Nimekula NYAMA YA MBWA

mahmood, Mungu amefanya kazi na watu wengi na kwa namna nyingi. kabla ya walawi, alikuwepo adamu, na baadaye NUHU. NUHU aliambia kila mmea wa kondeni itakuwa mboga kwenu, na kila kitambaacho kilcho hai kitakuwa nyama/chakula chenu. hapo hajabagua nini cha kula na nini cha kuacha. Ukija kwa walawi, walawi walikuwa ni watu walioteuliwa na MUNGU kwa kazi maalum ya kulihudumia hekalu. sasa ili kuwatenga na jamii nyingine, walipewa sheria ya kutokula baadhi ya wanyama. Lakini sheria hiyo, haikuwahusu watu wengine. kwa mfano, wakati walawi walikuwa hawali, wayuda, wabenyamini, waisrael(yakobo) hawakukatazwa kutumia kitu hiyo ispokuwa walawi tu. sasa wewe mahmood, unakataa kula nguruwe, wewe ni mlawi? wewe ni msukuma, mnyamwezi, mha, mnyantuzu n.k hivyo sheria hiyo haikuhusu mkuu.

Wakristo kwa nini hamuishiki Biblia yenu au Biblia sio yenu ?

Biblia inakataza kula nguruwe lakini Nyie mnakula (na mnasema kula nguruwe ni halali!)..

Biblia inasema Mungu ni Mmoja tu lakini nyie mnasema Mungu ni watatu (Trinity).

Biblia inasema Yesu ni Mtu lakini nyie mnasema Yesu ni Mungu! .............................. ...........

Nashangaa sana! Wakristo mnafuata mafundisho ya nani ?

Biblia inasema,

"Na nguruwe, kwa sababu yeye anazo kwato, ni mwenye miguu iliyopasuka kati, lakini hacheui, yeye ni najisi kwenu.
Msiile nyama yao, wala msiiguse mizoga yao; hao ni najisi kwenu." (Mambo ya Walawi 11:07-08)

"Yesu akamjibu, Ya kwanza ndiyo hii, Sikia, Israeli, Mungu wetu ni Mungu mmoja." (Marko 12:29)

"wakufahamu wewe ambaye pekee ni Mungu wa kweli,nakumfahamu Yesu Kristo ambaye umemtuma." (Yohana17:3)

Yesu anasema: "Lakini sasa mnatafuta kuniua mimi mtu ambaye nimewaambia iliyo kweli, niliyoisikia kwa Mungu..." (Yohana 8:40)

Yesu pia anasema,

"Msidhani ya kuwa nimekuja kutengua sheria ya Musa au mafundisho ya Manabii, sikuja kutengua bali kukamilisha". (Mathayo 5:17)

"Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Hamna lenu jambo mpaka muishike Taurati na Injili na yote mlio teremshiwa kutokana na Mola wenu Mlezi. Na hakika ulio teremshiwa wewe kutokana na Mola wako Mlezi yatawazidishia wengi katika wao uasi na ukafiri. Basi usiwasikitikie watu makafiri." (Quran 5:68)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom