Nimeanza maisha mapya kama Vegan

Nimeanza maisha mapya kama Vegan

Habari 👋🏾

Siku ya leo nikiwa natimiza miaka kadhaa nimekuwa VEGAN rasmi. Hatua hii nimekwisha ianza muda toka 28 January, hivi sasa naendeleza nadhiri hii rasmi katika mfumo wa maisha yangu.

Nimekuwa nikijiuliza utajiita vipi mwenye upendo, heshima au mtu unayejali hisia na kuheshimu wengine ikiwa umeshindwa kuheshimu uwepo wa viumbe wengine kama wanyama, ndege na wengineo?

Kwa kujali na kuona umuhimu wa kila kiumbe nimekuwa nikivijali viumbe vyote mfano, huwatengea waramba sukari kiasi chao pasi ya kuwapatia bugdha, uhifadhi mayai ya kuku na kutotoa wengine kuendeleza uzao wao, hutembea na wanyama mbalimbali katika maeneo kadhaa waweze kijihisi umiliki nk.

Leo nimepanda miti 28 maeneo yayonizunguka na miti 21 maeneo ya umma katika shule 2, hospitali, eneo la jeshi, kituo cha wasiojiweza na watoto waishio mazingira hatarishi na katika ofisi za wilaya.

Nikiwa kama kijana anayezingatia maisha halisi leo ni wazi sitotumia tena bidhaa zinazotokana na wanyama na viumbe mbalimbali. Hili linaambatana na masuala kadhaa katika mfumo wangu wa maisha ninaoendelea kuufuata ikiwa ni pamoja na;-
  • Sishiriki mapenzi (Sex)
  • Situmii vinywaji kemikali (Processed Drink's)
  • Situmii bidhaa zenye sukari ongezwa (Candy's)
  • Situmii bidhaa zinafanywa majaribio kwa wanyama
  • Nimejiweka mbali na uovu na negativity ya aina yoyote
  • Sifungamani na upande wowote
Najihisi mwenye furaha na amani, najiona mshindi. 😊

Sergio
hutoshiriki mapenzi? ina maana hutooa/kuolewa?
 
Mkuu hapo kwenye kutokusex naona kama hutendi haki ikiwa unashiriki kupanda miti kwa maana ya kuweka mwendelezo wa uhai/existance ya hivyo viumbe, meanwhile kusex ndo kunafanya mwendelezo wa uwepo wa binadam duniani.

Mwisho. Tukupe muda gani wa kutangazwa kuwa bilionea?! Make umechagua kujitenga na anasa zote za dunia, so obviously savings lazima iwe kubwa
 
Nimejitahid wee wapi zamn nilikua nakunywa had 3. Since corona ije nakunywa 1. Coca ya baridi ni kitu kingine jamani.
Hauna kitambi mkuu? Mara nyingi wanaokunywa sana soda wanatengeneza vitambi vya ajabu, manyama ya tumbo yale kushoto na kulia (love handle).

Mishikaki haina tatizo !

Ila soda acha kabisa Mkuu....kiwango cha sukari unachokiongeza sio vizuri, usiendekeze inawezekana, jali afya yako kama unavyojali kutafuta pesa 😂
 
Nakutamania, maisha mazuri hayo ila usijinyime sana ukatenda dhambi..mie nisipokula nyama 3dys roho hua inataka kutoka!

Soda nisipokunywa Coca sifanyi kitu nakua zoba.

Hapa niko sehem nasubiria mishikaki kwanza.

All the best
Yaani nimesoma mishikaki tayari nimeshaitamani hiyo mishikaki yako[emoji3]
 
Hauna kitambi mkuu? Mara nyingi wanaokunywa sana soda wanatengeneza vitambi vya ajabu, manyama ya tumbo yale kushoto na kulia (love handle).

Mishikaki haina tatizo !

Ila soda acha kabisa Mkuu....kiwango cha sukari unachokiongeza sio vizuri, usiendekeze inawezekana, jali afya yako kama unavyojali kutafuta pesa 😂
Bahati nzuri mie sinaga manyama uzembe...hayo malove handle mie sina...sema kakitambi kakuonesha katumbo kapo! Toka asbhbsijanywa coca..imebid niitafte nw akili itulie nataman kuacha sema sina substute...
 
