Nimeanza maisha mapya kama Vegan

Nimeanza maisha mapya kama Vegan

isajorsergio

Platinum Member
Joined
Apr 22, 2018
Posts
4,144
Reaction score
6,563
Habari 👋🏾

Siku ya leo nikiwa natimiza miaka kadhaa nimekuwa VEGAN rasmi. Hatua hii nimekwisha ianza muda toka 28 January, hivi sasa naendeleza nadhiri hii rasmi katika mfumo wa maisha yangu.

Nimekuwa nikijiuliza utajiita vipi mwenye upendo, heshima au mtu unayejali hisia na kuheshimu wengine ikiwa umeshindwa kuheshimu uwepo wa viumbe wengine kama wanyama, ndege na wengineo?

Kwa kujali na kuona umuhimu wa kila kiumbe nimekuwa nikivijali viumbe vyote mfano, huwatengea waramba sukari kiasi chao pasi ya kuwapatia bugdha, uhifadhi mayai ya kuku na kutotoa wengine kuendeleza uzao wao, hutembea na wanyama mbalimbali katika maeneo kadhaa waweze kijihisi umiliki nk.

Leo nimepanda miti 28 maeneo yayonizunguka na miti 21 maeneo ya umma katika shule 2, hospitali, eneo la jeshi, kituo cha wasiojiweza na watoto waishio mazingira hatarishi na katika ofisi za wilaya.

BLU Cess 20212801.jpg

Nikiwa kama kijana anayezingatia maisha halisi leo ni wazi sitotumia tena bidhaa zinazotokana na wanyama na viumbe mbalimbali. Hili linaambatana na masuala kadhaa katika mfumo wangu wa maisha ninaoendelea kuufuata ikiwa ni pamoja na;-
  • Sishiriki mapenzi (Sex)
  • Situmii vinywaji kemikali (Processed Drink's)
  • Situmii bidhaa zenye sukari ongezwa (Candy's)
  • Situmii bidhaa zinafanywa majaribio kwa wanyama
  • Nimejiweka mbali na uovu na negativity ya aina yoyote
  • Sifungamani na upande wowote
Najihisi mwenye furaha na amani, najiona mshindi. 😊

Sergio
 
Hivi miti na mimea si ni viumbe hai navyo mkuu? Huvionei huruma navyo? Kwanini unakula mchicha au spinachi wakati ili uukule lazima uuchume (Ndio kuua kwenyewe huko)?

We jilie tu vyote vinavyoruhusiwa ila mengine fanya kama ulivyoamua.

Nje ya mada, hautashiriki sex ndio kusema hautaoa wala nini? Vipi puchu?
 
Nakutamania, maisha mazuri hayo ila usijinyime sana ukatenda dhambi..mie nisipokula nyama 3dys roho hua inataka kutoka!

Soda nisipokunywa Coca sifanyi kitu nakua zoba.

Hapa niko sehem nasubiria mishikaki kwanza.

All the best
 
Hivi miti na mimea si ni viumbe hai navyo mkuu? Huvionei huruma navyo? Kwanini unakula mchicha au spinachi wakati ili uukule lazima uuchume (Ndio kuua kwenyewe huko)?

We jilie tu vyote vinavyoruhusiwa ila mengine fanya kama ulivyoamua

Nje ya mada, hautashiriki sex ndio kusema hautaoa wala nini? Vipi puchu?
Mimea ni viumbe hai vyenye kuwezesha uhai, kuunganisha asili ya maisha yetu ya kila siku na ndio sababu ya kutumia mimea.
 
Back
Top Bottom