Nimechanganyikiwa na Simu ya mtarajiwa wangu

Nimechanganyikiwa na Simu ya mtarajiwa wangu

Mkuu mbona kama kuna pupa ya ndoa hapo,wakati MTU anasafari!
Unajua atarudi lini?kwanini asisubiriwe arudi!

Hakuna pupa mkuu hapo
Atarudi baada ya mwezi


Sent from my iPad Air using JamiiForums mobile app
 
heee kumbe hamkuchangisha hata watu, hamkukodi hata ukumbi, hakuna gharama za before, au kwenu cost sio ishuuuu

Hakuna ukumbi baada ya ndoa kesho yake ni tafrija tu nyumbani (sehem inatosha)
By the way kama familia hivyo vitu wanaweza kua afford so, hakuna mchango kwa jamaa!


Sent from my iPad Air using JamiiForums mobile app
 
Ila wewe kijana, usipoangalia utafanywa bush.oke wa milele.


Yaani mkeo umuoe afu asafirishwe na baba mkwe kwenda kutunza mke wa mwingine? Sijui kile kipindi cha fungate wewe unapiga nyeto??

Mzazi hutunzwa na mama yake au mama mkwe wake waende wao. Oa mkeo kwa jinsi utakavyo na akae kwake atulie period!

Hebu niazimishe nikuolee huyo bi dada hadi decemba, nataka nikunyooshee ukweni kidogo.

WAKUU TUMESHAFIKIA TAMATI YA KIKAO...
BABA MKWE KAPIGIWA SIMU NA WASHENGA KUWA WANAHITAJI KUONANA NAE KWA MAZUNGUMZO ZAIDI NA KATOA UDHURU YUKO SAFARINI ILA BY THE DAY AFTER TOMORROW ATAKUWA AMESHARUDI KWAHIYO WAKAONANE SIKU YA ALHAMISI SAA 10 JIONI NYUMBANI KWAKE....

MAAZIMIO YA KIKAO NI:-
Tulivyoafikiana swala la kughairisha ndoa halipo na haliwezi kukubalika (kwasababu sisi waoaji ndio tuliopanga siku ya ndoa na kama kughairisha ni sisi) kama swala la kwenda na kurudi ni kuwa tufunge ndoa kuhusu mambo mengine Sherehe sijui na nini huko yaje baadae,,ya huo mwezi atakao rudi. After all sisi ni Waislam wote hakuna haja ya kufanya Jambo liwe kuuubwa hadi lini sijui kwani kuna inawezekana hata siku ile tuliyopeleka mahari nikafungishwa ndoa kabisa kwa mujibu wa dini inavyosema!!


Sent from my iPad Air using JamiiForums mobile app
 
Ila wewe kijana, usipoangalia utafanywa bush.oke wa milele.


Yaani mkeo umuoe afu asafirishwe na baba mkwe kwenda kutunza mke wa mwingine? Sijui kile kipindi cha fungate wewe unapiga nyeto??

Mzazi hutunzwa na mama yake au mama mkwe wake waende wao. Oa mkeo kwa jinsi utakavyo na akae kwake atulie period!

Hebu niazimishe nikuolee huyo bi dada hadi decemba, nataka nikunyooshee ukweni kidogo.

Nikishaoa haendi popote mkuu labda anitoroke..
Teh teh teh nikuazimishe mtarajiwa tena mkuu?


Sent from my iPad Air using JamiiForums mobile app
 
Mwanasheria wangu na msomi EMT , ukiondoa hizi dini zilizoletwa na meli/ndege. Kiafrika zaidi, mtu akishatoa mahari na kukubalika, mwali anakuwa hajaolewa?

Kama mleta mada ametumbukiza hoja yake kwenye dini..... hizi dini zinakubalije mahari?? Ni ahsante kwa mzazi au mhuri wa ndoa??

Ukiondoa hizi dini za kuja, implications za mahari zinatofautiana kati ya kabila na kabila. Mfano, kuna makabila mengine yanataka mahari kubwa hiyo mpaka MCHUNGUZI HURU alishapendekeza kuwa ziwe zinakatwa kodi ya TRA. Kongosho akashauri kuwa "Mahari ngombe 100, TRA wanapewa ng'ombe 18."

Lakini kama SMU alivyosema kwenye ile thread kuu ya "Mahari na Nafasi yake Katika Ndoa", traditionally "
Baada ya ukoo wa mwanaume kutoa mahari na ukoo wa mwanamke kuikubali na kuipokea, mwanamke anakuwa mali halali ya ukoo wa mwanaume. Ndio maana hata mwanaume akifa mwanamke alikuwa anarithiwa (kama mali nyingine!) ili kama bado kijana aendelee kuongeza ukoo pamoja na kufanya kazi. Hawezi kuolewa na mwanaume kutoka ukoo mwingine (kama ilivyo mali nyingine haziwezi kurithiwa na watu baki!)."

Kama Kiranga alivyosema kwenye uzi huo huo "Ukitaka kui address hii issue usianzie na mahari, anza na concept nzima ya kuoa." Na SMU akaongezea kuwa "Dhana ya 'kuoa' pia inapungua na tunaelekea zaidi kwenye 'kuoana'!"

Inawezekana mahari bado ikawa muhimu kwa wale wanaoamini katika kuoa na kuolewa lakini isiwe vile kwa wale wanaoamini kuoana. FaizaFoxy atawafafanulia tofauti kati ya "kuoa" au "kuolewa" na "kuoana".

