Ahsante sana mkuu
EMT,
Kwangu mimi, hayo ndiyo makubwa kuliko gharama za pesa....
Unajua watu wengine tunapoamua kufanya kitu, tunafanya kweli na siyo kujaribu jaribu. Kwa hiyo inapotekea mtu akavunja ahadi basi damage inakuwa kubwa kiasi kwamba kuiweka au kuithaminisha (quantify in monetary terms) inakuwa ni vigumu.
Naamini hata sheria zetu zitakuwa na nafasi ya kumwangalia mwathirika katika mrengo huo!
Nakubaliana na wewe. Kwa upande moja engagements nyingi sana zinavunjika kila mwaka. Nyingine zinakuwa very expensive kwa kweli. Kwa upande mwingine, wengine wanakandia sheria za kudai fidia kwa kuvunja uchumba kwa sababu mbalimbali.
Mfano wanadai kuwa mtu awe huru kuvunja uchumba bila kuogopa kuwa anaweza kushtakiwa. Wengine wanadai hizi sheria ziko bias kwa faida ya mwanamke. Pia wanadai hizi sheria zimepitwa na wakati kwa sababu fidia inaangaliwa kama vile ndoa ni biashara inayohusisha mali.
Lakini zipo circumstances ambazo naona ni haki kwa mlalamikaji kudai fidia. Kwa mfano kuna kesi moja ambapo mahakama iliamua kuwa ilikuwa haki kwa mlalamikaji kupewa fidia, baada ya mlalamikiwa kum-promise mlalamikaji kuwa angemwoa kama angehamia (yaani mlalamikaji) nchi nyingine aliyokuwa anaishi mlalamikiwa. Hapo imagine kama mwanamke alihama akaacha kazi, n.k, then hapo anaweza kuwa na haki ya kudai fidia.
Hapo kinachoangaliwa ni matendo ya wahusika. Imagine mmeshapanga tarehe ya ndoa, nguo za harusi zimenunuliwa, ukumbi na sehemu ya honeymoon imeshaandaliwa, wageni wameshaalikwa, halafu siku ya siku mwanaume hatokezei bila sababu za msingi. Surely, this jilted woman should be entitled to some sort of compensation.
Hata hivyo, inadaiwa kuwa moja ya sababu ya nchi nyingi kuamua kuifuta hii sheria ni kutokama na wanawake wa kima cha chini kuitumia kama njia ya kujitafutia pesa. Kumbuka wakati huo wanawake walikuwa hawafanyi kazi. Halafu fidia ilikuwa kubwa kweli kweli. Mfano mwaka 1881 kuna mwanamke alipewa fidia ya £500 ambayo ni karibu £51,500 kwa sasa. Fidia ilikuwa zaidi ya kipato cha mwaka cha mwanaume husika.
Mwaka 1900, kuna mwanamke mjane alimtrick mwanaume mmoja na kuwa mchepuko wake. Mwanaume alimdanganya mwanaume kuwa hajawahi kuolewa. Baada ya njia kuu kufariki, mwanaume akawa anamwambia mchepuko kuwa atamwoa lakini akawa anahairisha kila mara. Baada ya kuzaa nae, mwanaume akageuka na kudai kuwa mpango wake ulikuwa ni kuoa mwanamke tajiri. Mchepuko akamshtaki mahakamani kwa kuvunja ahadi ya kumwoa na kufanikiwa kupata fidia ya £4,000 ambayo kwa sasa ni karibu £417,000!- Chanzo:
Breach of Promise to Marry: A History of How Jilted Brides Settled Scores by Denise Bates
Of course, wapo baadhi ambao kweli walikuwa wanataka kulipwa fidia kwa kupoteza fedha na muda, with others for broken hearts. Pia kulikuwa na belief kuwa hakuna anayeweza kumwoa mwanamke aliyeachwa.
Lakini kwa karne hii ambayo elimu na ajira imeongezeka kwa wanawake, sidhani kama bado wanawake wanahitaji kutegemea maisha yao kwa mwanaume, though kwa hapa kwetu utegemezi bado upo sana. Pia wanaume wa siku hizi wanaoa au kutembea na wanawake waliochwa bila wasiwasi, though kwa maeneo ya vijijini bado ni shida.
Hivyo hizi ni baadhi ya sababu ambazo zimechangia sheria hii kupigwa stop kwenye nchi mbalimbali. Mkoloni wetu alifuta sheria hii mwaka 1971. Coincidentally, huu ni mwaka ambao sheria yetu ya ndoa ilipitishwa na bunge letu tukufu na kuweka kifungu cha kudai fidia for breach of a promise of marriage.