Nimekula NYAMA YA MBWA

nimeshakula sana mishikaki yake...walioishi CHINA wanajua hili huku tunaita "gourouchuan"

P200804211318089638308402.JPG
Inamaana hii kitu hapa kwenye jiko ni"dogi"au?!
 
Utakuwa umeaanza kula muda mrefu maana hukunote tofauti,
Inamaana radha ya mbuzi = to radha ya mbwa ?

Mh watakuwa wengi washakula haka kanyama
 
Leo kwenye hangaika zangu za kutwa nzima nikaamua nirudi nyumbani. Mama watoto hakutaka nitoke hivyo basi akaniambia mechi ya Brazil Vs Mexico niiangalizie nyumbani. Nikakaa nyumbani nikiangalia mechi mwenyewe kama jini Njabagumu. Katikati ya mpira nikaona siinjoi chochote, nikaaga kuwa naenda kununua vocha dukani. Nikaingia taratibi baa ya jirani, nikaagiza Serengeti moja baridi sana, nikaipiga fasta kama mwanariadha aliyetoka kumaliza marathon akutanapo na jagi la maji. Haikunitosha niaagiza ya pili, kabla haijaja mara ghafla mama watoto akapiga simu "vp darling mbona unakawia?" ndio lililokua swali lake, nikamjibu niko na mwenyekiti wa mtaa tuna mazungumzo. Nikaagiza mbuzi, daima huwa napenda jembe (wataalam wa mbuzi wanaelewa ninachokiongea). Baada ya nusu saa ikawa mezani. Nikapiga kama vipande kumi, nikaagiza Serengeti nyingine ya baridi. Nikiwa katikati ya zoezi la pombe nyama, mara wakaingia Polisi wakiwa na sare zao na kuelekea jikoni. Huko wakawaweka chini ya ulinzi watumishi wote na kufanya msako mkali. Jikoni vimekamatwa vichwa viwili vya mbwa na ngozi mbili. Na t ayari mie nsha kula huyu kiumbe mlinzi jamani. KUlia nataka, kucheka nataka, najitapisha sitapiki. Kuweni makini wenzangu, yasije kuwakuta yaliyonikuta.
iwe fundisho kwa wasio na heshima kwa wake zao
 
Mc Tilly Chizenga wee! Shauri yako utajajikuta unakula mbwa kwa kutamani-tamani hivyo!

mwaJ!iyo kitu mi nishakulaga sana iringa though bila mimi kujua!nilisoma mkwawa,kuna kina mama wanauzaga mbogamboga,msimu wa ulanzi nyama inakuwa nyingi sana sh 100 unajaziwa bakuli zima!kumbe wakati wa ulanzi mbwa huwa wanakunywa ukiwa umeanikwa wakati wa kutengenezwa,hivyo mbwa wengi hulewa na kugongwa sana na magari hivyo nyama ya mbwa inakuwa nyingi mtaani!

sasa mbwa wa kugongwa tu barabarani watamu vile itakuwa hao wa china ambayo ni mbegu ya kuliwa kabisa?mi nikifika china palepale airport naagiza gouruchuan!
 
Inamaana hii kitu hapa kwenye jiko ni"dogi"au?!

yup mkuu lakini hawa wapuuzi walivyo wajinga(wachina) ukiingia kichwa kichwa utaambiwa ni kondoo,kitimoto au ng'ombe...hii nyama ni tamu sana mkuu huwa inamwagiwa viungo mwanana "ziran"
 
pamoja,my id is my real name,mc nimeongezea kwa vile mimi ni mc ktk sherehe,niko pande za arusha,hata pande za facebook natumia same id!

nawe pia id yako iko familiar mno na mimi.....natumia sana lily flowers kupambia!mimi ni mpambaji pia

Sawa kabisa I was on the right route, nimepitia phone book yangu na namba yako pia ninayo (kama utakuwa hujabadilisha) tutatafutana kwenye mashuguli then.

 
Leo kwenye hangaika zangu za kutwa nzima nikaamua nirudi nyumbani.
Mama watoto hakutaka nitoke hivyo basi akaniambia mechi ya Brazil Vs Mexico niiangalizie nyumbani.
Nikakaa nyumbani nikiangalia mechi mwenyewe kama jini Njabagumu.
Katikati ya mpira nikaona siinjoi chochote, nikaaga kuwa naenda kununua vocha dukani.
Nikaingia taratibi baa ya jirani, nikaagiza Serengeti moja baridi sana, nikaipiga fasta kama mwanariadha aliyetoka kumaliza marathon akutanapo na jagi la maji. Haikunitosha niaagiza ya pili, kabla haijaja mara ghafla mama watoto akapiga simu "vp darling mbona unakawia?" ndio lililokua swali lake, nikamjibu niko na mwenyekiti wa mtaa tuna mazungumzo.
Nikaagiza mbuzi, daima huwa napenda jembe (wataalam wa mbuzi wanaelewa ninachokiongea). Baada ya nusu saa ikawa mezani.
Nikapiga kama vipande kumi, nikaagiza Serengeti nyingine ya baridi.
Nikiwa katikati ya zoezi la pombe nyama, mara wakaingia Polisi wakiwa na sare zao na kuelekea jikoni.
Huko wakawaweka chini ya ulinzi watumishi wote na kufanya msako mkali. Jikoni vimekamatwa vichwa viwili vya mbwa na ngozi mbili.
Na t ayari mie nsha kula huyu kiumbe mlinzi jamani.
KUlia nataka, kucheka nataka, najitapisha sitapiki.
Kuweni makini wenzangu, yasije kuwakuta yaliyonikuta.

Hahahahahhahahahahahh!!! nimecheka sana.... na ukome siku nyingine mkikibaliana na mkeo usikiuke...
 
Na nguruwe je ? mbona Biblia inasema kuwa "Nguruwe ni najisi kwenu.
Msiile nyama yao, wala msiiguse mizoga yao" ?

Biblia inasema hivi,

"Na nguruwe, kwa sababu yeye anazo kwato, ni mwenye miguu iliyopasuka kati, lakini hacheui, yeye ni najisi kwenu.
Msiile nyama yao, wala msiiguse mizoga yao; hao ni najisi kwenu." (Mambo ya Walawi 11:07-08)

Kumsema vibaya nguruwe ni uchochezi, hii kitu ni tamu iingizwe kwenye katiba mpya
 

Similar Discussions

12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom