Nimechoka kusubiri ajira za walimu

we unaesema kama n mwalm wa art hamna haja ya kusbl we ni nan, ingia tamisemi usome taarfa sio unakaa na kulopoka tu hum, ajira zipo kwa walimu wote japo kipaumbele n kwa walimu wa masomo ya sayansi but wote wanaajiliwa ,kama walimu wa art ni wengi mbona hapa shuleni kwetu tupo walimu wawil tu wa somo la kingereza acha kukatsha tamaa watu .
 
Mnaotuhukumu kama tulikuwa tuna penda anasa chuoni ni haki yenu ila mkumbuke tumetoka katika familia zenye viwango tofauti za kielimu,kiuchumi na hata kisiasa.Hivyo kuhitimisha kwa kutuita wapenda anasa si vema bali mje na suluhu la tatizo mfano mimi binafsi nimemaliza chuo nilikuwa na 1.9milion kwenye akaunt yangu ya bonus NMB .changamoto nikaanza kuzipata kwa miradi niliwekeza mfano nilinunua kuku mikoo 15, jogoo 1, banda nilitumia zaidi ya 270000 kuku walizaliana .nikafuata taratibu zote za chanjo lakini huwezi amini ugonjwa ukaingia vifaranga vikafa nikajitahidi kutumia madawa tofauti wakasalimika 25 kati ya 129 na mikoo 8 wakafa kwa ugonjwa pamoja na jogoo.nikaingia plan ya pili nikalima hekari 3 nikapanda mbaazi tatizo bei kg 1@700 garama nilizotumia nimeingia losi kubwa maana mwaka jana watu waliuza 2000 kwa kg 1. sasa hivi nimebakiwa na 450000 out of 1.9milion .niliyotoka nayo mlimani.Hivyo kwa wale mnaotushauri mje na suluhisho ambalo mtadadavua fursa ya shughuli husika na changamoto zake .asanteni
 
Nililima,nilipiga vibarua then kidogo nikajimudu katika mambo kadhaa,tatizo lilianza waliposema bungeni ajira wa 5,nikapiga chini,mara nkajikuta kale ka 1.8Mil nakatumia huku nikijipa matumaini.mara vuuu tamko la kustisha ajira kwa muda wa miezi miwili,afu nkawa kama nimepakwa mafuta ya fisi gundu kila kukicha,mara baba anaumwa afu mi ndo nategemewa,mara wadogo zang wa3 wanaoishi hostel za shule ya kata wanadaiwa mchango wa hostel na chakula.nyie mnaotupuuza tambueni sisi wengine ni walezi wa familia zetu
 
Nimekuwa kufarijiwa kwa muda mrefu kuwa nivumilie ajira za walimu zitatoka mapema. Ila sasa mpaka nimekata tamaa maana wanasiasa ni kawaida yao maneno mengi mwaka unaisha tunaingia mwaka mwingine mambo hayaelewiki.

Mtaani kunachosha yaani daah hata sijui
tulia tu afadhali hata nyie mna uhakika one day yes,,,, wengine hata hatujui kama zitatoka
 
kuna watu wanarahisisha maisha wanasema nenda private, jamani private wamejaza mabarua kibao ya graduates wetu si kwamba wajafika huko private, private bado msaada ni mdogo ukilinganisha na serikarin.
Tution zenyewe mtoto wa kitanzania unamwomba hata bure umfundishe ili afaidike yeye na ndugu zake lakin babo hata iyo bure haji kusoma, hapo tufanyaje.
 
Korasi ya haitazidi miezi miwili imeisha expire tunasubiri nyingine tuje tuimbe na kuicheza kwa sababu tunaendeshwa kwa matukio na sololist atautema mda si mrefu
 
Kadiri mwezi wa nane unavyoelekea kuisha kauli ya Rais ya haitazidi miezi miwili ndiyo inanifanya nimshangae His excellency
 
Back
Top Bottom