Nimeanza Biashara ya Kukopesha, naomba ushauri

Ramon Abbas

JF-Expert Member
May 4, 2021
1,964
3,900
Habari za asubuhi JF people?

Mimi ni Dalali wa Viwanja Magari Nyumba & Co. Kuna pesa huwa naipata gjafla kutokana na shughuli zangu za u middle Nimeamua kuanza kukopesha.

Watu ninaoanza nao ni waaminifu sana nawafahamu. Kwa kuanza tu nimeamua kuwapa mkopo wa masharti haya:
  • Kwa kila shilingi elfu 10, irejeshe Sh 500 kila siku.
  • Mkopo utakaa siku 14.
Jana nimetoa elfu 40, after two weeks ilete Riba ya Tshs 28,000

Je, nipo sahihi au najiumiza kwa kiwango nilichoweka?

Je, nikipandisha kwa kila elfu 10 izae buku kila siku nitakosea?

Note:
Mteja wangu ni mama ntilie
 
Je nikipandisha kwa kila elfu 10 izae buku kila siku nitakosea?
Kwa wadau wanao kopesha, huwa wanafanya 3,000 au 4,000 kwa kila 10,000 , Ila hii ni kwa mwezi mmoja, na sio kwa siku kama ilivyo wewe.

Ila kwa kuwa umeanza na 500 kwa siku, ni vyema ukabakia hapo, kwenye hicho kiwango, sio uongeze.
Kwa kila shilingi elfu 10, irejeshe Sh 500 kila siku.
Yaani hapo ulichofanya ni riba ya asimilia 100, kwa siku 20 za kazi katika mwezi, kwa mtu aliyechukua 10,000.

For long run, hii kibiashara haiko sawa.
 
Kwa hatua za awali na pesa ndogondogo bado hakuna shida na uko salama..lakini jitahidi ujisajili na kupata nyaraka husika ila riba itakuwa sio hiyo bali ile ya mwongozo wa bank kuu

Ukiendelea bila nyaraka kuna wajuzi watakopa ndefu na hawatarejesha na hutakuwa na cha kuwafanya kisheria labda uwaroge
 
Kwa hatua za awali na pesa ndogondogo bado hakuna shida na uko salama..lakini jitahidi ujisajili na kupata nyaraka husika.. Ila riba itakuwa sio hiyo bali ile ya mwongozo wa bank kuu
Ukiendelea bila nyaraka kuna wajuzi watakopa ndefu na hawatarejesha na hutakuwa na cha kuwafanya kisheria labda uwaroge
Asante sana mkuu kwa ushauri wako

Hii biashara kweli haina nyaraka na ni rahisi kutapelika ukikopesha watu wasiowaaminifu

mimi niliwahi kuifanya kipindi cha nyuma lakini sikuwa serious na ilidum kwa miezi miwili tu.

nilichokuja kugundua, hawa kina mama walioko kwenye vikundi ni wakopaji wazuri na wanaweka bondi vitu vyao vya thamani na ni warejeshaji wazuri sana

Pia nilikuwa nakopesha watu wenye makazi ya kudumu na wenye kipato/mshahara mwisho wa mwezi.

Kwa kifupi nilifanya vetting kali sana kwa watu niliokuwa nawakopesha
 
Omba usikopeshe wanasheria
Kuna mtu aliwahi kunishauri kwamba kama nakopesha basi niandikishane na mtu kwamba nilimsaidia sio nilimkopesha kwa sababu sina usajili

mfano, kama nakopesha elfu 40, rejesho ni 28,000 jumla 68,000 in two weeks

basi tuandikishane kwamba nimekusaidia elfu 68,000 umpeleke mtoto hospitali kisha utazirudisha baada ya wiki 2😅😅😅
 
Asante sana mkuu kwa ushauri wako

Hii biashara kweli haina nyaraka na ni rahisi kutapelika ukikopesha watu wasiowaaminifu

mimi niliwahi kuifanya kipindi cha nyuma lakini sikuwa serious na ilidum kwa miezi miwili tu.

nilichokuja kugundua, hawa kina mama walioko kwenye vikundi ni wakopaji wazuri na wanaweka bondi vitu vyao vya thamani na ni warejeshaji wazuri sana

Pia nilikuwa nakopesha watu wenye makazi ya kudumu na wenye kipato/mshahara mwisho wa mwezi.

Kwa kifupi nilifanya vetting kali sana kwa watu niliokuwa nawakopesha
Wahitaji ni wengi ifanye official uwe na kinga likitokea tatizo
 
Kuna mtu aliwahi kunishauri kwamba kama nakopesha basi niandikishane na mtu kwamba nilimsaidia sio nilimkopesha kwa sababu sina usajili

mfano, kama nakopesha elfu 40, rejesho ni 28,000 jumla 68,000 in two weeks

basi tuandikishane kwamba nimekusaidia elfu 68,000 umpeleke mtoto hospitali kisha utazirudisha baada ya wiki 2
Hii nzuri
 
Unakabidhi mtaji wako kwa watu, subiri muda kidogo utajua hujui. Bora ufungue genge ufanye biashara za kawaida. Sikia kukopesha, Mkopaji anaweza akaingia mkatabata wowote unaomnyonya ili mradi tu aipate hiyo ela, akishaipata utasubiri.
Business ni risk taking mkuu.

niambie Biashara isiyo na risk ama mikopeshano nikaifanye
 
Back
Top Bottom