Kwa msaada wa
https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/229694-mahari-na-nafasi-yake-katika-ndoa.html



 
Ujumbe????

eti mlivoniwowa bado mdingi alikuwa na maamuzi kuhusu ratiba zangu?
ujue moja ya maamuzi ya kikao walichojipanga kumpa maazimio baba mkwe eti wawowe af binti aende USA ,baba mkwe atagharamia safari kama kadawia!of coz tarehe ya kurudi atapabga yeye!
 
Mkuu EMT mambo ya kiislam naxhelea kuyasemea maana ni mbumbumbu kabisa wa taratibu hizo..mi nimeassume mketa mada ni mfuasi wa taratibu za kimila tu kwenye kuoa...

Kama kuna conflict kati taratibu za kimila na dini ipi ina-prevail?

Maana upande mmoja unaweza ku-rely kwenye mila na mwingine kwenye dini.
 
Hili nalo neno atii....


Labda chozi la yule binti alokataliwa na wazazi wako ndo linalipwa, na wewe unakataliwa na wazazi wa mtarajiwa wako...labda Karma...

Ila tuliza moyo, kama ndoa ipo ipo tu, hata aende wapi...atarudi.
 
Kama kuna conflict kati taratibu za kimila na dini ipi ina-prevail?

Maana upande mmoja unaweza ku-rely kwenye mila na mwngine kwenye dini.

Apo mkuu EMT inategemea na imani ya mtu imelalia wapi..kama kwwenye mila kama mimi na Asprin basi mila na iheshmiwe na watu wote. Lakini nilivomsoma apo juu naona mila inaelekea kushinda maanaa washenga wameitwa
 
Last edited by a moderator:
Pole sana, hapo hakuna ndoa, inaonekana wazazi wa huyo binti, hawataki umuoe binti yao, haina logic, aende safari ya mbali wakati amebakza mwz mmoja tu.Jipe moyo kua makini katka matumizi ya pesa za michango itakugharimu. Nnachojua mimi ni kwamba ndoa nzuri ni ile iliyopata kibali kwa wazazi wa pande zote, vinginevyo huko mbele, itakua ni shida. Ngumu kumeza lakini ndo dawa
 
Yaani unashindwa kuwaambia wazasi wako ambao wana influence kwa wakwe zako unakimbilia kutuambia hapa?

Kwa kifupi wazazi wa mtarajiwa wanakudharau na hiyo ndoa wataiongoza kwa remote.
Au hawakutaki?

Huu ndo muda wa kuonesha uanamme wako.

Mi like zat! excellent opportunity
 
Ila wewe kijana, usipoangalia utafanywa bush.oke wa milele.


Yaani mkeo umuoe afu asafirishwe na baba mkwe kwenda kutunza mke wa mwingine? Sijui kile kipindi cha fungate wewe unapiga nyeto??

Mzazi hutunzwa na mama yake au mama mkwe wake waende wao. Oa mkeo kwa jinsi utakavyo na akae kwake atulie period!

Hebu niazimishe nikuolee huyo bi dada hadi decemba, nataka nikunyooshee ukweni kidogo.

pamoja na upoyoyo wa huyu ila pia inaonekana familia ya huyo mwanamke ni kichomi, inawezekanaje wamtume binti yao kwenda mtunza mtoto wao mwingine? kwani kazi ya mama mtu, kama huyo dada huko nje hana mkwe ni ipi?
 
Mahusiano ya siku hizi yamekuwa pasua kichwa kweli kweli na wa mashaka mashaka tu!
 
Labda kwa mwanasheria wetu EMT, endapo huyo binti akichomokea ughaibuni na ndoa ikashindikana, dogo na familia yake wanaweza kudai fidia kutoka kwenye familia ya msichana?

Labda tuanze kwa kuangalia Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 inasemaje. Kwanza ina-define mahari as "means any payment of stock, goods, money or other property made or promised in consideration of an intended marriage". Kwa hiyo kutoa mahari inaweza kuwa consideration kwa promise ya kuoana.

Then, kifungu cha 69 (Right to damages for breach of promise of marriage) kinasema kuwa "A suit may be brought for damages for the breach of a promise of marriage made in Tanzania whether the breach occurred in Tanzania Tanzania or elsewhere, by the aggrieved party or, where that party is below the age of eighteen years, by his or her parent or guardian".

Hata hivyo, kifungu hicho kinaendelea kusema kuwa "no damages shall be awarded in any such action in excess of loss actually suffered as a result of expenditure incurred as a direct result of the promise." Kwa hiyo, itambidi mlalamikaji aonyeshe kuwa ame-suffer loss kutokana na breach of the said promise.

Kifungu hiki kinasisitiza kuwa "No suit shall be brought for specific performance of a promise of marriage." Kwa maana nyingine kama kuna breach of promise of marriage, mlalamikaji hawezi kumlazimisha mlalamikiwa waoane.

Kifungu za 70 kinasema malalamiko lazima yaletwe mahakamani ndani ya mwaka mmoja baada ya hiyo breach ifanyike. Kama kuna watu ambao walishatoa zawadi zao, kifungu cha 71 wanaweza kufungua mashtaka kuzidai kama ndoa haitafungwa.

Lakini mlalamikiwa anaweza kiji-defend kuwa kuna sababu halali ambazo zimemfanya a-breach hiyo promise. Baadhi ya sababu ni kama mlalamikaji alimdanganya kwenye masuala fulani kama maisha ya mlalamikaji, fraud, tabia ya mlalamikaji, nk.

Hizi sheria ni za zamani sana na nchi nyingi zimeamua kuzifutilia mbali lakini bado zipo kwenye vitabu vya sheria za Tanzania.
 
Back
Top Bottom