Nimekula NYAMA YA MBWA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimekula NYAMA YA MBWA

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bujibuji, Jun 4, 2012.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Jun 4, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 22,007
  Trophy Points: 280
  Leo kwenye hangaika zangu za kutwa nzima nikaamua nirudi nyumbani.
  Mama watoto hakutaka nitoke hivyo basi akaniambia mechi ya Brazil Vs Mexico niiangalizie nyumbani.
  Nikakaa nyumbani nikiangalia mechi mwenyewe kama jini Njabagumu.
  Katikati ya mpira nikaona siinjoi chochote, nikaaga kuwa naenda kununua vocha dukani.
  Nikaingia taratibi baa ya jirani, nikaagiza Serengeti moja baridi sana, nikaipiga fasta kama mwanariadha aliyetoka kumaliza marathon akutanapo na jagi la maji. Haikunitosha niaagiza ya pili, kabla haijaja mara ghafla mama watoto akapiga simu "vp darling mbona unakawia?" ndio lililokua swali lake, nikamjibu niko na mwenyekiti wa mtaa tuna mazungumzo.
  Nikaagiza mbuzi, daima huwa napenda jembe (wataalam wa mbuzi wanaelewa ninachokiongea). Baada ya nusu saa ikawa mezani.
  Nikapiga kama vipande kumi, nikaagiza Serengeti nyingine ya baridi.
  Nikiwa katikati ya zoezi la pombe nyama, mara wakaingia Polisi wakiwa na sare zao na kuelekea jikoni.
  Huko wakawaweka chini ya ulinzi watumishi wote na kufanya msako mkali. Jikoni vimekamatwa vichwa viwili vya mbwa na ngozi mbili.
  Na t ayari mie nsha kula huyu kiumbe mlinzi jamani.
  KUlia nataka, kucheka nataka, najitapisha sitapiki.
  Kuweni makini wenzangu, yasije kuwakuta yaliyonikuta.
   
 2. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #2
  Jun 4, 2012
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  "Ningalijua huja mwisho wa safari", ulipopata wazo la kumdanganya my wife, ndio ulipopata fursa ya kuonja nyama. Hujasema mkuu ukilinganisha woo na mbuzi, nani zaidi
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Jun 4, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 22,007
  Trophy Points: 280
  Nilidhani mbuzi, sijaona tofauti. Sijui sababu y aile bia niliyopiga fasta???
   
 4. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #4
  Jun 4, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,131
  Trophy Points: 280
  Makalio ya sufuria hayaogopi moto. Nakushauri, endele kula tu hiyo nyama maadam haikudhuru
   
 5. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #5
  Jun 4, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Bweka tu mkuu
   
 6. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #6
  Jun 4, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwani ukila utakufa au? Endelea kupiga kitoweo hicho.
   
 7. SIMBA WA TARANGA

  SIMBA WA TARANGA JF-Expert Member

  #7
  Jun 4, 2012
  Joined: Feb 14, 2012
  Messages: 992
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kachome sindano ya kichaa cha mbwa,
   
 8. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #8
  Jun 4, 2012
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Nyama haramu ni ya mtu tu.
  Zingine zote ni halali.
   
 9. Mahmood

  Mahmood JF-Expert Member

  #9
  Jun 4, 2012
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 7,851
  Likes Received: 1,336
  Trophy Points: 280
  1) Umedanganya ulipo sema kuwa "naenda kununua vocha dukani"
  2) Umeenda sehemu ya haramu (baa)
  3) Umekunywa ulevi
  4) Ukadanganya tena kuwa "niko na mwenyekiti wa mtaa tuna mazungumzo"
  5) Kisha Ukalishwa nyama ya mbwa!!!

  Rafiki, nakushauri uache tabii hizo (mbaya) nne.
   
 10. Mahmood

  Mahmood JF-Expert Member

  #10
  Jun 4, 2012
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 7,851
  Likes Received: 1,336
  Trophy Points: 280
  Na nguruwe je ? mbona Biblia inasema kuwa "Nguruwe ni najisi kwenu.
  Msiile nyama yao, wala msiiguse mizoga yao" ?

  Biblia inasema hivi,

  "Na nguruwe, kwa sababu yeye anazo kwato, ni mwenye miguu iliyopasuka kati, lakini hacheui, yeye ni najisi kwenu.
  Msiile nyama yao, wala msiiguse mizoga yao; hao ni najisi kwenu." (Mambo ya Walawi 11:07-08)
   
 11. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #11
  Jun 4, 2012
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Ngamia vile vile ni haramu lakini sijasikia mtu akituambia tusile. Hivi mnaingia kigugumizi kumwita ngamia haramu kwa vile Arabuni ni kitoeo safi na muhimu???

  Nakumbuka 1998 pale Manzese aliletwa ngamia akachinjwa msikitini wacha watu wafaidi nyama. Wengi niliwasikia wakisema kula Camel ni Suna.

  Leviticus 11:4
  Nevertheless these shall ye not eat of them that chew the cud, or of them that divide the hoof: as the camel, because he cheweth the cud, but divideth not the hoof; he is unclean unto you.

  Patamu hapo.

   
 12. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #12
  Jun 4, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  unaonaje ikiaralishwa mzee!
   
 13. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #13
  Jun 4, 2012
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  huko ni wapi? arusha?
   
 14. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #14
  Jun 4, 2012
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,067
  Likes Received: 1,805
  Trophy Points: 280
  Duh.. kumbe... mbona wanakula hawa wenzetu
   
 15. Sniper

  Sniper JF-Expert Member

  #15
  Jun 4, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,944
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Nyama ya mbwa ni nzuri sana kiafya. Ukiwa unakula mara kwa mara hupatwi na magonjwa ya hapa na pale. Pande hizi za Asia tunakamua kwa kwenda mbele tu. Kawaida sana
   
 16. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #16
  Jun 4, 2012
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Pilipili usoila...wahenga are very wise.
   
 17. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #17
  Jun 4, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Biblia haijakataza kula mbwa bwana...
  Kitimoto ilihalalishwa na Yesu
   
 18. Mangimeli

  Mangimeli JF-Expert Member

  #18
  Jun 4, 2012
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  pole kwa kuinjoi kitoweo cha IR a.k.a mbuzi kucha.
   
 19. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #19
  Jun 4, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,866
  Likes Received: 6,218
  Trophy Points: 280
  toooooooooooooooba.......
  pole sana
   
 20. Tmlekwa

  Tmlekwa Senior Member

  #20
  Jun 4, 2012
  Joined: Apr 27, 2012
  Messages: 185
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  duh,lakin kaka umeionaje c tamu eeeh,halaf kama had leo hujaharisha au hujaona madhara yoyote bac mi nakushaur we endelea tu kula sbb mbwa hajakatazwa kuliwa na mwenyez mungu.
   
Loading...