The Fishport Prince
Senior Member
- Sep 25, 2023
- 135
- 304
Baada ya kumchunguza mke wangu Kwa muda mrefu nimegundua kazi za nyumbani yaani chores zinamchosha na kupelea kuwa na hasira zisizo na msingi mara Kwa mara.
Hivyo nimeanza utaratibu wa kufanya kazi za ndani hasa juma mosi na jumapili ambapo siendi kazini.
Leo niliamka saa kumi na moja alfajiri, maza house kuamka kakuta kamba zimejaa nguo zangu, zake na za watoto.
Mtori wa watoto upo kwenye chupa na chai yetu pia ipo tayari.
Kwa kweli nimeona jinsi mama watoto alivyoamka Kwa bashasha!
Rai yangu Kwa wanaume tufanye kazi za nyumbani kama sehemu ya majukumu hasahasa kipindi hiki ambacho binti wa kazi hawakai.
Hii pia itasaidia kuwavuta watoto wajue wewe kama baba umewahangaikia.