afya ya binadamu na wanyama na Mazingira yao. Viongozi wa vijiji wakachukua Jukumu la kutoa elimu kwa wanakijiji, wasiyatumie.

Hata Mbwa waliokula nyama za mifugo hiyo iliyokufa walidhurika. Binadamu waliokula samaki wanaotakana na maji hayo walipata madhara. Samaki wanaotokana na maji hayo wanapoteza ladha ua kawaida ya samaki na wanatoa harufu mbaya ya uvundo.

Lakini tayari watu wengine walishakula vyakula vinavyopatikana katika maji hayo ya mto Mara na kudhurika, ikiwepo nyama za mifugo yao iliyokunywa maji hayo na kufa pia samaki waliopatikana kutoka katika mto Mara. Ikabidi viongozi wa Kijiji wapeleke taarifa ngazi za Juu

Watu wa kwanza kutoka serikalini kufika eneo hilo ni kutoka wizara ya maji na wizara ya uvuvi, wakafika na boti zao, wakaingia mtoni, wakachukua sampuli za maji hayo, na samaki wakapeleka maabara kwa ajili ya kufanya utafiti na vipimo vya kisayansi.

Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria imeeleza wamebaini uwepo wa kiwango kikubwa cha mafuta kuliko kiwango kinachokubalika kwa mujibu wa viwango vya ubora maji Tanzania (TZs 2068:2017), na kukosekana kwa hewa ya Oksijeni kwenye maji ya mto Mara kupelekea samaki na viumbemaji kufa

Waziri wa nchi, Ofisi ya makamu wa Rais-Mazingira na Muungano, Seleman Jafo akaunda kamati yake maalum kuchunguza suala hilo chini ya Profesa Samuel Manyele, kamati ikaeleza, maji yalichafuka kutokana na mimea ya asili jnayozalisha sumu, kinyesi cha ng'ombe na mvua kutibua tope.

Pia viongozi wa vijiji kadhaa waliwasilisha Taarifa za mifugo yao kufa kutokana na kutumia maji ya mto Mara baada ya halo hiyo kuonekana. Katika Kipindi cha wiki mbili pekee, kitongoji cha Burongo, Kijiji cha Bisarwi kata ya Manga, Tarime kilipoteza ng'ombe 54 na mbuzi nane.

NB: Wakati Mamlaka ya Maji Vijijini (RUWASA) Ilipaswa kutafuta mbadala wa upatikanaji wa maji kwa wananchi waliopo kandokando ya Mto Mara wakati uchunguzi ukiwa unaendelea, lakini mmezuia wasitumie maji, lakini serikali haijatoa mbadala wake. Mnataka watumie njia gani?

#MMM, Martin Maranja Masese
 
Safi sana mtoa mada. nishaangacho ni kuwa hao wavuvi wamekuta samaki wakielea baharini wakiashilia kufa kwa nini waliwaokota na kuwapeleka sokoni? inaonesha hata walala hoi nao ni hatari kwa kusaka pesa kuliko kujali maisha ya wenzi wao.

SERIKALI IPIGE MARUFUKU SHUGHULI ZOTE ZA UVUVI NA MATUMIZI YA MAJI YA KUNYWA ZIWA MARA kwa miaka mitano. WE do not like a pill after death!!!!!!!
 
"Kinyesi cha ngombe tani 1.8 milion na mkojo lita 1.5 bilioni kwa miezi nane"

Bado nayatafakari majibu ya hiyo ripoti ya tume.
 
Mkuu, hujarudi Tarime? Maana ulikula Hela ya chama kwa kisingizio Cha kuripoti kesi ya Lissu, biashara ya misokoto upo nayo?
 
Tutafika mbinguni tukiwa tumechoka Sana.

Kumbe tayari majibu ya tatizo ulikuwa nayo kabla ya utafiti wa kisayansi?!

Kumbe tokea 2015 mgodi unamwaga SUMU kwenye MTO Mara?!

Kumbe sampuli ziliwahi KUCHUKILIWA na wenye Majibu Yao binafsi kupinga uchunguzi rasmi?

Kumbe ripoti unayoipenda ilisema MAJI hayafai Kwa matumizi ya binadamu na MIFUGO na baada ya hapo mlichimba visima vingapi?

Kwakuwa ripoti nzuri ni Ile itakayosema mgodi umemwaga sumu kwanini tusiungane tuufute huo mgodi?

MAJI kupekwa kupimwa ulaya ukiongezewa tozo unatoa macho hata hivyo vitu vingi vya Afrika ukipeleka kupata vipimo vya kiafya utaleta TAHARUKI KUANZIA Nyumba zetu,magari,nguo chakula NK.

Katika hili umedanganya kuhusu MIFUGO kufa hata Maeneo ya Bisarwi WANANCHI waliendelea na uvuvi kama kawaida Kwa siku zote na hakukuwa na tatizo.

Nchi hii tumejikita katika mihemko ambayo haina tija Kwa mawazo yako finyu unataka kuamisha umma kwamba hiyo kamati Ilikuwa na maslahi gani?
 
Safi sana mtoa mada. nishaangacho ni kuwa hao wavuvi wamekuta samaki wakielea baharini wakiashilia kufa kwa nini waliwaokota na kuwapeleka sokoni? inaonesha hata walala hoi nao ni hatari kwa kusaka pesa kuliko kujali maisha ya wenzi wao.

SERIKALI IPIGE MARUFUKU SHUGHULI ZOTE ZA UVUVI NA MATUMIZI YA MAJI YA KUNYWA ZIWA MARA kwa miaka mitano. WE do not like a pill after death!!!!!!!

Kupiga marufuku ni sahihi, watatumia mbadala upi kupata huduma ya maji?
 
Kuna viashiria vya rushwa katika hili sakata na ndio maana taarifa za kiuchunguzi haziaminiki.
 
Tatizo letu Watanzania tunapenda sana mizaha. Ifike mahali hawa wapuuzi wawe assassinated kwa maslahi ya taifa. Wakidunguliwa wachache wa mfano wengine watajifunza kuwa sisi siyo wajinga
 
Nadhani turudi katika ile report ya mto tighite tuanzie hapo sababu inawezekana ikawa factor mojawapo ya kuchafua maji ya mto mara.
 
Nilifikiri una elimu na unaamini sayansi kumbe zerro...rudi darasani ukasome hujachelewa bro
 
Kupiga marufuku ni sahihi, watatumia mbadala upi kupata huduma ya maj kama kuna bomba la wese na gesi toka Urusi mpaka Ulaya yote leo vipi sisi tushindwe kupeleka maji mara kwa njia za bomba.tunasubuli mfadhili? wafadhili wa siku hisi karibia wengi ni ma-adnan kashogi,karl Peter, je tutaweza? Tatizo ni kuwa waziri wa maji is treating this problem of mto mara as a" red herring"!
 
Back
Top Bottom