Yaani nimesoma mishikaki tayari nimeshaitamani hiyo mishikaki yako[emoji3]
Hahhahahaa....! Muone..mishikaki jaman ni habar nyingine..nachomaga wknd uwiii naiwekea spices inakua laini..napika na ugali .hiyo huwa saa4 tu asbh....unashushia na wine..ah acha kbs
 
Hutaacha! Utakuwa unasogeza siku tu za kuanza rasmi, mpaka siku ya mwisho.

Mimi kuku wa kuchoma nimegundua sitaweza Acha kula hata vipi.
Kwa upande wangu sifahamu madhara ya kuku wa kuchoma,
Ila soda na juwa inachangia kupngeza uzito wa mwili sana , pamoja na sukari.

Naomba utupe experience kuna madhara yoyote unayapata ukila kuku wa kuchoma?
 
Mimi niache kula Kuku au mdudu alivo mtamu vile...
Hongera baba maisha ni kuchagua.
 
Kwa upande wangu sifahamu madhara ya kuku wa kuchoma,
Ila soda na juwa inachangia kupngeza uzito wa mwili sana , pamoja na sukari.

Naomba utupe experience kuna madhara yoyote unayapata ukila kuku wa kuchoma?
Mimi jamani soda kuongezea uzito mbona Sioni maana am constant kwenye uzito na mnywaji wa soda almost 3-5 per week but uzito wangu uko constant nikiongezeka labda ni ½kg tena after months but for four better years uzito wangu unarange tu vizuri na chips nakula sana tu...
Labda kwasababu ni mpenzi mno wa vegetables
 
Hahhahahaa....! Muone..mishikaki jaman ni habar nyingine..nachomaga wknd uwiii naiwekea spices inakua laini..napika na ugali .hiyo huwa saa4 tu asbh....unashushia na wine..ah acha kbs
Mate yamenijaa dada...na hii mvua ya Dar mishkaki na ugali wa motoooo na kikachumbari chako
 
Hongera,
Kuna vitu nataka niachane navyo kabisa ila kwa wakati fulani natumia japo kwa kiasi sana kutokana na mazingira
[emoji736]Soda naweza kumaliza hata miezi sita sijanywa,nakunywa napolazimika tu
[emoji736]Nina miaka mingi situmii majani ya chai/kahawa
[emoji736]Nataka niachane kabisa na sukari ya kiwandani ila sijapata mbadala kwa hio natumia japo kwa kiwango kidogo sana
[emoji736]Natamani niache kunywa dawa za viwandani nitumie herbs tu japo bado nakumbana na vikwazo fulani.

Hili la kuachana kabisa na sukari kama kuna mtu kafanikiwa atuambie amewezaje?
Hapo kwenye sukari ya kiwandani- unaweza kutumia ASALI...

Punguza vyakula vya Wanga , kula zaidi protein..

Anza maisha ya mazoezi.. na utayazoea tu japo mwazo mgumu
 
Mimi jamani soda kuongezea uzito mbona Sioni maana am constant kwenye uzito na mnywaji wa soda almost 3-5 per week but uzito wangu uko constant nikiongezeka labda ni ½kg tena after months but for four better years uzito wangu unarange tu vizuri na chips nakula sana tu...
Labda kwasababu ni mpenzi mno wa vegetables
Mkuu huwa unakula vyakula vya wanga kwa wingi , kama ugali, wali, mikate n.k?

Inawezekana upo kwenye blood group lisilo athiriwa sana na matumizi hayo ya sukari,

Maana wataalamu wa lishe huwa wanapendekeza aina za vyakula kutegemeana na blood group ya mtu!
 
Mimi jamani soda kuongezea uzito mbona Sioni maana am constant kwenye uzito na mnywaji wa soda almost 3-5 per week but uzito wangu uko constant nikiongezeka labda ni ½kg tena after months but for four better years uzito wangu unarange tu vizuri na chips nakula sana tu...
Labda kwasababu ni mpenzi mno wa vegetables
Vegetables zinakubeba....mie nimeadd weight zaidi ya 20kgs...najiangalia tu nabak nasema nhiiii....wiki zima natumia public transport nasaga lami balaa nasweat balaa
 
Back
Top Bottom